Quantcast
Channel: DUNIA KIGANJANI BLOG | Ifanye Dunia Kuwa Yako
Viewing all 2674 articles
Browse latest View live

TASWIRA MBALIMBALI ZA RAIS MAGUFULI NA RAIS KAGAME WAKIWA NCHINI RWANDA


WATU WATANO WAFARIKI DUNIA JIJINI DAR KWA KUANGUKIWA NA KIFUSI.

$
0
0

Watu watano wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa, baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuangukiwa na kifusi na mti wakiwa wamelala, ajali hiyo ilisababishwa na kupasuka kwa karo la majitaka la nyumba ya jirani iliyo juu ya mlima.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alisema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa karo hilo na kwamba maji yaliyotoka kwa kasi yaling’oa mti, kifusi na kisha kuifunika nyumba ya jirani iliyojengwa bondeni na kusababisha vifo hivyo.

Alisema tukio hilo lilitokea jana alfajiri katika Mtaa wa Ukwamani Kata ya Kawe jijini Dar es Salaam, na waliokufa ni Ephraim Manguli (47), watoto wake Daniel Ephraim (5) na Frederick Ephraim (1). Wengine ni mjukuu wa mwenye nyumba hiyo, Greyson Clarence (3) pamoja na msichana wa kazi za ndani aliyetambulika kwa jina moja la Maria.

“Majeruhi ni pamoja na Emilia Nakiete (19) aliyejeruhiwa mkono wa kulia na kidevu na Fadhili Fariji (8) aliyejeruhiwa mguu wa kulia. Wengine watatu walitibiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na kuruhusiwa. Majeruhi wawili bado wamelazwa na miili ya marehemu imehifadhiwa hospitalini hapo,” alisema Kamanda Fuime.

Baada ya kutafutwa, mmiliki wa nyumba hiyo Blandina Clarence Akilizao (49), alisema nyumba yake ilikuwa na wapangaji sita wenye familia, huku familia yake ikiwa na watu saba.

“Ndani ya nyumba nilikuwa na watoto wawili, wadogo zangu wawili na wajukuu wawili, pia kulikuwa na familia tano zilizokuwa na watu 17 jumla,” alisema mama huyo kwa uchungu.

Blandina alisema nyumba hiyo aliachiwa na mumewe aliyefariki dunia mwaka 2000 na kwamba hivi sasa hana msaada wowote, kwani akiba ya fedha aliyokuwa nayo kiasi cha Sh200,000 imefukiwa na kifusi na hajui namna ya kuipata.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni mpangaji, Msafiri Nyamolelo alisema ajali hiyo ilitokea ghafla na kabla ya ukuta kuanguka, ulisikika mlipuko na baadaye kelele za maji, kisha kishindo kikubwa juu ya paa.

“Karo lilipasuka na kwa kuwa ardhi hiyo hapo juu kwa muda mrefu ni dampo lenye mifuko mingi, ardhi ilikuwa imeoza, hivyo miti mikubwa ambayo iliota huko iling’oka baada ya karo kupasuka na kutua juu ya paa la nyumba sambamba na udongo kutoka juu nao ukafunika,”alisimulia Nyamolelo.

Akizungumzia tukio hilo, Katibu Mtendaji wa Mtaa wa Ukwamani, Kata ya Kawe Kassim Mbezi alisema chanzo cha ajali ni kupasuka kwa karo la choo na maji yaliyomwagika ambayo yaliuzoa mti huo na kifusi kilisombwa na kuifunika nyumba hiyo.

“Tulipofika eneo la tukio tuliwakimbiza majeruhi wote Mwananyamala, lakini kwa bahati mbaya walifariki baada ya kufika mapokezi wote walitoka wakiwa bado wanahema, lakini ilipofika saa tatu asubuhi tukaambiwa kwamba kulikuwa na ‘house girl’ hivyo baada ya kufukuafukua tukaupata mkono na baadaye kuufikia mwili mzima, huyu tulimtoa akiwa tayari amefariki,” alisema Mbezi.

Mbezi alitoa wito kwa wakazi wa bonde hilo kuhama kwa kuwa gema bado linaonekana na ni hatari na changamoto kubwa ni namna ya kukabiliana na maafa kabla ya kutokea. 

MBUNGE WA ZAMANI NA MOSHI VIJIJINI (CCM) APANDISHWA KIZIMBANI

$
0
0

Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Thomas Ngawaiya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la kujenga hoteli kwa kutumia makandarasi wasiosajiliwa.

Ngawaiya ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini na pia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Kilimanjaro, alipandishwa kizimbani jana na kusomewa shtaka hilo, siku moja baada ya kutiwa mbaroni na Polisi Kinondoni.

Kabla ya kumsomea shtaka, Mwendesha Mashtaka kutoka Bodi ya Usajili wa Makandarasi (ERB), Saddy Kambona alisema Ngawaiya amefikishwa mahakamani hapo kwa kukaidi amri ya Mahakama.

Pia, Wakili Kambona alimsomea mshtakiwa huyo shtaka linalomkabili, lakini Ngawaiya alikana na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.

Wakili Kambona alidai kuwa Machi 24, 2015 majira ya mchana, mshtakiwa alitenda kosa la kuagiza ujenzi wa jengo la hoteli, kwa watu ambao hawajasajiliwa na Bodi ya Usajili wa Makandarasi.

Alidai kuwa jengo hilo lipo Kiwanja Namba 32, makutano ya mitaa wa Dosi na Wazani, eneo la Magomeni Mapipa, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Aliendelea kudai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume cha kifungu namba 22 cha Sheria ya Bodi Usajili wa Makandarasi, Namba 17 ya Mwaka 1997.

Akitoa ufafanuzi nje ya Mahakama, Wakili Kambona alibainisha kuwa sheria hiyo inamtaka kila anayejenga jengo ambalo ni kwa matumizi ya umma lazima atumie makandarasi waliosajiliwa na ERB.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, kisha kuulizwa na Hakimu Hellen Liwa iwapo ni kweli au la, Ngawaiya alianza kujitetea.

Hakimu Liwa alimzuia na kumtaka ajibu shtaka kabla ya Wakili wake, Desidery Ndibalema kuingilia kati na kumuelekeza kwa kumnong’oneza cha kufanya, ndipo akakanusha shtaka.

Wakili Kambona baada ya kumsomea mshtakiwa shtaka hilo, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na kuomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Liwa aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili, 11.

VIONGOZI CUF WASHUTUMIWA KWA KUKOSA UZALENDO

$
0
0

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamekishiutumu Chama cha Wananchi (Cuf) pamoja na viongozi wao kwa kukosa uzalendo kutokana na kauli zao za kuunga mkono wahisani kuisitishia misaada Tanzania.

Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa kuteuliwa kutoka katika chama cha Ada-Tadea, Juma Ali Khatib ambaye aligombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa marudio, alipokuwa akichangia hotuba ya Rais wa Zanzibar kwenye baraza hilo mjini hapa.

Alisema, viongozi wa Cuf wameonesha udhaifu mkubwa wa kukosa uzalendo kwa kitendo chao cha kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo kususa misaada kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema, Zanzibar ni nchi yenye kufuata katiba yake kwa hiyo ilikuwa na mamlaka kamili kupitia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kuitisha uchaguzi wa marudio baada ya kuufuta wa Oktoba 25, mwaka jana.

“Nimesikitishwa na kauli za viongozi wa Cuf kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo kuhusu uamuzi wa kususia misaada kwa Tanzania. Viongozi hao wameonesha udhaifu na kukosa uzalendo,”alisema Khatib.

Alisema chama chake kiliamua kuingia katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20 kwa sababu umeitishwa na chombo halali kwa mujibu wa katiba, chenye majukumu ya kusimamia uchaguzi kikiwa hakiingiliwi na mtu yeyote.

Mwakilishi wa Jimbo la Mfenesini , Machano Othman Said, alisema kitendo cha viongozi wa Cuf kuunga mkono nchi washiriki wa maendeleo kususa kutoa misaada kwa Tanzania hakikubaliki hata kidogo kikionesha udhaifu mkubwa wa viongozi hao katika uzalendo wa nchi.

HAMAD RASHID: SERIKALI YA MUUNGANO ISIBABAISHWE NA WAHISANI

$
0
0

Mjumbe wa Kuteuliwa wa Baraza la Wawakilishi, Hamad Rashid (ADC) ametaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutobabaishwa na nchi washirika wa maendeleo kwa kususa misaada yao kwa kile alichosema, nafasi ipo ya kutumia rasilimali ziliopo kikamilifu.

Rashid, ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ADC katika uchaguzi wa marudio, alisema hayo wakati akichangia hotuba ya rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein aliyoitoa katika uzinduzi wa baraza la wawakilishi.

Mwakilishi huyo alionya nchi hizo akitaka zisitumie uwezo wao kwa ajili ya kulazimisha matakwa yao na kupinda sheria za nchi zinazotokana na demokrasia iliopo.

Alisema Tanzania bado inao uwezo mkubwa wa kutumia rasilimali zake zinazotokana na utajiri mkubwa kwa ajili ya kujenga nchi na kupambana na umasikini lakini viongozi walikuwa wakibweteka kutokana na kuwepo kwa misaada ya nchi matajiri.

“Tusibabaishwe na wahisani kwa tishio lao la kusitisha misaada ya maendeleo...wakati umefika wa kufanya kazi na kutumia rasilimali zetu kikamilifu ikiwemo kukusanya mapato na kupambana na viongozi wazembe na wabadhirifu."

Rashid mwanasiasa mkongwe ambaye aliwahi kuwa naibu waziri wa fedha na uchumi wa Serikali ya Muungano katika miaka ya 1987, alisema huu ni wakati wa kuiga mfano wa nchi ya Kenya wahisani walizuia misaada kwa asilimia 80 lakini walitumia walichonacho kwa ajili ya matumizi ya ndani.

Mapema Rashid alimpongeza Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohmed Shein kwa kumteua kuwa mwakilishi, hatua ambayo imetimiza ndoto zake za kuunda serikali itakayovishirikisha vyama vya siasa nchini kinyume ma matarajio ya wapinzani.

“Hii siyo serikali ya umoja wa kitaifa lakini ni serikali iliyowajumuisha wananchi na vyama vyote vya siasa na sasa tupo tayari kufanya kazi kwa ajili ya kuleta na kusimamia maendeleo kwa faida ya wananchi wote kwa sababu uchaguzi umekwisha,’’alisema.

MTOTO WA MIAKA SABA AJINYONGA KWA KAMBA

$
0
0

Mtoto George Elias (7) amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba ya katani katika Kijiji cha Buganzu, Kata ya Uyovu wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita, tukio linalodaiwa kusababishwa na michezo ya kitoto.

Baba wa mtoto huyo, Elias Martin alisema mwanawe alikuwa anasoma darasa la awali katika shule ya msingi ya kijiji hicho na siku ya tukio alikwenda kucheza na watoto wenzake.

Martin alisema akiwa nyumbani kwake akipata chakula cha mchana na wageni waliokwenda kumtembelea, walifika watoto watatu wa jirani yake wakidai mtoto wake ananing’inia juu ya mti.

Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo aliambatana na wageni wake mpaka eneo la tukio na kumkuta mtoto huyo akining’inia kwenye mti uliopo pembeni ya nyumba yake.

Mzazi huyo alisema chanzo cha tukio hilo ni michezo ya watoto na huenda alidanganywa na wenzake kuweka shingo kwenye kamba walipokuwa wakicheza.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Matayo Paschal alisema kuwa alipokea taarifa ya kifo hicho na kulijulisha Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Mpojoli Mwabulambo alisema wamefungua jalada la uchunguzi kuhusu tukio hilo, lengo likiwa kujua chanzo cha kifo hicho.

MIAKA 4 YA KIFO CHA KANUMBA, HII NDIYO HALI HALISI

$
0
0
Hii ndiyo hali halisi! Ikiwa leo ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa staa wa filamu Bongo, Steven Charles Kanumba ambapo ametimiza miaka minne kaburini, mambo mbalimbali yametokea tangu alipofariki dunia huku magari na kampuni aliyokuwa akimiliki vikiwa vimepukutika kama majani.
Kanumba alifariki dunia Aprili 7, 2012 maeneo ya Vatcan-Sinza jijini Dar nyumbani kwake alikokuwa akiishi ambapo aliyekuwa mpenzi wake kwa siri, staa wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alishikiliwa na polisi na kusweka katika Gereza la Segerea kwa mwaka mmoja, akidaiwa kuhusika na kifo chake kwani ndiye aliyekuwa naye chumbani usiku huo.
TASNIA YA FILAMU
Tangu Kanumba aondoke, tasnia ya filamu imedorora na wasanii wengi wamekuwa wakikiri kwamba ni kutokana na kifo cha staa huyo kwani ndiye aliyekuwa chachu na changamoto kubwa ambayo ilikuwa ikisababisha wengine kufanya kazi kwa bidii ili wamfikie au pengine wapite kiwango alichoku
wanacho.
TUZO ALIZO-NAZO
Kwa mujibu wa mama Kanumba, Flora Mtegoa hadi sasa marehemu anashikilia tuzo zaidi ya saba alizopewa na wadau wa sanaa hapa nchini kwa kutambua mchango wake tangu alipofariki dunia.
Kutokana na idadi hiyo ya tuzo, hadi sasa hakuna msanii yeyote wa filamu nchini ambaye ameweza kufikia rekodi hiyo.
unnamed---67Moja ya Gari alilokuwa anamiliki aina ya Toyota Lexus .
WASIKIE HAWA
“Kiukweli sanaa ya filamu imepoa sana na imekosa mwelekeo tangu alipofariki Kanumba, unajua alikuwa analeta changamoto ya kila mtu kufikiria atafanyaje ili amfunike Kanumba lakini sasa hivi watu wamebweteka, hakuna anayewaumiza kichwa tena, jambo ambalo limesababisha tasnia ya filamu kupoa na kukosa msisimko kama zamani,” anasema msanii wa filamu, Tiko Hassan.
Naye msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu, Hidaya Njaidi alisema:
“Kanumba alipofariki dunia tasnia ilikufa kabisa, sasa hivi ndiyo inaanza kufufuka kidogo baada ya serikali kuitambua na kuipa sapoti lakini vinginevyo hakuna ambaye ameonekana kuliziba pengo la Kanumba.”
Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray’ walikuwa ni washindani kwa kila kitu, iwe ni magari, blogu na hata katika filamu lakini Kanumba alipofariki dunia, hata Ray mwenyewe alipoa na manjonjo yake hayaonekani kama zamani.
MAGARI NA KAMPUNI
Miaka minne baada ya kifo cha Kanumba, magari yake matatu, Toyota Hiace, Toyota GX 110 na Toyota Lexus ambalo lilifanana na la Ray alilolinunua Sh. milioni 78. Toyota Hiace ambalo lilikuwa ni maalum kwa ajili ya kufanyia kazi za filamu ndani ya kampuni yake ya Kanumba The Great na Toyota Hiace yote hayaonekani. Yanadaiwa kuuzwa na sasa mama Kanumba anatumia usafiri wa daladala.
gari1Gali alilokuwa anatumia kwenye Movie Production.
Isitoshe pia Kanumba alikuwa na ofisi maeneo ya Sinza-Mori, Dar lakini kwa sasa haipo tena na kwa mujibu wa mama yake, vifaa vyote wamehamishia nyumbani kutokana na kushindwa kulipia kodi ya pango.
MAMA KANUMBA ANASEMAJE?
Akizungumza kwa uchungu, mama Kanumba alisema kuwa kuhusu magari, hayapo na anaomba mwanaye aachwe apumzike salama huko alipo kwani anapoulizwa maswali mengi ndipo anazidishiwa uchungu zaidi.
Kuhusu kampuni alisema vifaa vyote vipo nyumbani (Kimara-Temboni) na ikitokea kama kuna kazi ya filamu basi wahusika waliokuwa wanafanya kazi na Kanumba huwa wanakwenda kufanyia hapohapo nyumbani.
VIPI KUHUSU BLOGU YAKE?
Mama huyo alisema kwamba hafahamu chochote kuhusiana na mambo ya mtandao hivyo hajui chochote kuhusu Blogu ya Kanumba the Great.
1MDOGO WAKE KANUMBA YUKO WAPI?
Mdogo wa Kanumba anayejulikanakwa jina la Seth Bosco anasema baada ya Kanumba kufariki dunia mama yake ndiye aliyechukua nafasi ya mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mwanaye hivyo hajui chochote kinachoendelea na ikitokea kuna kazi ya filamu huwa anaenda kufanya lakini kwa sasa anajishughulisha na mambo yake binafsi ya sanaa.
Kwa upande wa blogu ya Kanumba www.kanumbathegreat.blogspot.com ambayo picha ya mwisho kuwekwa ilikuwa Aprili 6, 2012 anasema kwamba walishindwa kuiendeleza kutokana na kuwa hawana namba ya siri ‘password’ yake kwani alikuwa nayo mwenyewe Kanumba na hakuna anayeifahamu hadi sasa.
MIRATHI VIPI?
Mama Kanumba anasema suala la mirathi halipo tena na bado yupo anasikilizia kama anavyosikilizia kesi ya Lulu kuanza kutajwa mahakamani ila kama Baba Kanumba, Charles Kanumba ataibuka na kuzungumzia tena mali za mwanaye, ataenda kufungua mirathi.
NINI HATMA YA LULU?
Baada ya kukaa gerezani kwa mwaka mmoja, Lulu aliachiwa huru kwa dhamana baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza kesi hiyo na kukutwa na kesi ya kuua bila kukusudia, mpaka sasa haijaanza kusikilizwa.
Katika kumbukumbu ya kifo cha Kanumba leo, ibada ya kumuombea itafanyika Kanisa la KKKT, Temboni jijini Dar na baada ya hapo mama yake pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wataelekea Makaburi ya Kinondoni kulifanyia usafi kaburi lake.
Mama Kanumba anasema kwa mwaka huu utaratibu utakuwa ni huo tu lakini kwa mwaka kesho atakapotimiza miaka mitano atamfanyia kitu maalum, hakukiweka wazi.

PADRI AMTOLEA TAMKO JOKATE

$
0
0
IMG-20151118-WA0010-721x1024IMG-20151118-WA0010-721x1024Mbongo Fleva na Miss Tanzania No. 2, 2006, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
DAR ES SALAAM: Baadhi ya watu waliodai kuwa wao ni waumini wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam ambako anaabudu Mbongo Fleva na Miss Tanzania No. 2, 2006, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wamesema nyota huyo hatakiwi kushiriki ibada kwa vile uhusiano wake na Mbongo Fleva, Ali Kiba upo wazi sana, sasa kanisa hilo limetoa tamko, tambaa na Amani.
Akizungumza na gazeti hili juzi kanisani hapo, padri aliyejitambulisha kwa jina moja la Edward ‘Faza Edward’ alisema wao kama kanisa wanamtambua Jokate kama muumini wao wa miaka mingi na kwamba mambo mengine hayawahusu.
“Jokate namtambua kama muumini wetu hapa ana anashiriki vizuri tu. Sisi hatuna tatizo naye. Kwanza sisi  mtu yeyote anaruhusiwa kuja kusali hapa, hata kama ni Mwislam ilimradi tu afuate taratibu zetu.
“Kwa hiyo Jokate tunaye hapa kanisani na anaendelea vizuri tu. Umemuulizia na paroko, yeye muda huu ana wageni,” alisema Faza Edward.
Ali-mkiba-jokate-na-wema-2….Akiwa na Ally Kiba.
Awali waumini hao walisema kuwa, kitendo cha Jokate kuonekana kwenye vyombo mbalimbali vya habari akiwa na Kiba huku si mwanandoa wake jambo ambalo wao wanaliona si sawasawa kwa vile mrembo huyo hushiriki pia kuimba kwaya ya kanisa hilo.
Mwaka jana, gazeti dada na hili, Ijumaa liliandika habari yenye kichwa kisemacho; Waumini: Jokate anatutia aibu.
Katika habari hiyo, Jokate alidaiwa kuwakera waumini wenzake kufuatia kupiga picha za nusu utupu na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii huku midume ikijirushia na kujifaidia kwa macho.
Pia, alilalamikiwa kwa tabia yake ya kupanda jukwani kwenye kumbi za muziki na kunengua huku yeye akiwa ni mwanakwaya wa kanisa hiyo.
Akijitetea kuhusu madai ya waumini wenzake katika habari hiyo, Jokate alisema kuwa, kanisa hilo halimzuii kuvaa nguo fupi wala kukata mauno jukwaani kama mwanamuziki kwani kazi ni kazi.
Alisema kanisani anakwenda kama kawaida na kwaya anaimba kama ‘kawa’.
Katika habari hii mpya, Jokaye alipoulizwa alisema: “Mimi sitaki mnifuatilie mambo yangu ya imani, sitaki kabisa, mnanikwaza.”
Waandishi Hamida Hassan na Imelda Mtema.

POLISI DAR WAMCHUNGUZA ZARI!

$
0
0
ZARI47817ZARI47817Zarina Hassan ‘Zari’ au mama Tiffah.
DAR ES SALAAM: Kufuatia kamatakamata ya wafanya-biashara wanaodaiwa kujihusisha na madawa ya kulevya ‘unga’ Bongo, kuna madai kwamba, Jeshi la Polisi Tanzania linawachunguza upya mastaa wanaoingia na kutoka kwa kutumia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar huku Zarina Hassan ‘Zari’ au mama Tiffah akitajwa kuwemo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, hatua hiyo imekuja baada ya jeshi hilo kubaini ‘ingia toka’ ya mastaa hao ambao baadhi yao wamemaliza vitabu vitatu vya hati za kusafiria kwa mwaka mmoja kwa kupigwa muhuri wa uhamiaji kwa sababu ya safari.
CHANZO NI HIKI
“Mimi nawapa habari, jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania linamchunguza Zari na mastaa wengine wanne, leo siwataji. Kisa ni safari zao za kuingia Tanzania mara kwa mara.
“Polisi wanajua kwamba Zari anakuja Bongo kwa sababu ya kumfuata Diamond (Nasibu Abdul) ambaye ni mzazi mwenzake. Ndiyo maana leo yupo Afrika Kusini, kesho Dar es Salaam.
“Lakini jeshi la polisi haliwezi kulegezea hilo eti kisa anamfuata Diamond. Linachotaka kujua ni je, kweli anamfuata Diamond au anasafirisha unga? Si kwamba wanajua anajihusisha na unga bali wanamchunguza,” kilisema chanzo hicho kutoka jeshi la polisi.
Diamond-PlatnumzDiamond Platinumz.
POLISI NA WASHIRIKA Chanzo kikadai kuwa polisi hao wanashirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania na uongozi wa uwanja huo ili kufanikisha uchunguzi wao kwa watu wanaopita mara kwa mara.
MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE
Baada ya taarifa hizo, gazeti hili juzi lilipiga simu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kwa lengo la kutaka kuongea na bosi wao anayekaimu, Mhandisi George Sambali  lakini katibu muhtasi (sekretari) wake aliyepokea simu alitaka kujua shida ya gazeti kabla ya kuunganishwa na bosi wake huyo.
Sekretari:  “Mamlaka ya Viwanja vya Ndege hapa, nikusaidie nini?”
Amani: “(baada ya kujitambulisha) nataka kuongea na mkurugenzi.”
Sekretari: “Kwa shida gani ndugu?”
Baada ya kuambiwa shida mwanzo hadi mwisho…
Sekretari: “Hiyo siyo hapa, piga simu namba…(anazitaja namba) za uwanja wa ndege kule.”
AMANI NA UWANJA WA NDEGE
Amani lilipiga simu JNIA na kupokelewa na sekretari aliyejitambulisha kwa jina la Joyce Batenga.
Sekretari: “Uwanja wa Ndege Dar es Salaam hapa, naitwa Joyce Batenga, nani mwenzangu?”
Baada ya Amani kujitambulisha na kuanika shida yake, dada huyo alisema:
“Ngoja nikuunganishe na Security Officer (Ofisa Usalama wa Uwanja).”
Baada ya muda, Amani lilipokelewa na ofisa usalama huyo ambaye alikataa katakata kutaja jina lake. Alipoelezwa shida ya gazeti hili, alisema:
“Sisi hapa uwanjani tunamchunguza kila mtu anayepita kutoka na anayepita kuingia. Hatuachi mtu hata mmoja.”
Amani: “Sasa hilo za Zari unasemaje, kuna ukweli wowote?”
Ofisa: “Si kila kitu cha kusema ili kiandikwe gazetini kaka. Kama unaweza njoo tuongee ana kwa ana. Tafuta muda ukifika jitambulishe tutaongea kila kitu lakini si kwenye simu.”
AMANI NA MKUU WA POLISI KITUO CHA UWANJA WA NDEGE
Baada ya hapo, gazeti lilimtafuta kwa simu, Mkuu wa Kituo cha Polisi Uwanja wa Ndege, Leocadia Marcian baada ya kusikiliza madai mpaka mwisho, alisema:
“Sawa, nimekusikia lakini mimi sasa nipo likizo na nipo safarini.”
Amani: “Nani anakukaimu?”
Mkuu wa Kituo: “Siwezi kujua, mimi niko njiani nasafiri, nipo likizo halafu si msemaji.”
AMANI NA KAMANDA WA MADAWA YA KULEVYA
Baada ya kuzungumza na wote hao, gazeti hili lilikwenda mbele zaidi kwa kuongea na Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kuzuia Madawa ya Kulevya, ACP Mihayo Msikhela ambaye alipoambiwa ishu yote alisema kwa ufupi:
“Tunamfuatilia. Karibuni sana ofisini kwangu.”
Amani: “Tumetoka hapo ofisini kwako muda si mrefu, tukaambiwa upo makao makuu.”
Kamanda Mihayo: “Basi karibuni tena.”
SASA NI DIAMOND
Diamond alitafutwa kwenye simu kwa kutumia mtandao wa WhatsApp ambapo alipopatikana alisema:
“Mimi tangu nimekuwa na Zari sijawahi kumwona akiwa na mambo hayo. Watu wanasema tu. Kule Uganda waliwahi kusema lakini hakuna kitu. Ndiyo maana unamwona anadunda. Mbona yuko poa sana.”
ALIWAHI KUTAITIWA KABISA
Mbali na madai ya Zari kuchunguzwa, Juni mwaka jana, Diamond aliwahi kutaitiwa na askari wa uwanja huo kwa muda wa saa mbili akiwa na mabegi matatu.
Diamond alikumbwa na nusanusa hiyo baada ya kutua uwanjani hapo akitokea Afrika Kusini ‘Sauzi’ alikokwenda kwa shoo ambapo askari walitaka kujiridhisha kama hajabeba unga.

DAYNA NYANGE AWACHANA MASHABIKI

$
0
0
Dayna
Dayna
Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’

Staa wa Ngoma ya Angejua, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’ amewatolea uvivu watu wanaofuatilia maisha yake katika mitandao ya kijamii kuwa hakuna anayemsaidia kuyaendesha.
Akichonga na Showbiz, Dayna aliyewahi pia kubamba na ngoma kadhaa kama vile Mafungu ya Nyanya alisema kuwa, suala la kuwa na skendo kwa msanii ni jambo la kawaida hivyo anawashangaa wanaoendelea kumuandama kila kukicha kutokana na skendo anazokumbana nazo.
“Huwa inanikera sana kuona watu wananiandama bila mpango wakati hakuna anayenisaidia kuendesha maisha yangu, niachwe huru maana hata hizo skendo wao haziwahusu,” alisema Dyna.

VENGU ASAKWA KWA SAA 72

$
0
0
Vengu3Mchekeshaji maarufu Bongo, Joseph Shamba ‘Vengu’.
DAR ES SALAAM: Baada ya wasomaji mbalimbali kuonesha hamu ya kutaka kujua hali ya mchekeshaji maarufu Bongo, Joseph Shamba ‘Vengu’, Amani lililazimika kuingia ‘front’ kumsaka msanii huyo kwa takriban saa 72 na kuibuka na majibu yanayokinzana.
MSOMAJI AANZA KUMUULIZIA
Awali, mmoja wa wasomaji wetu aliyejitambulisha kwa jina la Anna Michael, alipiga simu katika chumba cha habari na kueleza kiu aliyonayo kutaka kujua hali ya msanii huyo aliyekuwa akitikingisha alipokuwa na wenzake wa Kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Mujuni Silvery ‘Mpoki’, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvanga’ na Alex Chalamila ‘Mac-Reagan’.
“Jamani Global (Global Publishers Ltd; wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi) mbona hamtuletei habari za mchekeshaji Vengu? Yupo wapi siku hizi? Bado anaumwa au ameshapona? Tunatamani kumuona akiwa kwenye runinga.
“Tunamisi vile vituko vyake. Tangu mlipokuwa mnaripoti habari zake za ugonjwa ni miaka kama mitano sasa imepita, hebu fuatilieni mtujuze maana ninyi ndiyo tunawategemea kama chombo cha habari,” alisema.
IMG_1908Mapaparazi wakiwa katika doria jirani na kwa Vengu.
WASOMAJI WENGINE
Kama hiyo haitoshi, kwa nyakati tofauti, wasomaji mbalimbali wamekuwa wakiwauliza wahariri wa magazeti ya Global ambapo wengi wao wamekuwa wakitaka kumjulia hali.
AMANI MZIGONI
Kama ilivyo desturi ya Global kuhakikisha inakata kiu ya wasomaji wake kwa habari za uhakika, liliingia mzigoni ambapo lilifanikiwa kuzungumza na mtu wa karibu na familia (hakutaka jina lake lichorwe gazetini) ambaye alisema amesikia Vengu hajambo na yupo kwenye nyumba yake, Kigamboni-Kibada, Dar.
“Nasikia anaendelea vizuri. Anapiga misele ya hapa na pale. Yupo Kibada kwenye zile nyumba walizokopeshwa na NSSF,” alisema mtu huyo wa karibu na familia.
AMANI LATUA KIBADA
Machi 30, mwaka huu, mapaparazi wa gazeti hili walifunga safari hadi Kibada ambapo walilazimika ‘kupatroo’ kutwa nzima maeneo yanayoizunguka nyumba ya Vengu ili kujiridhisha.
Hata hivyo, jitihada za kumnasa Vengu akipiga misele hazikuzaa matunda kwani licha mapaparazi kutega kamera, hawakufanikiwa kumnasa.
IMG_1931…..Wakiongea na mama wa Vengu.
MAPAPARAZI WABISHA HODI
Mapaparazi walilazimika kubisha hodi katika mlango wa mbele wa nyumba hiyo ambapo waliitikiwa na mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni mama yake mdogo Vengu. Alikuwa amekaa kwenye varanda la uani.
Amani: “Mama habari za hapa na mnaendeleaje na hali?”
Mama: “Nzuri tu, za kwenu?”
Amani: “Hatujambo mama, sisi ni waandishi wa habari tumetokea…(mama anakatisha mazungumzo ya mapaparazi).”
Mama: “Aliyewaelekeza hapa ni nani?”
Amani: “Kuna mtu wa bodaboda tumekutana naye (kujaribu kumuondoa wasiwasi) ndiyo tukamuuliza. Tunaona umefanana na Vengu, bila shaka wewe  ni mama Vengu mwenyewe, si ndiyo?”
Mama: “Mimi siyo mama yake mzazi. Mimi ni mama yake mdogo.”
Amani: “Labda utuambie Vengu anaendeleaje?”
Mama: “Hajambo.”
Mapaparazi: “Sijui yupo ndani na tunaweza kumuona au…(mama akatisha mazungumzo).”
Mama: “Hayupo hapa, yupo kwa kaka yake Kunduchi. Halafu ninyi nawajua vizuri, hapa mnanirekodi. Najua sauti yangu mnayo mnataka mkaitumie. Kama mnataka kumuona nendeni Kunduchi kwa kaka’ke?”
IMG_1944….Wakiondoka nyumbani kwa Vengu.
Amani: “Mashabiki wake wametuuliza, wanataka kujua anaendeleaje ndiyo maana tumekuja kuuliza na pengine wanaweza kumpa msaada kama anahitaji.”
Mama: “Hamna lolote. Mlikuwa mnaandika ili muuze magazeti. Wenye lengo la kumsaidia wanaendelea kimyakimya sasa ninyi mnaojifanya kutangaza, hamna lolote.”
Amani: “Basi mama hamna tabu, tunashukuru ngoja twende huko Kunduchi. Si ni kwa yule kaka yake ambaye ni refa (Andrew Shamba) wa mpira wa miguu?
Mama: “Ee huyohuyo.”
KAKA MWINGINE APATIKANA
Wakati mapaparazi wakiendelea kuchimba, waliipata namba ya simu ya kaka mwingine wa Vengu anayefahamika kwa jina la Donat Shamba ambaye alipoulizwa kuhusu hali ya Vengu, hakutoa ushirikiano wa kutosha zaidi ya kusema kama kuna kitu Amani limekipata kuhusu afya ya Vengu liandike.
“Kwanza nani amewapa namba yangu? Sikia nyinyi mmekuwa mkiandika habari nyingi za uongo huko nyuma sisi tulikaa kimya. Sasa naona mnaleta mpya hapa, muulizeni Imelda (mwandishi wa Global ambaye aliwahi kumfokea)… sasa ninyi kama mna ushahidi na mnachotaka kuandika andikeni, mimi sitaki kuzungumzia chochote.”
AMANI LATUA KUNDUCHI
Kwa kuwa siku hiyo muda ulikuwa si rafiki, Machi 31, mapaparazi wetu walifika Kunduchi na kumuulizia refa huyo wakiamini kuwa ni maarufu hivyo ni rahisi kumfikia lakini bahati mbaya kila aliyeulizwa na Amani, alisema hamfahamu.
Kama hiyo haitoshi, Amani lilishinda siku nzima maeneo ya Kunduchi bila mafanikio ambapo jioni mapaparazi walipata wazo la kutafuta namba ya simu ya refa. Akapigiwa simu na alipopokea, alisema yeye haishi Kunduchi na hajawahi kuishi huko hata siku moja.
“Mimi siishi Kunduchi bwana. Naishi Kigogo Freshi, Pugu Kajiungeni. Yaani ukifika tu Pugu Kajiungeni pale mwisho, ukiuliza Kigogo Freshi ukifika tu hapo, ukiuliza hata mtoto mdogo kwa refa ni wapi atakuelekeza. Sema tu leo niko safarini nakwenda Mbeya kuchezesha mechi ya Mbeya City na Coastal Union,” alisema kaka huyo hivyo kulifanya Amani libaini kuwa, Vengu ana kaka wawili tofauti waliotajwa na mama mdogo.
NDANI YA KIGOGO FRESHI SASA!
Kutokana na muda kuwa si rafiki, Aprili  Mosi, mapaparazi wetu walifika Pugu Kajiungeni na kuelekezwa eneo maarufu la Kigogo Freshi ambapo kabla ya kufika kwenye nyumba ya refa, Amani lilizungumza na mmoja wa majirani ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, akasema Vengu haishi hapo.
MAJIBU TOFAUTI
“Mh! Vengu kama kuishi hapa labda awe amehamia jana usiku lakini siku zote hapa kwa refa najua anaishi yeye, mdogo wa mke wake na mke wake. Tena mkewe leo hayupo. Ameenda kazini. Nafikiri atakuwepo mdogo wake tu ndani, jaribuni kugonga, refa atakuwa kawapoteza maboya bwana, Vengu angekuwepo hapa sisi majirani zake tungejua,” alisema jirani huyo.
NDANI KIMYA
Hata hivyo, Amani lilibisha hodi nyumbani hapo lakini hakukuwa na majibu. Hadi siku hiyo ambayo Amani lilitimiza siku tatu (saa 72) tangu mapaparazi wake wamfungie kazi Vengu, lilibaini kuwa ndugu wa Vengu hususan ‘mama mdogo’ na refa hawakuwa wawazi!
TUJIKUMBUSHE
Vengu aliugua mwaka 2009. Agosti 2011 alizidiwa  ambapo alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar. Rais wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete alikwenda kumjulia hali akiwa hospitalini hapo.
Baada ya hali yake kutotengemaa, alipelekwa kwenye Hospitali ya Apollo nchini India ambako alipatiwa matibabu na kurejeshwa nchini akiendelea kuuguzwa na familia.

TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

$
0
0

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA

YAH: TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari “NDALICHAKO NA WALIMU TZ”.

Taarifa hiyo inadai kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazo vaa wakati wa kazi.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza.

Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.

IMETOLEWA NA

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
07/04/2016

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 22 YA MAUAJI WA KIMBARI NCHINI RWANDA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishuhudia  wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame pamoja na binti yao wakiweka shada la maua katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame wakiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjini Kigali, Rwanda, leo katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 22 ya mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994 ambapo watu takribani milioni 1,000,000 waliuawa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiweka shada la maua wakishuhudiwa na  wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame wakiweka shada la maua katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Rais Paul Kagame kwa pamoja wakiwasha "Urumuri Rutazima"  (Mwenge/mwali wa Matumaini)  katika maadhimisho Kumbukumbu ya miaka  22 ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo

Wabunge Wanawake wa UKAWA watoka nje ya Bunge baada ya Mbunge wa CCM Kuwatuhumu Kwamba Wamepata Ubunge Kwa Kufanya Mapenzi na Viongozi Wao

$
0
0
Wabunge wanawake wa Upinzani wametoka wote nje ya Bunge kwa madai ya kudhalilishwa bungeni na Mbunge wa jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga (CCM ) aliyedai jana kuwa viti maalum Ukawa hutolewa kwa rushwa ya ngono.

Mlinga alitoa kauli hiyo jana wakati akichangia hotuba Wizara ya Katiba na Sheria  ambapo alisema ili uweze kuwa mbunge wa viti maalum chadema, lazima ufanye mapenzi na kiongozi wako wa chama.
 
Wabunge hao leo asubuhi  waliomba mwongozo kwa Naibu Spika 
kupitia kwa Mbunge Sophia Mwakagenda wa viti maalumu (Chadema) kumtaka mbunge huyo athibtishe kauli yake  lakini hawakusikilizwa na badala yake Naibu spika aliwataka wakae chini.

Baada yamabishano ya dakika kadhaa pasi kusikilizwa, wabunge hao  walisimama wote na kuamua kutoka nje  ya ukumbi wa bunge huku wakiahidi kuja na tamko kali kuhusu udhalilishaji waliofanyiwa.
 
==>Msikilize hapa Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CHADEMA, Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya wabunge hao kutoka nje.
 

Mahakama Kuu Yaitupilia Mbali Rufaa iliyoletwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali(DPP) dhidi ya Kesi ya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA na Wenzake

$
0
0

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliyokuwa ikipinga kuondolewa kwa shitaka la 8 la utakatishaji fedha linalomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya na wenzake wawili.

Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Moses Mzuna alipokuwa akitoa majibu ya rufaa iliyokuwa imekatwa na DPP.

“Ninafahamu kila kesi inaamuliwa kutokana na mazingira yake lakini nimefuta rufaa hii kwa kuwa hoja zilizotolewa hazina nguvu kisheria” alisema Jaji Mzuna.

Aidha Jaji Mzuna amefafanua kuwa hata kama amefuta rufaa hiyo lakini upande wa Jamuhuri bado una nafasi ya kubadilisha shitaka au hati nzima ya mashtaka inayowakabili washtakiwa hao.

Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali Timony Vitalis amekubaliana na uamuzi uliotolewa na Mahakama hiyo juu ya pingamizi lake ingawa bado anasimamia watuhumiwa kutofutiwa shitaka la utakatishaji wa fedha.

Naye Wakili wa Utetezi Majula Magafu amesema kuwa wao wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na Wakili wa Serikali ili wajue namna ya kuikabili kesi hiyo.

Tamko la wizara ya Afya Kulaani Mauaji ya Mama na Mtoto Huko Bagamoyo

$
0
0
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inasikitishwa na inalaani vikali tukio la kuuawa kwa kuchinjwa, mwanamke Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emmanuel (3), wakazi wa eneo la Zinga, kata ya Dunda, wilayani Bagamoyo, kutokana na wivu wa kimapenzi.

Wizara inakemea maauji hayo, yanayodaiwa kutekelezwa na Frowin Mbwale  mkazi wa Kawe, Dar es salaam, ambaye ni mme wa marehemu, kwani yamesababisha kukatisha maisha ya mama na mtoto, katika kipindi ambacho Taifa linahimiza uzingatiaji wa mchango na haki za wanawake katika maendeleo ya taifa, na mwitikio wa haki ya kuishi ya Mtoto katika mipango na programu za maendeleo endelevu.

Wizara inasisitiza kutambua kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa wanafamilia liko mikononi mwa kila mwananchi, hivyo jamii inawajibu wa kusaidia udhibiti wa ukatili na mauaji katika familia na jamii zetu.

Jamii ikiwa na uelewa wa pamoja katika haki za wanawake na watoto katika jamii, itawezesha kuwekeza katika haki ya kuishi ya Mtoto, na  kuendelea kuwaamini wanawake kwamba wanaweza kutoa mchango mkubwa wa kuendeleza familia zao, na taifa likaweza kupiga hatua kufikia maendeleo endelevu. 

Wizara inapenda kupongeza Polisi mkoa wa Pwani na wananchi walitoa taarifa za kuwakamata watuhumiwa wa mauaji haya, na tunaamini kuwa watakapofikishwa mbele ya vyombo vya sheria haki itaweza kutendeka.

Wizara inapenda kutoa pole kwa familia za marehemu hao waliopoteza maisha kwa kuchinjwa na kuawa, na kuwaombea kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi makubwa. Wizara inaitaka jamii itambue kuwa hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa mtu mwingine, na mwanamke na mtoto anahaki ya kuthaminiwa utu wake, bila ubaguzi wowote ambao unaweza kukatisha maisha yao.

      Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
     Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee

Jengo La NSSF La Eneo La Akiba Lawaka Moto

$
0
0
Jengo lililoko eneo la akiba posta jijini Dar es salaam limeripotiwa kuwaka moto kuanzia majira ya jioni na chanzo cha moto huo kinasemekana ni mtungi wa gesi kulipuka na kusababisha moto.

Inasemekana hakuna madhara makubwa kutokana na zimamoto kufika kwa wakati katika eneo la tukio.  

Here Are All Tanzania Newspapers Today 07 May 2016

Jason Rweikiza Achaguliwa Kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM

$
0
0

WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamemchagua Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza kuwa Katibu wao.

Rweikiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, ambaye safari hii hakuwania nafasi hiyo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Msekwa uliopo ndani ya viwanja vya Bunge, Katibu huyo mpya wa Wabunge wa CCM alikuwa akipambana na Mary Chatanda, Mariam Kisangi na Abdalah Ulega.

Wabunge wote wa CCM pia walipiga kura kuwachagua wabunge 10 kati ya 21 walioomba ujumbe wa NEC.

Waliochaguliwa ni Livingstone Lusinde, Dk Hamis Kigwangalla, Stanslaus Nyongo, Steven Ngonyani, Peter Serukamba, Faida Bakari, Agness Marwa, Munde Tambwe, Angella Kairuki na Jamal Kassim Ali.

Wabunge ambao kura hazikutosha ni Mbaraka Dau, Alex Gashaza, Hawa Ghasia, Ibrahim Raza, Profesa Norman Sigalla ‘King’, Almas Maige, Angelina Malembeka, Yahya Massare, Mattar Ali Salum na Hafidh Ali Tahir.

Mbunge Ataka Walawiti na Wabakaji Wahasiwe

$
0
0
MBUNGE wa Viti Maalumu, Angelina Malembeka (CCM) ametaka watu wanaohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la ubakaji na ulawiti, wahasiwe ili wawapo gerezani wasiendeleze tabia hizo.

“Tumeshaona wanaohukumiwa kifungo cha maisha, wakiwa huko gerezani wanaendeleza vitendo vya kulawitiana, kwa nini sasa wasihasiwe?” Alihoji. 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe, wakati akimjibu jana alisema, “siwezi kuwa na jibu kwa sababu Bunge ndilo linalotunga sheria, mbunge aje na wazo lake hapa bungeni lipitishwe kama sheria sisi Serikali hatuwezi.”

Akitoa ufafanuzi zaidi juu ya hali ya ubakaji na ulawiti, Dk Mwakyembe alisema kila siku nchini kunaripotiwa matukio 19 ya kubakwa na kulawitiwa.

Alisema hali ni mbaya sana na sasa kuna mashauri 2,031 yaliyoripotiwa mahakamani katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu. 
Kati yake mashauri hayo, 111 yameshakamilishwa kwa kuhukumiwa ambapo watu 99 wamefungwa, watuhumiwa 18 wameachiwa huru kwa kukosa ushahidi na kesi 1,920 hazijakamilika.

Akijibu swali la msingi la mbunge huyo aliyehoji mpango wa Serikali kuhakikisha kesi za kubakwa na kulawitiwa hazimalizwi kifamilia, Dk Mwakyembe alisema kumalizwa kwa kesi kifamilia kunachochea vitendo hivyo kuendelea katika jamii.

“Tatizo la kuficha ushahidi na kumaliza kesi hizo kifamilia, haliwezi kumalizwa na vyombo vya dola peke yake bila ushirikiano na wananchi wanaoishi na watuhumiwa. Hivyo Serikali imekuwa ikitoa elimu kwa umma kuwa kuficha ushahidi na kuyamaliza matukio hayo ya jinai kifamilia si kosa peke yake, bali vilevile utaratibu huo unachochea vitendo hivyo kuendelea katika jamii,” alifafanua.

Ili kuweka mazingira rafiki kwa waathirika na wananchi wenye taarifa au ushahidi wa aina hiyo, alisema Serikali imeanzisha madawati ya jinsia katika vituo mbalimbali vya Polisi yanayopokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi na kuliwezesha Jeshi la Polisi kuendesha upelelezi kwa ufanisi.

“Pindi tukio la kubaka au kulawiti litakaporipotiwa, upelelezi hufanyika na mtuhumiwa kufunguliwa mashitaka mara moja, kwa utaratibu huu Serikali inahakikisha kuwa matukio haya hayamalizwi nje ya utaratibu wa haki jinai,” alisema.

Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 imeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu yeyote anayekutwa na hatia ya kumbaka msichana. Pia sheria imeweka adhabu ya kifungo cha miaka 14 kwa kosa la kulawiti.
Viewing all 2674 articles
Browse latest View live