Quantcast
Channel: DUNIA KIGANJANI BLOG | Ifanye Dunia Kuwa Yako
Viewing all 2674 articles
Browse latest View live

WATU 580 WAJITOKEZA KUHAKIKI SILAHA DAR ES SALAAM

$
0
0

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imesema watu 574 wamejitokeza kuhakiki wa silaha zao.

Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda alitoa siku 90 kwa wakazi wa Dar es Salaam wawe wamehakiki silaha zao ifikapo Julai mosi, ikiwa ni miongoni mwa mikakati yake ya kupambana na uhalifu uliokithiri.

Hivi karibuni, Rais John Magufuli alihakiki silaha zake anazomiliki.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema wanaendelea kuwahimiza wananchi waendelee kujitokeza kuhakiki silaha zao kwa muda uliotolewa.

“Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliokaidi kujitokeza kuhakiki silaha zao, baada ya siku 90 zilizopangwa kumalizika”alisema.

Wakati huohuo, Siro alisema wafanyabishara wanaouza vipuri vya magari vilivyotumika maeneo ya Kariakoo, wengi wanauza vilivyoibwa sehemu mbalimbali nchini.

 “Nimeshapata mtandao mzima wasipoacha kununua vitu vya wizi tutawakamata na wale wanaojifanya madalali wao, wanashirikiana na majambazi hivyo nataka waache mara moja,” alisema.

MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM, ISAYA MWITA AAPISHWA

$
0
0

Meya Wa Jiji La Dar Es Salaam, Isaya Mwita amesema kati ya Aprili 10 na 11 ataitisha kikao cha kwanza cha Baraza la Jiji, kwa ajili ya kumpata naibu meya.

Mwita aliyasema hayo jana  muda mfupi baada ya kuapishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Sokoine.

Machi 22, Mwita alichaguliwa kuwa meya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kupata kura 84 dhidi mpinzani wake, Yusuf Yenga (CCM) aliyeambulia 67.

Mwita alisema kinachoendelea hivi sasa ni taratibu za kuwapata wajumbe watakaoingia katika baraza hilo, ambalo lipo tofauti na lililomchagua yeye.

“Ningeweza kuitisha baraza hili hata Ijumaa, lakini sheria inanitaka nikishateuliwa, niitishe baada ya siku saba,” alisema Mwita ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema).

Machi 23, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe alisema kuwa naibu meya atapatikana katika Baraza la Jiji litakaloongozwa na meya akishirikiana na yeye.

Hata hivyo, Kabwe alisema jana kuwa wanaendelea na maandalizi ya baraza hilo, ikiwamo kusubiri kuwasilishwa kwa akidi ya wajumbe watakaoshiriki kikao hicho.



Baada ya kuapishwa, Mwita aliwaambia wanahabari kuwa anadhamiria kuwa kiongozi muunganishi bila kujali tofauti za kiitikadi.

Alisema hatarajii kipindi chake cha uongozi kiwe na vurugu au machafuko katika Jiji la Dar es Salaam.

‘’Viongozi wangu wa chini wajisikie amani, kwani mimi nitakuwa kiongozi bora kwa watu wote. Wala sikuja kwa ajili ya kuleta machafuko na ugomvi, bali nahitaji amani ili tutafute maendeleo,’’amesema.

Mwita alisisitiza ushirikiano kwa viongozi wote ili washughulikie changamoto za muda mrefu katika jiji hilo – usafiri, miundombinu, afya, elimu, na huduma nyingine za jamii.

WANANCHI WAANZA KUGOMBANIA KITI ALICHOKIKALIA RAIS MAGUFULI KWENYE MGAHAWA JIJINI MWANZA

$
0
0

Mgahawa aliotumia Rais John Magufuli kupata mlo wa mchana na msafara wake juzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza, umekuwa kivutio kwa wateja wengi wakinunua chakula na kutaka kukalia kiti na meza alivyotumia kiongozi huyo.

Meneja wa mghahawa huo wa Victoria, Elizabeth Maneno (pichani) alisema jana kwamba hali hiyo ilijitokeza mara baada ya Rais kuondoka hapo.

“Hata leo tumepokea wateja wengi kulinganisha na siku nyingine,baadhi yao wanaagiza chakula kwa sharti la kutaka kukikalia kitina meza aliyotumia Rais Magufuli,” alisema Elizabeth.

Akizungumzia hali ilivyokuwa juzi kabla na wakati wa ugeni huo meneja huyo alisema: “Ilikuwa ni hofu na woga uliochanganyika na furaha kumwona Rais akiingia kwenye mgahawa wetu wa chai ya rangi ya Sh200 na ya maziwa Sh300.

“Mshtuko wetu uligeuka furaha baada ya kubaini kuwa oda ya sahani 28 za kubeba (takeaway), tulizoagizwa mapema asubuhi bila kuelezwa zinakoenda zilikuwa za ujumbe wa Rais,” alisema na kuongeza:

“Kabla Rais Magufuli hajaingia kwenye mgahawa wetu, alikuja mtu mmoja tusiyemfahamu na kuagiza sahani 28 za chakula kwa gharama ya Sh5,000 kila moja,”

Alisema baada ya kumtaarifu mteja wake kuwa chakula kiko tayari, alielekezwa kuandaa meza na viti kwa sababu wageni wake (wa mteja), sasa wameamua kula palepale mgahawani.

“Ghafla tulimwona Rais anaingia ndani ya mghahawa wetu; kwanza tulishikwa hofu, woga na kihoro tusijue tufanye nini hadi tulipogutushwa na aliyetoa oda kwa kutuagiza tugawe chakula alichoagiza,” alisema meneja huyo; “hapo ndipo tulipobaini kumbe chakula kile kilikuwa cha ugeni wa Rais.”

Pamoja na chai ya rangi na ya maziwa, mghahawa huo pia unauza vyakula vya aina mbalimbali kwa bei kati ya Sh1,500 hadi Sh5,000 kwa vyakula vya kubeba, huku soda ikiuzwa kwa Sh500 kwa chupa.

BREAKING NEWZZ!!! WAKUU WA MIKOA WAWASILISHA RIPOTI ZA WATUMISHI HEWA ........MWANZA YAONGOZA KUWA NA WATUMISHI HEWA WENGI IKIFUATIWA NA ARUSHA

$
0
0

Hatimaye  wakuu wa Mikoa yote nchini wametii agizo la Rais John Magufuli lilokuwa linawataka wasilishe ripoti ya idadi ya watumishi hewa kwenye mikoa husika.

Wakuu hao wa mikoa wapya wamewasilisha ripoti za watumishi hao jana Jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Georgy Simbachawene ili kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watumishi waliohusika katika kashfa hizo.

Katika ripoti hizo zilizowasilishwa, Mkoa wa  Mwanza unaongoza kuwa na watumishi hewa 334 ukifuatiwa na mkoa wa Arusha  270.

Mkoa wa Dar Es Salaam.
Akiwasilisha ripoti ya watumishi hewa,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema katika mkoa wake baada ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na kamati mbali mbali wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 73 ambao watumishi hao hewa wamepelekea serikali kupotea pesa zaidi ya Milioni 316 kwa mwaka mmoja.

“Katika mkoa huu tumepata watumioshi hewa 73, ila wengi watahoji mkoa huu mkubwa kwa nini unakuwa na watumishi hewa wachache, nataka kukwambia Waziri, bado tunaendelea na uchunguzi wa kina,”alisema Makonda .

Mkoa wa Arusha.
Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda alisema mkoa huo umegundurika kuwepo na watumishi hewa 270ambao wamekuwa wakiisababishia hasara serikali ya Bilioni 1.8 kwa kipindi cha Mwaka mmoja,

Mkoa wa Dodoma.
Pia Mkuu wa Dodoma Jordan Rugimbana alisema katika mkoa wake wamegundua kwenye mkoa huo una watumishi hewa 101 ambao amedai wameisabishia hasara serikali milioni 287.3 kwa kipindi cha miezi sita.

Mkoa wa Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema katika mkoa wake wamegundua kuwa kuna watumishi hewa 15 ambapo amemweleza Waziri Simbachawene kuwa licha ya hao,  kuna watumishi 145 ambao hajaonana nao huku akidai kuwa akimaliza kuonana nao huenda idadi ya watumishi hewa ikaongezeka.

Mkoa wa Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenelal Mstaafu Salum Kijuu alisema mkoa wake wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 14 ambao wamesababisha upotevu wa pesa za serikali Milioni 49.1

Mkoa wa Katavi.
Pia Mkuu wa mkoa huu, Jeneral Raphael Muhuga alisema mkuo huo umegundulika kuwepo kwa watumishi hewa 21 ambao wameitia hasara serikali Milioni 20.7.

Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Mkuo huyo, Bregedia Jenaral Mstaafu Emmanuel Maganga alisema katika mkuo huo wamebaini kuwepo watumishi hewa 171ambao wameitia hasara serikali milioni 114.6.

Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa huo,Merck Sadick alisema wamebaini mkoa wake unawatumishi hewa 111 ambao wameisababishia serikali hasara ya milini 281.4.

Mkoa wa Lindi
Kwa Upande wa Mkuu wa mkoa huo,Godfrey Zambi alisema mkoa wake unawatumishi hewa 57 ambao wameitia hasara serikali milini 36.2.

Mkoa wa Manyara.
Kwa Upande wake mkuu wa mkoa huo,Joel Bendera, alisema mkoa huo umekuwa na watumishi hewa 42 ambao wameitia hasara serikali Milioni milioni 313.9.

Mkoa wa Mara.
Kuhusu Mkuoa wa Mara,Mkuu wa mkoa huo,Magesa Mulongo alisema katika mkoa wake wamebaini kuna watumishi hewa 94 ambao wameitia hasara serikali milioni 121.

Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya,Mkuu wa Mkuo huo,Amos Makalla alisema katika mkoa wake kumekuwa na watumishi hewa 98 ambao pia wameitia hasara serikali Milioni 459 .6.

Mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa mkoa huo,Dkt Steven Kebwe,ambapo alisema mkoa wake umegundulika kuwepo na watumishi hewa 122 ambao wameitia hasara serikali milioni 450.7.

Mkoa wa Mtwara.
Mkuu wa mkoa huo, Halima Dendegu amesema mkoa wake umebainikika kuwepo kwa watumishi hewa 17, huku watumishi wengine 285 uchunguzi ukiendelea, ambapo watumishi hao 17 wameitia hasara serikali milioni 216.5.

Mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa John Mongella alisema mkoa wake umengundulika kuwa na watumishi hewa 334.

Mkoa wa Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Dkt Rehema Nchimbi alisema mkoa wake umekuwa na watumiwa na hewa 34 ambao amedai wamekuwa wakiitia hasara serikali Milioni 20.1.

Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Mkoa huyo,Mhandisi Evarist Ndikilo alisema Mkoa wake umekuwa na watumishi hewa 150 huku akishindwa kusema hasara ya fedha za serikali kwa madai kuwa uchunguzi unaendelea.

Mkua wa Rukwa.
Mkuu wa mkoa huo,Kamishna Mstaafu Zerote Steven alisema mkoa wake umekuwa na watumishi hewa, 18 na wametia hasara serikali milioni 55.6.

Mkuo wa Ruvuma,
Mkuu wa Mkoa huo,Thabiti Mwambungu alisema mkoa huo umekuwa na watumishi hewa 35 ambao wameitia hasara serikali milioni 58.4.

Mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa huo,Antony Mataka alisema mkoa huo umegundulika  kuwa na watumishi hewa 62  ambao wameitia hasara serikali ya Milioni 320.9.

Mkoa wa Singida,
Mkuu wa mkoa wa huo,Mhandisi Methew Mtigumwe alisema kuwa wafanyakazi hewa katika mkoa wake  ni 231 na kueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini zaidi.

Mkoa wa Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alianisha kuwa katika mkoa wake watumishi hewa ni 48 ambapo wanaitia hasara Serikali Milioni 118.7.

Mkoa wa Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela alisema kuwa watumishi hewa katika mkoa wake ni 104 ambapo alisema kuwa tathimini ya kuhakiki bado inaendelea.

Hata hivyo katika mkoa wa Shinyanga hali ilikuwa tofauti na mikoa mingine ambapo hadi sasa hakuna watumishi hewa kutokana na mikakati iliyowekwa  kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 na mkuu wa mkoa aliyepita.

Pia, Mkoa wa Songwe hauna  watumishi hewa kunatokana na kwamba mkoa huo ni mpya  na mkuu wake wa mkoa ameapishwa wiki moja iliyopita. 

RAIS MAGUFULI AZUNGUMZIA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI

$
0
0

Rais John Magufuli amewatoa hofu wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhusu uteuzi wao kwa kuwataka kuchapa kazi kwa bidii ili wawe na nafasi nzuri ya kuteuliwa badala ya kufanya kazi kwa wasiwasi jambo ambalo matokeo yake yatakuwa kuondolewa.

Dk Magufuli alitoa kauli hiyo juzi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Chato mara baada ya kutua kwa helikopta akitokea Mwanza kuelekea nyumbani kwake Kijiji cha Rubambangwe kwa mapumziko.

Akiwahutubia mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika uwanjani hapo, Dk Magufuli alisema anatambua kuwa bado hajachagua wakuu wa wilaya na wakurugenzi hali ambayo imewafanya baadhi yao kuwa na wasiwasi na kushindwa kutekeleza majukumu inavyotakiwa.

“Kama wewe ni mchapakazi mkuu wa wilaya, mkurugenzi una wasiwasi gani? Tena unapokuwa na wasiwasi ndivyo uwezekano wa kung’olewa unakuwa mkubwa,” alisema Dk Magufuli huku akishangiliwa na kuongeza:

“Lazima niwaambie waheshimiwa wakuu wa wilaya, ukiwa na wasiwasi hutafanya kazi na sisi tunakuona tu unafanya kazi kwa wasiwasi utaondoka tu kwani wasiwasi ni dalili nzuri ya kukufanya uondoke.”

Aliwatoa hofu akisema hata watakaoondolewa kwenye nafasi hizo watapangiwa kazi nyingine lakini akawaambia kwamba hata kama wataondolewa wasihofu kwani haitakuwa mbaya kwa kuwa hawakuzaliwa na ukurugenzi au ukuu wa wilaya.

Alisema Watanzania wanatakiwa kumwamini na kurudia kauli yake kwamba hatawaangusha akiahidi kuondoa kero ambazo zimegeuka mzigo kwa wananchi.

“Wako wengine walianza kulalamika natumbua mno majipu, siyo kutumbua tu ikiwezekana kuna mengine nitayakata kabisa na mguu wake, Tanzania lazima iwe yenye neema, haiwezekani kuwa na wafanyakazi 5,000 wanaolipwa mishahara mikubwa halafu Watanzania milioni 50 wanalia… nitakwenda kujibu nini kwa Mungu,” alisema.

Alisema ataendelea kuwatumbua (kuwawajibisha viongozi wazembe) hata kama wanafika 50,000 ilimradi Watanzania milioni 50 wapate neema ya kufaidika na rasilimali yao.

Alisema watu katika nchi hii wanaishi bila raha na kuwaahidi kuwa itapatikana kwa kila mmoja kufanya kazi kwa bidii hasa vijana na kuacha tabia ya kucheza pool huku mama zao wakienda shambani kulima na kusubiri kula tu.

BREAKING NEWZZ!!! BINTI AJINYONGA HUKO LONGIDO ...AACHA MAJINA YA WATU ANAOWADAI NA KUAGIZA WALIPE KABLA MAITI YAKE HAIJASAFIRISHWA

$
0
0

Binti mmoja anayejulikana kwa jina la Jesca ambaye ni mfanyakazi wa Longido Mountain Lodge amekutwa amejinyonga katika hotel ya Longido Mountain Lodge na kuacha ujumbe kuwa kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote 

Amesema amejinyonga kwa ridhaa yake mwenyewe.Katika ujumbe huo, ametaja majina ya watu anaowadai na kuagiza  walipe madeni yake kabla ya mwili wake kusafirishwa kwao pamoja na namba za Mama yake mzazi.
Mimi Jesca Reinald Elisante Leo tarehe 29 , 03 , 2016 nimeamua kujinyonga kwa ridhaa yangu mwenyewe hakuna mtu yeyote anayehusika na kifo changu na hizi ni namba ya Mama  yangu,0672740439.

Ninao wadai
Mama Diana  33,000/=
John Memory card 4 GB
Boss Mshahara 60,000/=

wanao nidai
Zai 20,000/=alipwe na ninao wadai wahakikishe wanalipa kabla sijarudishwa kwetu.

NB:HAKUNA ANAYEHUSIKA NA KIFO CHANGU.
Ndugu zangu nawapenda sana
vitu vyangu vyote vipelekwe kwetu
Jau Kwenye Kuni.

TRA YAKAMATA MAGARI MATANO YA TFF KUTOKANA NA MALIMBIKIZO YA KODI YA BILIONI 1.118

$
0
0

Mamlaka ya mapato nchini (TRA) imeibukia tena Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lakini safari hii haijapiga kufuli account za TFF badala yake imeondoka na magari matano yanayomilikiwa na shirikisho hilo kutokana na kulidai kiasi kikubwa cha kodi.

TRA imeamua kuchukua magari hayo ikitaka TFF kulipa deni la malimbikizo ya kodi mbalimbali wanayodaiwa ili warejeshewe magari yao.

Richard Kayombo ni afisa wa TRA amethibitisha kuyakamata magari hayo yanayomilikiwa na TFF lakini amefafanua sababu zilizopelekea kufanya hivyo.

“Ni kweli tumekamata magari matano ya TFF na hayo magari yamekamatwa kama sehemu ya mwendelezo wa kuweza kupata mapato yanayotokana na deni la kodi ambalo TFF hawajalipa.

“Mpaka sasa tunawadai billion 1.118 ambayo ni kodi mchanganyiko kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Ikumbukwe hapo nyuma tulikamata account zao kwasababu deni lilikuwa ni billion 1.6 na tukaweza kupunguza sehemu ya deni lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari matano.”

Hii ni mara ya pili kwa TFF kupigiwa hodi na TRA ikilalamikiwa kulimbikiza madeni ya kodi, mara ya kwanza TRA ilizifunga account zote za TFF lakini safari hii wameamua kuyashikilia magari yao.

Kwa mujibu wa Kayombo, magari hayo yapo kwenye yard ya YONO likiwemo basi ambalo hutumiwa kuisafirisha timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

BREAKING NEWS: LEMBELI ANENA BAADA YA MAHAKAMA KUTUPILIA MBALI KESI YAKE YA KUPINGA USHINDI WA UBUNGE KAHAMA MJINI

$
0
0
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Mahakama ya Wilaya ya KAHAMA bada ya hukumu kutolewa.
 
Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo imetupilia mbali maombi ya James Lembeli wa CHADEMA ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini wa Octoba, 25’2015, kwa madai kwamba taratibu zilikiukwa.

Akisoma hukumu iliyochukua saa tatu Jaji wa Mahakama hiyo Moses Mzuna amesema, ushahidi uliotolewa na upande wa Lembeli haukuwa na nguvu za kutosha kuishawishi mahakama hiyo kutengua matokeo ya uchaguzi kwani sehemu kubwa ni wa maneno.

Jaji Mzuna amesema, kitendo cha Lembeli kulalamikia vitendo vya rushwa vidavyodaiwa kufanywa na mgombe wa kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi-CCM Jumanne Kishimba kushindwa kuvitolea taarifa kwenye vyombo vya dola kimedhoofisha ushahidi na kuuwekea mashaka.

Kwa upande wa mashahidi waliounga mkono kuwepo kwa vitendo vya rushwa Jaji Mzuna amesema wameshindwa kujenga hoja kwa mlolongo unaofanana kiasi kwamba wameonekana kana kwamba walikuwa na ushahidi wa kutengenewa.

Amefafanua kuwa madai ya unyanyasaji wa wafuasi wake waliokamatwa na polisi katika hoteli ya Golden Rock na wengine katika kata ya Ngogwa yamekosa nguvu kufuatia kukosekana kwa kielelezo cha maandishi kinachoonesha kwamba walikuwa mawakala wake.

Mzuna amesisitiza, sababu ya Lembeli kushindwa kupeleka malalamiko kwenye kamati ya maadili ya uchaguzi iliwekwa kisheria kwamba hakuwa na muda wa kutosha haikubaliki kwa kuwa mpiga kura yeyote anayemuunga mkono angeweza kulalamika.

Kufuatia uamuzi huo wa mahakama kutupilia mbali maombi ya kutengua matokeo hayo Lembeli amesema anaiheshimu mahakama, na kwamba atashauriana na wakili wake kuona kama haki haikutendeka ili kukata rufaa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini aliyekuwa mlalamikiwa namba moja katika shauri hilo Kishimba alipohojiwa amesema Jaji ametenda haki kama walivyotenda haki wananchi wa kahama kwa kumpa kura za ushindi katika uchaguzi wa oktoba 25,2015.

Shauri hilo lilikuwa limevuta hisia za wananchi wa Kahama na kuhudhuria kwa wingi leo kwenye hukumu yake huku makundi ya kisiasa yaani wana-CCM na wana-CHADEMA yakijionesha wazi kwa kushangilia bila dalili zozote za uvunjifu wa Amani.

NSSF YAPIGWA MARUFUKU UJENZI WA MIRADI MIPYA

$
0
0

Bunge limesimamisha utekelezaji wa miradi yote mipya ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mpaka hapo Kamati na Wizara itakapopitia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), sambamba na kuitisha taarifa za utekelezaji wa miradi yote iliyofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

Aidha, imeagiza ukaguzi wa kina wa ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Makamu wa Rais kwa kuangalia usalama wa jengo, hesabu zilizotumika kama zinaendana na thamani ya jengo na kama washauri walitoa ushauri wao ipasavyo.

Akizungumza katika kuhitimisha ukaguzi wa miradi mbalimbali ya serikali iliyofanywa na Kamati ya Katiba na Sheria, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa alisema NSSF ilitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ikiwa haijitoshelezi kwa kutoonesha gharama zilizotumika mpaka sasa, bajeti iliyopangwa kutumiwa na kiasi kilichosalia ili kubaini kama fedha zilizotumika zinalingana na thamani ya ujenzi wenyewe.

Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa takribani siku tano kuanzia Machi 29, mwaka huu, ilitembelea Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu na Mahakama.

Akizungumzia taarifa za utekelezaji wa miradi iliyofanywa na mifuko yote ya hifadhi za jamii, Mchegerwa alisema kamati yake inataka kupitia taarifa zote za utekelezaji wa miradi sambamba na kupitia sera ya uwekezaji ili kuangalia kama yamefuata taratibu na hakuna upotoshaji.

“Kwanza kuna madeni makubwa ambayo mifuko hiyo inadai kwa wapangaji wao. Pia tunaangalia sera ya uwekezaji ili kujiridhisha kama ushauri wa kitaalamu uliotolewa unakidhi matakwa ya ujenzi unaoendelea.

Aliongeza: “Kuna majengo mengi yamejengwa hayana wapangaji lakini sera ya uwekezaji itatusaidia kujua kama inafuatwa. Pia itatusaidia kubaini mapungufu yaliyojiri, maana wajumbe wengi wana wasiwasi kuwa huenda ujenzi wa majengo unalenga kwa wahusika kupata asilimia 10 bila kuangalia mahitaji halisi, kwani majengo mengi yako wazi.”

MKUU WA MKOA WA MBEYA, AMOS MAKALLA AAGIZA HEKTA 5,000 ZIREJESHWE KWA WANANCHI

$
0
0

Mkuu  wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ameamuru hekta 5,000 za ardhi zilizokuwa za Chama cha Ushirika cha Luhanga Amcos zirejeshwe kwa wananchi wa kijiji cha Luhanga wilayani Mbarali kutokana na mchakato wa kutoa ardhi hiyo kuwa batili.

Makala alitoa agizo hilo jana mbele ya wakazi wa kijiji cha Luhanga, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo, huku akimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali, Jeremiah Mahinya kuwachukulia hatua viongozi wa kijiji waliohusika kutoa ardhi hiyo.

“Ardhi hiyo sasa ni ya wananchi kwa kuwa mchakato uliofanyika ni batili na lazima Mkurugenzi uchukue hatua dhidi ya yeyote aliyehusika kwenye mchakato huu. Iwe alighushi mihtasari au alifanya nini lazima achukuliwe hatua”, alisema.

Alisema wanachama wa Luhanga Amcos walikubaliana na kijiji hicho kupewa ekari 800 za ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo na wao kuahidi kuwa watasaidia kutatua tatizo la maji lililokuwa likiwakabili wakazi wa kijiji hicho ambao ni wakulima na wafugaji.

Hata hivyo, ilielezwa kuwa baadaye nyaraka zilibadilishwa na kubainisha kuwa ardhi waliyopewa wawekezaji hao ni hekta 5,000, hatua iliyoleta mkanganyiko na malumbano baina ya wananchi, uongozi wa kijiji na wawekezaji.

Alisema pamoja na malalamiko ya ongezeko kubwa la ardhi pia wawekezaji hao hawakutimiza ahadi ya kupeleka maji hadi sasa wakati wao wameanza kutumia sehemu ya ardhi waliyopora kwa kijiji hicho.

Makalla alisema, kurejeshwa kwa hekta 5,000 za ardhi kwa wananchi kunazingatia vigezo muhimu kikiwemo cha kijiji kutoruhusiwa kuuza au kutoa ardhi inayozidi ekari 50 kwa mtu yeyote sambamba na kutotimizwa kwa ahadi ya kupelekwa maji kijijini hapo.

Alisema kwa sasa serikali inahimiza kila mtu kujituma katika kazi lakini iwapo hakuna maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo vijana watakuwa wanaonewa pale inaposisitizwa kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu.

Aliitaja wilaya ya Mbarali kuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa migogoro mingi ya ardhi aliyosema mingine ni ya kujitakia au ile inayotokana na watendaji kutosikiliza wananchi.

MZAZI AMLAWITI MTOTO WA MWAKA MMOJA NA NUSU, SERIKALI YATOA TAMKO

$
0
0

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesikitishwa na kukemea vikali tukio la mzazi kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, kitendo kilichofanywa na John Donald (35) mkazi wa Kiyangu, Manispaa ya Mikindani mkoani Mtwara. 

Tukio hili la kubaka na kulawitiwa ni ukatili wa hali ya juu dhidi ya mtoto maana husababisha maumivu makali ikiwa ni pamoja na kumdhuru mtoto kimwili, kisaikolojia, kijamii na kihisia. 

Aidha, vitendo hivi, vinaacha kovu la kudumu kimwilini, kiakili, kimaadili, kijamii, ulemavu, maumivu, na wakati mwingine husababisha kifo; jambo ambalo linahitaji ulinzi thabiti katika kuhakikisha watoto wanaishi mazingira salama na rafiki. 

Ukatili aliofanyiwa mtoto eneo la Kinyangu, manispaa ya Mikindani, ni ukiukwaji mkubwa wa haki za mtoto ambao huchangia kurudisha nyuma ustawi na maendeleo ya Mtoto na ni kinyume cha Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009.

Wizara inatoa pongezi kwa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara kwa kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha mahakamani ili hatua za kisheria zichukuliwe. 

Vile vile, Wizara inaipongeza Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mkoani Dar es salaam dhidi ya  Omary hamisi (25), mkazi wa Gongo la Mboto, Dar es salaam, ya kutumikia kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka tisa mwenye ulemavu wa kusikia na kuongea. 

Uamuzi huu ni kielelezo kuwa, wananchi wakitoa ushahidi wa matukio ya ukatili dhidi ya watoto, watuhumiwa watachukuliwa hatua kali ili kuwa fundisho kwa wananchi wanaowanyanysa watoto.

Wizara inamwelekeza Afisa Ustawi wa Jamii na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Mtwara kuwasiliana na wadau wengine katika ngazi zote kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma ya afya na  ushauri na kufuatilia mwenendo wa shauri hili. 

Imetolewa na

Erasto Ching’oro
Msemaji wa Wizara
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

AFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KUMLAWITI MTOTO MLEMAVU WA KUSIKIA NA KUONGEA.

$
0
0

Mkazi wa Gongo la Mboto, Omary Hamis (25) amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka tisa ambaye ni mlemavu wa kusikia na kuongea.

Hakimu Mkazi, Flora Haule wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, alisema mahakama imeridhishwa na ushahidi wa mashahidi tisa ukiwamo wa daktari na fomu namba tatu ya polisi (PF3), iliyotolewa mahakamani hapo kama kielelezo dhidi ya mshtakiwa huyo.

“Mahakama imekukuta na hatia hivyo inakuhukumu kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na kosa la kumlawiti mvulana wa miaka tisa ambaye ni mlemavu wa kusikia na kuzungumza, ili iwe fundisho kwa jamii,” alisema hakimu Haule.

Katika ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, ilidaiwa kuwa mtoto huyo siku ya tukio alifika kwenye banda la kuonyeshea video ambalo linamilikiwa na Hamisi saa za jioni, kwa ajili ya kuangalia video, lakini Hamis alimfukuza kutokana na kutokuwa na pesa ya kiingilio.

Baada ya kumfukuza mtoto huyo aliondoka, lakini baadaye alirudi bila ya Hamis kuwa na taarifa akakaa ndani ya banda na kisha kupitiwa na usingizi uliosababisha abaki kwenye banda hilo peke yake hadi usiku.

Hamis alitumia mwanya huo kumlawiti mtoto huyo kwenye jumba bovu lililopo jirani na ofisi yake hiyo.

Mashahidi waliieleza mahakama kuwa walisikia sauti ya mtu ambayo ilikuwa haisikiki vizuri akiomba msaada, ndipo waliposogea na kumkuta Hamis akitekeleza kitendi hicho huku akijua kuwa ni kosa kisheria.

Mashahidi walidai hata walipomkaribia, Hamis aliendelea kutekeleza kitendo hicho hadi walipolazimika kumpiga mateke. Hamis alikiri kuwa siku hiyo watoto walifika kwenye banda lake hilo.

Wakili wa Serikali, Ester Kyara aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wote wanaotumia mabanda ya kuonyesha video kufanya ukatili kwa watoto.

Katika utetezi wake, Hamisi alisema ana familia inayomtegemea hivyo apunguziwe adhabu, maombi ambayo yalitupiliwa mbali na mahakama hiyo na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Hamisi anadaiwa kutenda kosa hilo Agost 26, 2014 eneo la Gongo la Mboto.

JESHI LA POLISI LAPEWA SIKU 7 LIWE LIMEPELEKA MIKATABA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)

$
0
0

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imelipa siku saba kuanzia jana Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi, iliyopewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima.

Hadi sasa kampuni hiyo imeshalipwa asilimia 99 ya fedha, ilihali vituo vilivyofunga mashine hizo ni 14 kati ya 108.

Maagizo ya kamati hiyo yaliyotolewa jana Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilal wakati kamati hiyo ilipokutana na Jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Aeshi alisema jeshi hilo mwaka 2011 liliingia mkataba na Kampuni ya Lugumi Enterprises kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima ambavyo viko 108.

Alisema mkataba huo ulikuwa wa Sh bilioni 37 pamoja na kodi na kwamba hadi sasa kampuni hiyo imeshapewa asilimia 99 ya fedha zote ili hali vituo vilivyofungwa mashine hizo ni 14 tu, kati ya vituo vyote 108.

“Ukiangalia kazi iliyofanywa tangu mwaka 2011 hadi leo ni kidogo na pesa hawa kampuni wameshachukua asilimia 99, sasa tumewaagiza watuletee huo mkataba ndani ya wiki moja walioingia na kampuni hiyo ili tuupitie,” alisema Aeshi.

Kuhusu mali zinazokamatwa na polisi kwenye matukio mbalimbali nchini yakiwemo ya wizi, Kamati imewaagiza CAG, Polisi na Mhakiki Mali wa Serikali kufanya ukaguzi wa mali zote zinazokamatwa na polisi ili kuzifahamu kuzipa thamani halisi kulingana na idadi yake.

Alisema hivi sasa mali zinazokamatwa na polisi hazifanyiwi uhakiki kujua idadi na thamani yake hivyo nyingi zinapotea bila kujua zilipokwenda na nyingine ambazo kesi zake zimeisha, zinauzwa kwa bei ndogo kuliko thamani halisi.

Kuhusu maduka ya bidhaa ya majeshi nchini, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeiomba serikali idhini ya ukaguzi na utoaji mizigo ya maduka ya jeshi bandarini ufanywe na jeshi hilo badala ya utaratibu wa sasa ambao mzabuni ndiye anayesimamia jambo hilo.

Akizungumzia hilo, Aeshi alisema maombi hayo ya jeshi yalitolewa wakati kamati hiyo ilipokutana na JWTZ juzi na kuomba ukaguzi wa bidhaa zinazoagizwa kwa ajili ya maduka yao zifanyiwe ukaguzi na wao kwani inawezekana bidhaa zinazoingizwa zikawa nyingi au zikachanganywa na vitu vingine kwa kuwa wao hawana dhamana ya kukagua.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Ernest Mangu alisema jeshi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile uhaba wa nyumba na kwamba mikakati yao hivi sasa ni kufanya mabadiliko na kulifanya jeshi hilo liwe la kisasa zaidi.

HATIMAYE UTUMISHI WAFAFANUA KUHUSU MSHAHARA WA RAIS MAGUFULI NA KIKWETE

$
0
0

OFISI ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) imefafanua kuhusu mshahara wa Rais John Magufuli ikisema kuwa mishahara ya watumishi wa umma na viongozi wa umma hupangwa katika bajeti, hivyo mshahara wa Rais ni ule ulioidhinishwa katika Bajeti ya mwaka 2015/16.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Dk Laurian Ndumbaro, bajeti ya mishahara yote ya watumishi wa umma na viongozi wa umma hupangwa kila wakati pale bajeti inapoandaliwa na kuidhinishwa na kwamba Rais mpya hakutengenezewa mshahara mpya.

“Wizara yetu ndiyo yenye dhamana ya mishahara ya watumishi wa umma na viongozi wa umma, na hii huandaliwa kila mwanzo wa mwaka kabla ya kuanza kwa mwaka mpya wa fedha. Kwa hiyo mwaka 2015/16 fedha zake ziliidhinishwa Juni mwaka jana na kuanza kutumika Julai,” alisema Dk Ndumbaro.

“Kwa hiyo, bajeti hiyo iliidhinishwa kwa viongozi wote, Rais, Makamu wa Rais, wabunge na watumishi wote wa umma. Hivyo, mshahara wa Rais, kwa mantiki hiyo, Rais Kikwete (Jakaya) ndio huo ambao unatumiwa na Rais John Magufuli. Kama mshahara, hakuna tofauti, hakuna mabadiliko, kiwango ni kile kile. Rais mpya hakutengenezewa mshahara mpya,” alifafanua Katibu Mkuu huyo wa Utumishi na Utawala Bora.

Kumekuwapo na taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari  kuhusu mshahara wa Rais na hivi karibuni, baadhi ya vyombo hivyo vilidai kuwa Rais mstaafu Kikwete alikuwa analipwa Sh milioni 34. 

Aidha, Rais Magufuli alikaririwa hivi karibuni akiwa nyumbani kwake Chato mkoani Kagera akisema kuwa analipwa mshahara wa Sh milioni 9.5 na akasema yupo tayari kuonyesha nyaraka zote.

BREAKING NEWZZZ!!! MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) ATEKETEA KWA MOTO AKIWA NDANI YA GARI LAKE

$
0
0

Mhadhiri  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta (CoICT), Dk Richard Mgaya amefariki baada ya kuteketea ndani ya gari lake jijini Dar es Salaam juzi.

Gari la Dk Mgaya liliteketea baada ya kugongana na lori katika eneo la Mbezi Africana, Wilaya ya Kinondoni usiku wa kuamkia juzi na kuwaka moto uliosababisha kifo chake.

Juzi picha mbalimbali zilisambaa zikionesha gari aina ya Toyota Prado lililopata ajali eneo hilo la Africana baada ya kugongana na lori, baadaye ilibainika kuwa aliyekuwa katika gari hilo ni Dk Mgaya.

Akizungumza  kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alisema gari la Dk Mgaya liliteketea na hata kushindwa kujulikana dereva wa gari hilo.

Alisema baadaye ndugu wa marehemu ndio walithibitisha kuwa gari hilo lililoteketea na dereva aliyekuwemo ni Dk Mgaya ambaye hata hivyo naye aliteketea ndani ya gari hilo.

“Lile gari liliungua na hakuna kitu kilichopatikana, hata wakati polisi wanafika eneo la tukio walikuta tayari dereva amekuwa majivu kutokana na kuteketea kwa moto… labda baada ya kupima vinasaba ndio itathibitika kama ilikuwa ni yeye,” alisema Kamanda Fuime.

Alisema hata gari hilo hawakuweza kulitambua mara moja na baada ya kufuatilia Mamlaka ya Mapato (TRA) ilibainika kuwa mmiliki wake ni Dk Mgaya.

Alisema “ndugu wa marehemu ndio wamesema kuwa ni ndugu yao.” 

Dk Mgaya alijiunga na idara hiyo miaka kadhaa iliyopita akitokea masomoni nchini Marekani na alikuwa ni mtaalamu wa artificial intelligence.

MISHAHARA YA VIGOGO WA SERIKALI WALIOKUWA WANALIPWA MILIONI 36 HADI MILIONI 40 KWA MWEZI YAANZA KUFYEKWA

$
0
0

Siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kutoa agizo la kupunguza mishahara mikubwa ya watendaji wa mashirika ya umma, hatimaye Serikali kupitia Bodi ya Mishahara imeanza kazi ya kufanya marekebisho hayo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Magufuli, kuagiza kushushwa kwa viwango vya mishahara ya viongozi wa mashirika ya umma ambapo wengine hulipwa Sh milioni 36 hadi milioni 40 kwa mwezi.

Jana  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alisema katika kipindi cha miezi 15 kuanzia sasa mishahara ya watumishi hao itapunguzwa na kuwa yenye uwiano.

“Katika kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa tunayo Bodi ya Mishahara ambayo ilianzishwa katika Serikali ya awamu ya nne na jukumu lake kubwa ni kufanya mapitio ya mishahara mbalimbali na kuhakikisha mishahara ya watumishi wa umma haipishani sana.

“Hatua ambazo tumeanza kuzitekeleza, tayari mamlaka zetu zimeanza kukutana kupitia Utumishi, Hazina na Msajili wa Hazina ili kuangalia namna ya kulitekeleza agizo hilo,” alisema Waziri Kairuki.

Alisema kutokana na hali hiyo mamlaka hizo hivi sasa zinaangalia mishahara ya taasisi mbalimbali na watumishi ili kuweza kubaini wale wanaolipwa zaidi ya Sh milioni 15 ni wangapi na itakatwa vipi.

Akizungumzia taasisi zinazozalisha kwa kiwango kikubwa na kuwa na uwezo wa kujiendesha, Waziri Kairuki, alisema Bodi ya Mishahara hivi sasa ina jukumu la kuangalia uwiano baina ya mtumishi wa umma na mashirika ya Serikali.

“Unakuta mtumishi wa taasisi X kiwango chake cha elimu, uzoefu, ujuzi, muda wa kuingia kazini pamoja na kazi anayoifanya ni sawa na ya mtumishi wa taasisi Y lakini unakuta mtumishi X analipwa mshahara mkubwa zaidi ya mara tano ya mtumishi Y jambo ambalo si haki katika utumishi,” alisema.

Kauli ya Rais Magufuli
Machi 30, mwaka huu akiwa wilayani Chato, Mkuu huyo wa nchi, alisema kuna watu wanalipwa kiwango kikubwa cha mishahara na wamekuwa wakiishi kuliko hata malaika na sasa ni lazima washushwe ili waishi kama shetani.

Hatua ya Rais Magufuli, kupitisha panga na kuweka uwiano wa mishahara kwa watendaji wa taasisi hizo unaelezwa kuwa utaisaidia uwajibikaji na usawa kwa watendaji.

Katika mkutano huo, Rais Magufuli, alishangazwa na baadhi ya bodi za wakurugenzi kushindwa kufanyakazi zao kwa mujibu wa sheria na badala yake wamekuwa na kazi ya kupandisha mishahara kwa watendaji.

Alisema anashangazwa na bodi hizo, kwani kila kukicha zimekuwa zikifanya kazi ya kupandisha mishahara pamoja na kufanya vikao nje ya nchi.

Alisema hivi sasa ameunda timu ya wataalamu ambayo imeanza kufanya kazi ya upunguzaji mishahara mikubwa kwa watendaji wakuu wa mashirika ya umma.

“Tena hawa wakurugenzi ndio wanaongoza kwa kulipwa fedha nyingi na hata kwenda kufanya vikao ulaya. Ninasema hapa kwamba suala hili litaanza kushughulikiwa katika bajeti hivi karibuni,” alisema Rais Magufuli.

Alisema tayari ameunda timu ya wataalamu ambayo inafanya kazi ya kupunguza mishahara hiyo na kufikia Sh milioni 15 kwa mwezi ili asipatikane Mtanzania anayelipwa zaidi ya kiwango hicho.

“Kuna watu wanaishi kuliko hata malaika lazima tuwashushe waishi kama shetani,” alisema Rais Magufuli.

DR. SHEIN: UPINZANI HAUJAKIDHI VIGEZO VYA KUTOA MAKAMU WA RAIS

$
0
0
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema hakuna chama kilichokidhi matakwa ya kikatiba kutoa makamu wa kwanza wa Rais.

Rais Shein aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na Baraza la Wawakilishi visiwani Zanzibar kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake kwa mara ya pili kuongoza Umma wa Wazanzibar.

''Hakuna Chama chama kinachokidhi kutoa makamu wa kwanza wa Rais huo ni uamuzi wa wananchi na ni uamuzi wa kidemokrasia unaostahili kuheshimiwa ''Alisema Rais Shein.

Aidha Rais Shein katika hotuba yake kwa Baraza hipo pamoja na wananchi wa Zanzibar aliahidi kuhakikisha Zanzibar inasonga mbele kimaendeleo kwa kujenga viwanda maeneo mbalimbali na kuboresha huduma za kijamii pamoja na kupandisha mishahara hadi kufikia shilingi laki 3 kwa kima cha chini.

Pia Rais Shein alisema ataongoza Zanzibar kwa haki na watu wote ni lazima wafahamu kwamba yeye ndiye Rais ambaye alichaguliwa kwa asilimia 91.4 hivyo uchaguzi haupo tena hadi mwaka 2020.

RAIS MAGUFULI NA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME WAZINDUA RASMI DARAJA LA KIMATAIFA LA RUSUMO NA KITUO CHA HUDUMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi daraja hilo la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

Ujenzi wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma Pamoja Mpakani Rusumo ni moja ya miradi inayotekelezwa kwa msaada kutoka Serikali ya Japan kwa Nchi za Tanzania na Rwanda kupitia shirika lake la maendeleo la JICA. 

Mradi huu kwa upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha TShs. 33,206,508,072.07 hadi kukamilika. Miradi mingine inayotekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia JICA ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa – Dodoma, Namtumbo – Kilimasera – Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya Masasi - Mangaka. 
 Muonekano wa sehemu ya Daraja hilo la Rusumo
 Jiwe la msingi lililowekwa baada ya uzinduzi wa daraja hilo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakipita kwenye Daraja hilo la Rusumo mara baada ya uzinduzi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi  wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
 Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huo

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI YA APRIL 7

$
0
0

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI YA APRIL 7


BAJETI YA SERIKALI 2016/ 2017 NI TRILIONI 29.5.....MATUMIZI YA KAWAIDA NI TRILIONI 17.7, MIKOPO NI TRILIONI 11.1. BOFYA HAPA KUONA VIPAUMBELE VILIVYOTAJWA

$
0
0
Bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano itaizidi ya Serikali ya Awamu ya Nne kwa Sh7.1 trilioni baada ya Waziri wa Fedha kutangaza sura ya bajeti ya mwaka 2016/17 inayoonyesha kutakuwa na makusanyo na matumizi ya Sh29.5 trilioni.

Sura hiyo ya bajeti ya mwaka 2016/17 inatofautiana na iliyopita iliyokuwa ya Sh22.45 trilioni katika maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na kiwango cha fedha kitakachotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo, ambacho ni zaidi ya mara mbili ya fedha za eneo hilo katika bajeti iliyopita.

Waziri wa Fedha, Dk Phillip Mpango alisema wakati akiwasilisha mapendekezo ya kiwango cha ukomo wa bajeti jijini Dar es Salaam jana kuwa kati ya fedha hizo, Sh18.46 trilioni, ambazo ni sawa na asilimia 62.5 ya bajeti yote, zitatokana na jumla ya mapato ya ndani yanayohusisha na halmashauri.

Kiwango hicho kimezidi Sh3.64 trilioni ya bajeti iliyopita ambayo ililenga kukusanya Sh14.82 trilioni.

“Kati ya mapato hayo, Serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi ya jumla ya Sh15,105 bilioni, sawa na asilimia 82 ya mapato ya ndani,”alisema Dk Mpango.

Alisema makisio ya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi yameongezeka kwa kuwa kuna viashiria vingi vinavyoonyesha kwamba Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kushirikiana na wizara na taasisi zinazokusanya maduhuli, zina uwezo wa kukusanya kiasi hicho.

Alisema: “Kipaumbele cha kwanza cha Serikali kitakuwa ni kujizatiti katika ukusanyaji wa mapato kwa kubuni vyanzo vipya na kuendelea kudhibiti mianya mbalimbali ya ukwepaji wa kodi. Suala hili linahitaji ushirikiano wa karibu na wananchi ili tujiletee maendeleo ya haraka kwa kushiriki kulipa kodi na kuwafichua wakwepa kodi kwa kuwaona kama maadui wa maendeleo yetu.”

Kwa mujibu wa Dk Mpango, Sh17.72 trilioni zitakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, wakati Sh11.82 trilioni, sawa na asilimia 40 ya bajeti nzima, zimetengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Katika bajeti iliyopita, matumizi ya kawaida yalitengewa Sh16.7 trilioni, sawa na asilimia 74.3 wakati shughuli za maendeleo zilipangiwa Sh5.76 sawa na asilimia 25.9.

“Asilimia 40 kwenda kwenye mipango ya maendeleo, hili ni jambo jema,” alisema Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, alipoongea na waandishi.

“Kwamba tumepunguza matumizi ya kawaida ya Serikali na kuelekeza fedha zaidi kwenye mipango ya maendeleo, nasema hili ni jambo jema kama litatekelezeka.” 

Vipaumbele 
Kwa mujibu wa Dk Mpango, shughuli zitakazopewa kipaumbele kwenye mipango hiyo ya maendeleo zimegawanywa katika maeneo manne ambayo ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda, kufungamanisha maendeleo ya uchumi na rasilimali watu, mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji na pia usimamizi wa utekelezaji wa mpango.

Dk Mpango alisema washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia Sh3.6 trilioni, ikiwa ni ongezeko la Sh1.7 trilioni kulinganisha na Sh1.88 trilioni zilizokuwa zinategemewa kwenye bajeti iliyopita.

Fedha hizo zitakuwa za misaada na mikopo nafuu kutoka nje ambayo ni pamoja na GBS, Basket Fund na miradi ya maendeleo.

Aidha Serikali inatarajia kukopa Sh5,374.3 bilioni kutoka soko la ndani kwa ajili ya kulipia hati fungani na dhamana za Serikali zinazoiva pamoja, wakati kutoka kwenye soko la nje kwa masharti ya kibiashara inatarajia kukopa Sh2.1 trilioni.

Awali Spika Job Ndugai alisema kwa mujibu wa utaratibu mapendezo hayo yalipaswa kuwasilishwa tangu Machi 11, lakini kutokana na ratiba za wabunge wengi kuwa kwenye majimbo yao, aliamua kuongeza siku.

“ Sasa ninawashauri wabunge wote kwenda kuyasoma mapendekezo hayo vyema ili mpate nafasi ya kuchangia fedha bajeti itakapowasilishwa bungeni. Pia mhudhurie kwenye vikao vya kamati zenu ili kujipanga vyema. Wale watakaokuwa hawaonekani kwenye vikao, tutawasilisha majina yao kwenye vyama vyao ili wachukuliwe hatua zinazostahili.”

Miradi ya maendeleo 
Katika kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi, Dk Mpango alisema sera za mapato kwa mwaka 2016/2017 itajielekeza kufanya tathimini ya mkupuo ya majengo ili kuongeza mapato.

Katika mpango wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, Dk Mpango alisema kipaumbele kitakuwa ni mradi wa magadi soda ulioko kwenye Bonde la Engaruka ambako utafiti umebaini kuna magadi ya mita za ujazo bilioni 4.68 ambazo huongezeka kila mwaka kwa mita milioni 1.9 za ujazo.

“Mradi utahusisha kiwanda cha kuzalisha tani milioni moja za magadi kwa mwaka kwa ajili ya matumizi ya viwanda, hususan madawa, vioo na sabuni,” alisema.

Mradi huo utakapokamilika utaliingizia taifa Sh 400 bilioni kwa mwaka.

Eneo jingine ni kufufua kiwanda cha General Tyre cha Arusha, ambacho kimetengewa Sh2 bilioni kwa kazi hiyo. Pia kiwanda cha viuadudu kilichopo Kibaha mkoani Pwani ambacho mradi wake utatekelezwa kwa awamu tatu, mbili za mwisho zikihusisha ujenzi wa kiwanda cha mbolea na cha virutubisho.

Pia mpango huo utahusisha uendelezaji wa viwanda vidogo mkoani Morogoro, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza.

Katika kufunganisha maendeleo ya uchumi na rasilimali watu, Serikali itaweka nguvu kwenye elimu na mafunzo ya ufundi, ikihusisha kuimarisha mifumo, majengo na miundombinu katika shule za awali, msingi na sekondari.

Pia itahusisha ukarabati, upanuzi na ujenzi wa vyuo vikuu, mradi wa upanuzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (Mkwawa, Duce, Udom na OUT, Ardhi, Mzumbe, Sokoine, Muhimbili, Ushirika, Chuo Kikuu cha Sayansi cha Mwalimu Nyerere na pia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Eneo hilo litahusisha uendelezaji ustawi wa jamii kwa kuangalia huduma za afya, maji, kazi na ajira, na uwezeshaji wananchi kwa kutoa Sh50 milioni kwa kila kijiji.

Mazingira wezeshi 
Katika kujenga mazingira wezeshi, Serikali itaongeza uwezo wa uzalishaji umeme, usambazaji umeme mijini na vijijini, ujenzi wa kiwanda cha kupokea, kuchakata na kubadilisha gesi asilia kuwa katika kimiminika kwa ajili ya kusafirisha nje, ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha gesi asilia, ujenzi wa miundombinu ya usafiri, teknolojia ya habari na mawasiliano, miradi ya makaa ya mawe na mradi wa chuma wa Liganga.
Viewing all 2674 articles
Browse latest View live