↧
SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO MPYA WA DIAMOND- UNAITWA CCM NO. 1
↧
NIMEKUWEKEA HAPA WIMBO MPYA WA SNAIDA- Unaitwa UKAWA TAIFA KUBWA,USIKILIZE NA UU DOWNLOAD HAPA
↧
↧
MAFURIKO YA JANGWANI YAHAMIA SHINYANGA,ZIKO HAPA PICHA 38 ZA MKUTANO WA CHADEMA/UKAWA ZA UFUNGUZI WA KAMPENI JIMBO LA SHINYANGA MJINI,LEMBELI AFUNGUKA KUHUSU MAGUFULI NA WASUKUMA
Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako maelfu ya wakazi wa Shinyanga wamefurika katika uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi mkuu ujao wilaya ya Shinyanga hususani jimbo la Shinyanga Mjini.Mkutano huo umeongozwa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema ndugu Patrobas Katambi maarufu kwa jina la "Mzimu wa Shelembi".
Viongozi wengine machachari waliohudhuria mkutano huo ni mgombea ubunge kupitia Chadema jimbo la Kahama mjini mheshimiwa James Lembeli,mgombea ubunge jimbo la Kishapu Fred Mpendazoe na mgombea ubunge jimbo la Msalala kupitia Chadema ndugu Paul Malaika.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog Kadama Malunde, alikuwepo eneo la tukio ametusogezea picha 38,Angalia hapa chini
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Ukawa/Chadema katika jimbo la Shinyanga
Makamanda wa Ukawa wakiwa meza kuu
Wagombea udiwani kupitia Ukawa katika kata 17 za manispaa ya Shinyanga wakitambulishwa wakati wa mkutano huo
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano
Makamanda wa Ukawa na wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Msalala Paul Malaika akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo alisema hata kama kuna mgombea mwenye sifa nzuri ndani ya CCM wananchi wasimchague kutokana na kwamba mfumo mzima wa CCM ni mbovu hivyo wafanye mabadiliko kwa kuiweka Ukawa madarakani
Mkutano unaendelea
Mgombea ubunge jimbo la Kishapu kupitia Ukawa ndugu Fred Mpendazoe akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka watanzania kukubali mabadiliko kwani CCM imechoka huku akisisitiza kuwa mgombea urais wa CCM John Magufuli hana kabila zaidi ya kabila la CCM ambayo kamwe haiwezi kutoa rais bora
Mkutano unaendelea
Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Uenezi kanda ya ziwa Chadema Juma Protas akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni ambapo aliwasisitiza wananchi kuchagua viongozi wa Ukawa ambayo ndiyo mwarobaini wa maendeleo ya watanzania
Mgombea Ubunge jimbo la Kahama mjini James Lembeli akikaribishwa jukwaani kwa ajili ya kuzungumza na wakazi wa Shinyanga
Mgombea ubunge wa jimbo la Kahama mjini mkoa wa Shinyanga wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kupitia Ukawa James Lembeli akiuzngumza katika mkutano huo ambapo aliwataka watanzania kupuuza propaganda inayoenezwa kuwa mgombea urais wa CCM Dkt John Magufuli kuwa ni msukuma ili kuwarubuni watu wa kanda ya ziwa wampatie kura.
Lembeli alisema hakubaliani na propaganda kuwa Magufuli kuwa ni msukuma hivyo wasukuma wamuunge mkono kutokana na kutokuwa na msaada wowote kutetea haki za wasukuma akitoa kuwa wakati akiwa mwenyekiti wa kamati ya bunge iliyochunguza dhambi na shida waliyopatiwa wafugaji wakiwemo wasukuma ambao waliuawa,waliteswa na kuibiwa mali zao ,Magufuli anayedaiwa kuwa ni Msukuma hakufungua mdomo wake kutetea wafugaji/wasukuma dhidi ya matatizo yaliyowakuta.
Wakazi wa Shinyanga wakimshangilia James Lembeli
Lembeli aliongeza kuwa kutokana na kitendo hicho cha kukaa kimya dhidi ya vitendo vya wafugaji hao inadhihirisha kuwa hayuko pamoja na wasukuma hivyo asionewe huruma bali watanzania wamchague Edward Lowassa ambaye ni jasiri na msema kweli.
Mheshimiwa James Lembeli akimwombea kura mgombea urais wa Ukawa mheshimiwa Edward Lowassa na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi kwa wakazi wa Shinyanga
Lembeli alitumia fursa hiyo kuwataka Wafuasi wa CCM wenye uchu wa kufanya mabadiliko na kiu ya maendeleo wahamie Ukawa mara moja kwani kuna watu ambao walikuwa na nguvu kubwa ndani ya CCM wamefanya maamuzi akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga baada ya kuchoshwa na madudu ya CCM.
Mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alisema pamoja na hujuma anazofanyiwa na baadhi ya watu wakiwemo wafuasi wa CCM akiwemo mgombea ubunge wa CCM jimbo hilo Stephen Masele hatakata tamaa kuwapigania haki wananchi na kwamba yuko tayari kufa kwa ajili ya wananchi
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakimsikiliza mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi
Katambi alizungumzia pia sakata la kutekwa kwake kisha kuchaniwa fomu zake za ubunge sambamba na kufunguliwa mashtaka ya kupinga ubunge wake ambapo alisema alipambana kuhakikisha kuwa jimbo hilo haliendi CCM na atahakikisha kuwa CCM haishindi katika jimbo hilo
Katambi alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa Shinyanga kukubali mabadiliko na hata ikitokea akafariki wakati mapambano ya kuiondoa CCM madarakani yakiendelea wasikate tamaa wasonge mbele
Mkutano unaendelea
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo wa Ukawa/Chadema
Mgombea huyo wa ubunge wa Chadema katika jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi amewataka wanaShinyanga kushikamana na kuepuka vitendo vya usaliti na kuhakikisha kuwa wanawapa kura wagombea wa Ukawa badala ya kushangilia pekee kwenye mikutano.
Mkutano unaendelea
Kulia ni mgombea udiwani kata ya Shinyanga mjini atakayechuana na aliyekuwa meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukaam(CCM) akitambulishwa kwa wakazi wa Shinyanga
Mheshimiwa James Lembeli na fimbo yake ya kimila akimsikiliza kwa umakini zaidi mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi
Mkutano unaendelea
Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas akizungumza katika mkutano huo
Wananchi wakiwa wamenyoosha mikono baada ya kuulizwa kama wako tayari kuleta mabadiliko katika jimbo la Shinyanga mjini na nchi kwa ujumla
Katambi alisema tayari wasaliti wa Chadema wameshajulikana na kuapa kutokata tamaa katika kuwapigania haki wananchi huku akiwataka wakazi wa Shinyanga kumpa kura nyingi Lowassa,wabunge wa Ukawa na madiwani wote wa Ukawa
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Makamanda wa Ukawa wakifurahia jambo eneo la mkutano
Makamanda wa Ukawa wakiwa eneo la tukio
Katambi akizungumza na wakazi wa Shinyanga leo ambpo alivitaja baadhi ya vipaumbele vyake kuwa ni elimu,kilimo na ufugaji,viwanda,kupambana na umaskini,ujinga na malazi..
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
↧
PERUZI HAPA MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMATATU AGOSTI 31,2015- UDAKU,MICHEZO NA HARD NEWS
↧
MGOMBEA URAIS WA UKAWA EDWARD LOWASSA ADAI ANAHITAJI KURA MILIONI 10 TU

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa Gangilonga Iringa Mjini uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji huo, Lowassa aliyeambatana na Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye alisema vyama tawala vilivyokuwa rafiki na CCM vimeshang’oka madarakani na kwamba hivi sasa ni zamu ya chama hicho tawala kuondolewa.
“Nataka kura nyingi ili hata wakiiba tushinde, asilimia 90 ziwe zetu hizo 10 waache waibe. Msipoiondoa CCM mwaka huu hatutaiondoa tena, CCM na Tanu walikuwa na marafiki zao lakini karibu wote wameondoka.
“Chama cha Kanu cha nchini Kenya kimeshaondoka madarakani, kile cha Malawi (Malawi Congress Party) nacho kimeondoka, UNIP (The United National Independence Party cha Zambia) nacho imeondoka na kile chama cha Mzee Obote (Dk Militon) cha Uganda kimeondoka, tunaona pia jinsi Rais wa Zimbabwe (Robert Mugabe) anavyohangaika,” alisema Lowassa.
Katika mkutano huo, Lowassa alirudia vipaumbele vya ilani ya uchaguzi ya Ukawa, huku akimponda mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya CCM, Frederick Mwakalebela kuwa hawezi kushinda kwa maelezo kuwa amepanda gari bovu.
Sumaye alieleza ufisadi mbalimbali uliotokea tangu Lowassa alipojiuzulu mwaka 2008, huku akihoji yalipo majina ya wauza dawa za kulevya na majangili ambayo alidai kwa nyakati tofauti Rais Jakaya Kikwete amenukuliwa akisema kuwa anayo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi ambao walianza kufika uwanjani saa nne asubuhi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Baada ya kumalizika kwa mkutano huo saa 11.58 jioni, baadhi ya wananchi hao walilisukuma gari la Lowassa na mgombea ubunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa hadi katikati ya mji huo kabla ya magari hayo kushika kasi na kuwaacha wakiendelea kukimbia barabarani huku wakiimba nyimbo mbalimbali.
Baadhi yao walionekana kubeba kitu mfano wa jeneza na kukivisha bendera ya CCM huku wakisema mwisho wa chama hicho tawala ni Oktoba 25.
Aomba kura milioni 10
Akiwa Mafinga Mjini, Lowassa alisema anahitaji Watanzania wampigie kura si chini ya milioni 10.2 ili awe rais na kumaliza kilio cha wakulima nchini.
Akiwa katika siku ya kwanza ya kampeni zake mikoani hapa, Lowassa aliwaeleza wananchi wa Mafinga kuwa amechoshwa na manyanyaso ambayo wakulima wanaendelea kuyapata ikiwamo kukopwa mazao yao na kutozwa ushuru na Serikali bila ya wao kupata faida yoyote.
Lowassa alisema mara atakapochaguliwa kuongoza nchi, kitu kikubwa atakachokifanya kuwasaidia wakulima ni kufuta ushuru wote wa mazao na kuhakikisha wananufaika na jasho wanalolitoa wakati wa kilimo.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Wambi, Mjini Mafinga, Lowassa alisema: “Nakataa wakulima kuendelea kukopwa mazao yao na kutozwa ushuru, kuendelea kufanya hivi ni kuwanyonya na kutaka waendelee kuwa maskini wakati wao wanafanya kazi kwa kujituma sana.”
Alisema hayo yatafanyika iwapo wananchi watampigia kura za kutosha na kuzilinda huku akigusia madai kwamba CCM ni wezi wa kura na kubainisha kuwa maneno hayo si ya kubeza wala kuyafumbia macho.
“Mimi nataka kila mtu akihifadhi vizuri kichinjio chake (kadi ya kupigia kura) na siku ya kupiga kura ikifika nawaomba wanawake kwa wanaume wajitokeze kwenda kupiga kura ila kina baba ninawaomba mkishapiga kura fanyeni kazi ya kuzilinda kura zenu,” alisema Lowassa na kuongeza: “Kweli CCM ni wajanja sana kazi tunayotakiwa kufanya ni kuziba mianya yote, hata kama tukipigwa chenga wawe wamepata asilimia 10 ili asilimia 90 zibaki kwetu.”
Sumaye: Tunataka wabunge 300
Akizungumza katika mkutano huo, Sumaye aliwataka wananchi wa Mafinga kutokuwa na shaka na Ukawa kwa sababu wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika uchaguzi wa Oktoba 25, licha ya CCM kujipanga kupata ushindi wa goli la mkono.
“Tunawaomba Watanzania wachague Ukawa kwa sababu umefika muda wa mabadiliko, tunataka tupate wabunge 300, hizo nafasi nyingine wagawane vyama vingine vilivyo nje ya Ukawa,” alisema Sumaye.
Alisema Serikali ya sasa ni dhaifu kwa sababu wamekuwa wakipeana nafasi ya uongozi kindugu na ushikaji, hali inayofanya wananchi kuendelea kupata shida.
“Tumemwambia Lowassa akichaguliwa anatakiwa kuunda Serikali inayowajibika kwa umma tofauti ya Serikali iliyopo sasa madarakani, chama kinapokuwa madarakani kwa muda mrefu kinajenga kiburi na dharau kwa wananchi wake na ndivyo inavyofanya CCM sasa, ni muda wake kuondoka madarakani,” alisema Sumaye.
Sumaye alisema amekuwa akisikia CCM wakisema Magufuli hana utani na rushwa wakati amekuwa waziri wa ujenzi kwa miaka kadhaa na bado kumekuwa na tuhuma za rushwa katika sekta ya ujenzi.
“Nataka kumuuliza Magufuli, yeye ni waziri wa ujenzi, ameshindwa kitu gani kuondoa rushwa katika wizara yake halafu anakuja kusema akiwa rais ataweza?” alihoji Sumaye.
Katika mkutano wa pili wa Lowassa uliofanyika katika Uwanja wa Maendeleo wa (FDC), Ilula katika Jimbo la Kilolo, aliwataka wananchi wamchague ili awaondolee kero zinazowakabili ikiwamo ya ukosefu wa maji.
Katika uwanja huo uliofurika huku wananchi wakiwa na mabango mbalimbali yanayoeleza kero zinazowabali, Lowassa aliwataka wasiwe na hofu na yeye katika kutatua kero za maji na kama wanabisha wawaulize wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ambao walihangaika kwa muda mrefu na kero ya maji lakini aliwezesha mkoa huo kupata maji kutoka Ziwa Victoria.
Alisema atahakikisha elimu inapanda kwa kasi ili kupunguza umaskini. “Najivunia na ujenzi wa shule za kata nchini kwani Mkoa wa Iringa ulikuwa maarufu kwa kutoa wasichana wanaokwenda kufanya kazi za majumbani, lakini kwa sasa kuwapata imekuwa shida baada ya kupatikana shule hizo ambazo zimeleta mapinduzi hayo,” alisema Lowassa.
Kuhujumiwa
Lowassa alisema Ukawa wamekuwa wakihujumiwa katika mchakato wa uchaguzi ikiwamo kukataliwa kufanya mambo kadhaa na kukatwa umeme pindi mikutano ya hadhara ya chama hicho inapokuwa ikirushwa moja kwa moja na televisheni.
“Hata wakikakata umeme, CCM hawatatuweza, wamezoea kutuhujumu ila tarehe 25, mwezi Oktoba hawawezi kukata umeme kwenye vichwa vya watu wanaotaka mabadiliko."
↧
↧
POLISI YAKAMATA MAJAMBAZI 38 YAKIWA NA SILAHA NZITO PAMOJA NA MILIONI 170......MAJAMBAZI HAYO YANADAIWA NA MAFUNZO YA KIJESHI
Jeshi la Polisi limewakamata watu 38 wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi ambao pia wamepatiwa mafunzo ya kigaidi katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Lindi.
Sambamba na kukamatwa watu hao, polisi pia imekamata bunduki 10, risasi 300 na bomu moja la mkono.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna, Suleiman Kova ametangaza leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kova aliongeza kuwa watuhumiwa hao pia wanajihusisha na kutoa mafunzo ya kigaidi.
‘’ Hawa tumefanikiwa kuwakamata, tunawaita majambazi au magaidi kwa kuwa licha ya kufanya ujambazi pia wanajihusisha na kutoa mafunzo ya kigaidi katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Lindi,’’alisema Kamanda Kova.
Amesema kuwa polisi wamefanikiwa kuwanasa watu hao ikiwa ni operesheni endelevu ya kuwasaka wahalifu wote wanaovunja amani hapa nchini.
Ameeleza kuwa baadhi ya silaha zilikamatwa zikiwa zimefichwa maeneo ya Mkuranga mkoani Pwani ambapo baadhi ya silaha hizo tayari zilikuwa zimeshapata kutu.
Kamanda Kova amesisitiza kuwa polisi wanaendelea na upelelezi na ukishakamilika watuhumiwa hao watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Mpekuzi blog
↧
JESHI LA WANANCHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) LAANDAA SHEREHE ZA KUMUAGA RAIS KIKWETE
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinaandaa sherehe ya kumuaga Amiri Jeshi Mkuu tarehe 01 Septemba 2015 kwa gwaride rasmi litakalofanyika katika viwanja vya Uhuru, kuanzia saa 2.00 Asubuhi hadi saa 6.30 mchana.
Waandishi wa Habari mnakaribishwa katika uwanja wa Taifa kwa ajili ya Coverage ya tukio hilo la kihistoria.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756 - 342279
0783- 309963.
Mpekuzi blog
↧
WANANCHI WAFUNGA BARABARA BAADA YA GARI LA POLISI KUGONGA WANAFUNZI WAWILI
Wananchi wa eneo la Misugusugu Wilayani Kibaha Mkoani Pwani hii leo wamefunga barabara baada ya Wanafunzi wawili kugongwa na gari la Jeshi la Polisi na kupelekea kifo cha Mwanafunzi Mmoja
Akiongea na Mtandao huu, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Jaffary Mohammed amesema baada ya tukio hilo Wanachi walifunga barabara kutokana na hasira ya tukio lakini jeshi la Polisi limetuliza hali na linamshikilia Dereva wa gari hilo kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda Jaffary ameongeza kuwa katika tukio hilo Mwanafunzi aliejeruhiwa amelazwa katika hospitali ya Tumbi na mwili wa marehemu upo mochwari katika hosptali hiyo.
Aidha Jaffari ameongeza kuwa kwa sasa hali ya kiusalama imetulia baada ya jeshi la polisi kutuliza hali iliyojitokeza huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi na badala yale wafuate sheria.
Katika hatua nyingine amewataka madereva wafate sheria za barabarani kwa kufuata alama zilizowekwa pamoja na kupunguza mwendo katika maeneo ya watu ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
Mpekuzi blog
↧
PITIA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPT 01,2015, KWA HABARI ZOTE ZA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS NIMEKUWEKEA HAPA
↧
↧
SAMWEL SITTA AWAJIBU UKAWA
Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta amesema serikali italifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATC) ili liweze kununua ndege nne na kuanza biashara.
Sitta pia amesema Rais Jakaya Kikwete atazindua ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha `standard gauge’ itakayogharimu Sh16 trilioni huku akiwataka viongozi wa vyama vya upinzani kuacha kuiba mipango ya serikali ya CCM.
Sitta amesema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar ikiwa ni siku chache baada ya mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akifungua kampeni za chama hicho katika uwanja wa Jangwani, alisema akichaguliwa atajenga upya reli ya kati na kufufua ATC.
Waziri Sitta alisema anashangazwa na wapinzani kusema watajenga reli na kufufua ATC wakati hiyo ni ni mipango ya serikali ya CCM ambayo utekelezaji unaanza kabla ya uchaguzi.
Akifafanua, alisema Rais Kikwete Septemba 15 mwaka huu atazindua ujenzi wa reli katika eneo la Soga Mpiji wilayani Kisarawe na fedha hizo zitatoka katika benki ya Rolthschild ya Marekani.
↧
LOWASSA APOKELEWA KIFALME NJOMBE........HAPA KUNA PICHA 14 ZA MAFURIKO YAKE

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwasili kwenye viwanja vya Shirika la Nyumba (National Housing) Mjini Njombe tayari kwa kuhutubia Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu, anazoendelea kuzifanya kwa nchi nzima. Picha zote na Othman Michuzi, Njombe.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Makambako, waliofurika kwa wingi wenye Polisi Makambako, Mkoani Mkoani Njombe Agosti 31, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake.
Katika hotuba yake, Mh. Lowassa amewatoa hofu wana CCM wanaotaka kujiunga na Ukawa kutoogopa kuchukua uamuzi huo kwani huu ni mwaka wa mabadiliko.
Pia amewaomba Watanzania wanaomuunga mkono katika mikutano yake ya hadhara kutoishia hapo na badala yake kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa Mwaka huu wa Oktoba 25 mwaka huu.



Sehemu ya wananchi wa Mji wa Makambako, wakishangilia hotuba ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipongeza na baadhi ya Wagombea Udiwaki wa Kata mbali mbali za Mji wa Makambako, Mkoani Njombe baada ya kuhutubia Mkutano wake wa Kampeni.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Makambako, Mhema Oraph, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi Makambako, Mkoani Mkoani Njombe Agosti 31, 2015.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Polisi Makambako, Mkoani Mkoani Njombe Agosti 31, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, na kuhudhuliwa na umati wa wananchi wakazi wa maeneo mbali mbali ya Mji wa Makambako.




↧
MAGUFULI ATIKISA SONGEA......AWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA MAREHEMU KAPTENI JOHN KOMBA
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea jana ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi mkoani humo.
Akizungumza katika mkutano huo wakati akiomba kura Dr. John Pombe Magufuli aliwaambia wananchi hao kuwa anataka kuijenga Tanzania mpya yenye viwanda vikubwa, vya kati na vya chini ili kuboresha uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania na kuleta mabadiliko bora na siyo bora mabadiliko.
Alisema pia serikali yake itaongeza kasi ya ujenzi wa barabara , Zahanati na Hospitali , kuongeza mafao ya wafanyakazi wa sekta mbalimbali ili kuongeza tija ya kazi , wanafunzi kusoma bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne nk.
Alisema ataongeza zaidi kasi yake katika utendaji tofauti na alipokuwa Waziri wa ujenzi kwani hapo awali alikuwa akiagizwa kama waziri na sasa akichaguliwa na watanzania kuwa rais yeye ndiye atakayeagiza na ole wake waziri atakayemteua asitekeleze maagizo yake atakiona cha moto.
Dr John Pombe Magufuli pia alitembelea na kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kada maarufu wa CCM marehemu Kapten John Damiano Komba ambaye alifariki miezi kadhaa iliyopita jijini Dar es salaam katika hospitali ya jeshi Lugalo na kuzikwa nyumbani kwao huko Lituhi wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitoa heshima katika kaburi la Kada maarufu wa CCM Marehemu John Damiano Komba katika kaburi lake huko Lituhi mkoani Ruvuma kulia ni Mjumba wa Kamti kuu ya CCM Ndugu William Lukuvi.![]()

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Kapteni John Komba huko Lituhi mkoani Ruvuma.

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa kata ya Lituhi.![]()

Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika uwanja wa taifa mjini Mbinga katika mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Dr. John Pombe Magufuli.![]()

Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Mh William Lukuvi akiwapa salam za mikoa mingine ambako Dr. John Pombe Magufuli amepita.![]()

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Mbinga.![]()

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika Peramiho mkoani Ruvuma.![]()

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiingia kwenye uwanja wa Majimaji.![]()

Majimaji ikiwa imetapika

Mwigulu Nchemba akitema cheche kwenye uwanja wa majimaji
↧
LIVE UPDATE KUTOKA SERENA HOTEL AMBAKO DR. SLAA ANAONGEA
1.Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutujalia uzima.
2. Nimeamua kujitokeza leo hii ili kukomesha upotoshaji na kuuweka wazi ukweli.
3.Sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia ninachokiamini.
4.Sina ugomvi na kiongozi yeyote maana siasa sio uadui.
5. Siasa inapoongozwa kwa misingi ya upotoshaji, matokeo yake ni vurugu.
6. Naweka wazi kuwa mimi sikuwa likizo na hakuna mtu yoyote aliyenipa likizo.
7.Kilichotokea ni kuwa niliamua kuachana na siasa tangu tarehe 28.7.2015 saa sita usiku baada ya kutoridhishwa na kilichokuwa kinaendelea ndani ya chama changu.
8.Ni kweli nilishiriki kumleta Lowassa CHADEMA Lakini nilikuwa na misimamo yangu ambayo ilitufanya tusielewane.
9. Baada ya Lowassa kukatwa pale Dodoma, Gwajima ambaye ni mshenga wa Lowassa alinipigia simu kutaka kujua ninii cha kufanya.
10. Nilimpigia Mwenyekiti Mbowe kumjulisha na tukakubaliana kupanga muda wa kuwasikiliza.
11. Kabla ya kuanza kuwasikiliza, msimamo wangu ulikuwa ni kumtaka Lowassa kwanza atangaze kuhama chama, aweke wazi ni chama gani anaenda na ajisafishe juu ya tuhuma zake
12.Tangu akatwe jina, Lowassa hakutangaza kujitoa CCM na wala hakujisafisha na tuhuma zake, kitu kilichonifanya nitofautiane naye.
13. Niliwauliza wanachadema wenzangu kuwa Lowassa anakuja kama Mtaji au Mzigo?
14. Swala sio urais kama watu wanavyozusha, mimi nilikuwa nataka mgombea mwenye uwezo na sifa ambaye ataweza kuitoa CCM. Sikuwa na tamaa ya urais kama watu wanavyosema
15. Tangu Gwajima atupe taarifa za ujio wa Lowassa, Swali langu la Lowassa kuwa Mtaji au mzigo halikuwahi kujibiwa.
16. Nilitaka kujua ni mtaji gani lowassa atakuja nao na ni viongozi gan atakuja nao.
17. Nilijibiwa kuwa anakuja na wabunge 50 wa CCM, wenyeviti 22 wa mikoa na wenyeviti 80 wa wilaya.
18.Baada ya ahadi hiyo, nilitaka sasa nipewe majina ya hawa watu lakini mpaka tarehe 25 july sikupewa hayo majina
19. Wenzangu waliniambia kuwa tarehe 27 niitishe kikao cha dharura ila niligoma kwa sababu nilikuwa sijapewa haya majina
20. Ndani ya kikao hicho, tulianza kwa mabishano makali kati yangu na Mbowe, Lissu na Gwajima, viongozi wenzangu ni shahidi na mungu anajua. Msimamo wangu ulikuwa ni uleule kujua mchango wa Lowassa
21. Kikao kile kikavunjika, baadae tukaingia kamati kuu lakini bado msimamo wangu ulikuwa ni uleule. Baadae nikaandika barua ya kujiuzulu.
22.Profesa Safari aliichana ile barua.
23.Cha kusikitisha ni kuwa Kesho yake picha zikaanza kusambaa mtandaoni zikimuonyesha na lowassa japo viongozi wangu walizikana zile picha. Kibaya ni kuwa viongozi waliuficha ukweli
24. Kesho yake niliandika tena barua rasmi ya kujiuzulu.
25. Baada ya pale zikaanza propaganda za uongo zikimuhusisha hadi mke wangu eti kanizuia.
26. Naomba watanzania wajue kuwa mke wangu hakuwahi kunizuia kwa lolote, lkn hata angefanya hivyo sio mbaya maana hata yeye ni mwanaharakati mwenye uchungu na nchi hii.
27. Mke wangu aliwahi hadi kuumia wakati akipigania ukombozi wa nchi hii.....Lakini sio mbaya, familia yangu imezoea propaganda.
28. Kikubwa katika harakati ni credibility ambayo lazima uilinde na mimi sitaki jina langu liharibiwe na ni haki yangu.
29. Maslah mapana ya taifa ndiyo yaliyotufikisha hapa na sio maslahi binafsi.
30.Lowassa na wapambe wake ni waongo maana hakuna hata kipengele kimoja walichokitekeleza.
31. Tulitaka hao wabunge 50 waje kwanza kabla ya mchakato wa uteuzi ccm
32. Napinga kuchukua makapi ya CCM na kuyaita MTAJI.
33.Mtu kama Sumaye ni FISADI na nilikuwa siongei naye
34. Sumaye aliwahi kusema CCM wakimchagua Lowassa atahama chama. Leo Lowassa kawaje msafi??
35. Tulitaka Mtaji toka kwa Lowassa na sio MAKAPI
36. Wenyeviti walioletwa na Lowassa ni MIZIGO na namjua vizuri. Akithubutu kunijibu ntamwaga UOZO wake wote
37.Nani asiyejua Guninita pia ni mzigo??
38: Nawataka viongozi wangu wanijibu ni mtaji upi walioupata toka kwa Lowassa.
39. Mimi ni Padri Mstaafu, sipendi siasa za uongo.
39. Ukisema unataka kuiondoa CCM ni lazima ujikumbushe misingi ya CHADEMA ambayo ilikuwa ni uadilifu. Leo chadema hii ina Uadilifu gani??
40. Namshangaa sana Lowassa eti kusimama mbele ya watu akijinasibu kuwa ni msafi.....kwamba mwenye ushahidi aende Mahakamani. Ni dhambi kupotosha watu.
41. CCM hawana ujasiri, ni waoga na ndiyo maana wamewalea watu kama akina Lowassa
42. Ukitoa kinyesi chooni na kukipeleka Chumbani maana yake hata chumba chako ni CHOO na kitakuwa kinanuka zaidi kuliko choo cha kawaida
43.Mimi nilikuwepo wakati sakata la Richmond likijadiliwa.Mimi nina ugomvi wa muda mrefu na Lowassa.
44. Mwaka 2010 mimi nilimtaka Lowassa atangaze Richmond ni ya nani.
45. Leo tena namtaka Lowassa Lowassa atoke hadharani atangaze Richmond ni ya nani. Unaposema ni ya mkubwa, atuambie mkubwa gani
46. Ukitaka kuijua Richmond rejea Ripoti ya Mwakyembe. Nampongeza Mwakyembe na Sitta kujitokeza hadharan kuusema ukweli.
47. Siku moja kabla ya ripoti kusomwa, nililetewa Rushwa ya milioni 500 ili tukaupindishe ukweli bungeni lakini nilikataa
48. Ripoti ya mwakyembe iliamua mambo mawili, moja; Lowassa ajipime au bunge lijadili na lichukue hatua. Lowassa kuona hivyo akaamua kukimbilia kujiuzulu kukwepa aibu ya kung'olewa na bunge
49: Lowassa haaminiki, ni muongo na hastahili kuwa Rais wa nchi....
50. Lowassa ni FISADI na kama mimi ni muongo ajitokeze hadharani akanushe
51. Anasema Lowassa ataleta maji, mbona jimbo lake la Monduli halina Maji???
52. Mnasema Lowassa kaanzisha shule za kata, iv mjua msingi wa shule za kata? waandishi rudini shule mkajifunze upya.
53.Nilifanikiwa kuijenga Chadema na ikawa tumaini jipya la watanzania.....Vijana wangu wa Chadema, naomba niwe mkweli propaganda imekivamia chama.
54. Inasikitisha kuona CHADEMA inajazwa kwa mabasi pale jangwani .....alafu mnawadanganya watu eti ni MAFURIKO
55. CHADEMA ya kipindi changu ilikuwa inakemea Rushwa. Niambien leo chadema watasema nini kwenye majukwaa?
56. Mnaomtetea Lowassa na nyie jitokezen hadharani...mimi nasema kwa sababu nina ushahidi na sio lazima ushahidi huu niupeleke mahakamani.
57. Wenye uwezo wa kumpeleka Lowassa Mahakamani ni Serikali, na mwakyembe alisema juzi kuwa kesi ya jinai haina kikomo, mtu anaweza kushitakiwa muda wowote
58. Sitaki kuingila swala la Babu Seya, lakini waliolawitiwa ni watoto waliokuwa chini ya umri. kwa nini haki yao ipotee?
59. Rais hana mamlaka ya kumtoa Babu Seya. Lowassa asiwadanganye.
60. Kuhusu swala la Masheikh, Sumaye ndiye aliyeamuru mapolisi wavamie misikiti wakiwa na mbwa......Watanzania msikubali kudanganywa. hizo ni propaganda za wasaka urais
61. Masikubali Rais Muongo na mimi naapa ntapiga kelele kila kona kumpinga Lowassa.
62.Lowassa alipokuwa waziri mkuu, matatizo yanayotokea leo hayakuwepo? mapigano ya wakulima na wafugaji hayakuwepo?
63. Lowassa akiwa waziri mkuu alisababisha migogoro mizito sana kati ya monduli na karatu. Rais wa aina hii wa nini?
64. Naomba nisiongee mengi kwa sababu ntakosa ya kusema siku nyingine.....Nawataka Lowassa na Sumaye wajitokeze kunijibu.
65. Siku nyingine ntakuja kuongelea kuhusu hisa za Lowassa kwenye makampuni
66. Nahitimisha kwa kusema kuwa Nimestaafu siasa na sina chama lakini nina nchi, hivyo ntaendelea kuwatumikia watanzania kwa jinsi mungu alivyonipa vipawa
67. Narudia tena, Sina chama na sitajiunga na chama chochote.
Waandishi wanauliza Maswali:
Mwandishi: Umesema hujiungi na chama chochote, utawasaidiaje watanzania? Rais gani unamuunga mkono?
Mwandishi Guardian: Ulisema Lowassa atakuwa assert kama atakuja na wabunge na hao wenyeviti. Je angekuja kama assert ungeyasema haya yote?
Mwandishi binafsi: Umesema waliohamia Chadema ni makapi. Mwaka 1995 Uliihama CCM, ukahamia chadema. Je na wewe ni KAPI?
Mwandishi-Azam: Umetangaza kustaafu siasa, lakini bado unakadi ya CCM na CHADEMA? Je utazirudisha?
Mwandishi Blog: Inaonekana baada ya chedema kukutosa ndo maana unamshambulia Lowassa, je ni kweli?
Majibu:
1. Kadi ni mali zangu na siwezi kuzirudisha. Ya chadema nimeilipia miaka 20,ya CCM bado haijaisha muda wake.
2. Kuhusu urais, mimi sijagombea urais na sikuchukua fomu. sasa kwa nini nikasirike kisa wamempa Lowassa?
Sina ugomvi na Mbowe na nakumbuka alinisaidia nyumba
3. Mimi sio KAPI....Ili kuujua ukweli unahitaji kutumia kigezo. KAPI ni yule aliyekataliwa na chama flani, mimi sikuwahi kukataliwa. Sikuwa na uchafu wowote wakati naingia CCM.
4. Lowassa ni mzigo tu hata kama angetuletea hao watu wake.....Lowassa ana makandokando mengi. Angetuletea hao watu ndo tungeamua tumpokee au tusimpokee
5.Mimi sina chama na sitampigia kampeni mtu yeyote. Mimi nimefanya utafiti kwa Lowassa pekee, kwamba taifa litapata madhara gan Lowassa akiwa Rais.....Lowassa ni Fisadi.
-Kazi yangu leo ilikuwa ni kuwaambia watanzania waachanane na ushabiki.Ukihamishia CHOO chumbani, manake harufu itahamia huko.
-Chadema ya leo kwa sasa imetekwa na Lowassa na hawawezi tena kuongelea Ufisadi
Maswali ya nyongeza
1.Umesema waliohamia chadema kwa sasa ni sawa na mfano wa Choo. Je, wewe ulipohama hukuwa choo? kwa nini wewe uliweza kukibadili chama halafu akina Lowassa washindwe?
Jibu: Wakati mimi nahama sikuwa mchafu kama hawa akina Lowassa na Sumaye.
↧
↧
SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO KUANZA KUTUMIKA LEO
Serikali imewatoa hofu wananchi kuhusu Sheria ya Makosa ya Mtandao inayoanza kutumika rasmi leo kuwa haijatungwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu, bali kwa maslahi mapana ya taifa na kuleta maendeleo ya nchi, kujenga uchumi imara na kupambana na wahalifu.
Aidha, serikali imewasisitizia wananchi kutumia vizuri mitandao kwa faida yao na taifa na kujiepusha na mambo ambayo yanakatazwa na sheria hiyo ili kutoingia matatani.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kuanza rasmi kutumika kwa sheria hiyo na ya miamala ya kielektroniki.
“Serikali imejiridhisha baada ya kufanya maandalizi yote muhimu ikiwamo kutoa elimu kwa umma na kujenga uelewa kwa watekeleza wa sheria hizi. Sasa sheria hizi zitaanza kutumika rasmi Septemba 1 (leo),” alisema Prof. Mbarawa.
Alisema sheria hiyo itasaidia kupambana na uhalifu kwenye mtandao kutokana na watu wengi kutumia vibaya mtandao na kuwalaghai watu kutuma fedha ama kuiba katika mabenki.
Alisema kwa mujibu wa sheria hiyo, watu wanaosambaza meseji za uchochezi ama za uongo kwa watu wengine ni kosa la kisheria na kufanya hivyo watakumbana na adhabu kali.
Alisema mtumiwaji wa meseji za aina hiyo akifuta pasipo kusambaza kwa watu wengine sheria hiyo haitamwadhibu wala kumhusu.
“Sehemu ya kifungu cha sheria ya makosa ya mtandao, kifungu cha 16 kinaeleza: mtu atakayechapisha taarifa au data katika picha, maandishi, alama au katika namna nyingine yoyote katika mfumo wa kompyuta, huku akijua kwamba taarifa au data hizo ni za uongo, zinapotosha, zisizo sahihi, na kwa lengo la kudhalilisha, kutishia, kuudhi au kwa njia nyingine au kudanganya umma au kuchochea utendaji wa kosa, atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua Sh. milioni tano au kutumika kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja,” alisema.
Prof. Mbarawa alitoa wito kwa wananchi wazingatie matumizi salama na sahihi ya huduma za mawasiliano na mitandao kwa manufaa ya kila mtu na kwa maendeleo ya taifa na kuepuka matumizi yasiyo sahihi.
Baadhi ya makosa ambayo yanaweza kukufanya ushtakiwe
Kuweka mtandaoni picha za kingono za watoto
Kuweka mtandaoni picha za ngono au za utupu
Kuweka taarifa za uongo mtandaoni
Kuweka taarifa za uchochezi mtandaoni
Kutukana au kumdhalilisha mtu
Kuweka mtandaoni tetesi zisizothibitishwa
Kutukana au kumdhalilisha mtu kwa misingi ya udini/ukabila.
↧
PICHA 3 ZA MKUTANO WA LOWASSA RUVUMA NI NOUMA...JIONE MWENYEWE
↧
MAGUFULI AMESEMA ENDAPO ATACHAGULIWA ATASHUSHA BEI YA VIFAA VYA UJENZI
Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli amesema endapo atachaguliwa, atashusha bei ya vifaa vya ujenzi vikiwamo saruji na mabati kuanzia mwakani akisema tayari kuna viwanda vikubwa ambavyo vimeshaanza kujengwa nchini.
Akiwahutubia wananchi wa Namtumbo, Ruvuma jana, Dk Magufuli alisema kuongezeka kwa viwanda hivyo akitolea mfano wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote ambacho kitakuwa kikubwa zaidi Afrika Mashariki na kuimarika kwa Barabara ya Songea – Masasi ambayo makandarasi wapo kazini, kutasaidia kuvutia wawekezaji na kusisimua biashara katika mikoa ya Kusini.
Akiwa Tunduru, Dk Magufuli aliahidi kuendeleza uchimbaji wa madini ya urani ili yaweze kuchochea maendeleo nchini.
Akiwahutubia wakazi wa Namtumbo wilayani Tunduru, Dk Magufuli alisema anafahamu bayana kuwa eneo hilo lina madini hayo hivyo akiingia madarakani, Serikali yake itaendeleza urani ili kuwasaidia kukuza uchumi wa wananchi hao.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa CCM mjini hapa, mgombea huyo alisema iwapo atapatiwa ridhaa hiyo Oktoba 25, ataimarisha uhusiano mzuri na nchi zote jirani na wafadhili wa maendeleo.
“Tutaendelea kuuenzi uhusiano mzuri na majirani zetu wanaotuzunguka wa Kenya, Malawi, Zambia, Msumbiji, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hadi Sudan Kusini. Pia, kuimarisha uhusiano na nchi nyingine za Afrika na mabara mengine na wafadhili wetu ambao wanatuamini sana na kutusaidia,” alisema Dk Magufuli.
Alisema wafadhili wengi wanachangia katika miradi ya maendeleo ya barabara kwa sababu wanaiamini Serikali na kuwa fedha hazitaliwa na mafisadi.
Alitokea mifano ya Barabara za Namtumbo – Tunduru-Mtambaswala zinazojengwa kwa ushirika na Shirika la Maendeleo la Japan (Jica) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kuwa ni matokeo ya uaminifu katika matumizi ya fedha za miradi.
“Wafadhili wanamwamini Magufuli kwa kuwa fedha zikitolewa hazichukuliwi. Hivyo msilete mtu ambaye haaminiki hata kwa wafadhili, akipatiwa fedha anakula, halafu akachukiwa na wafadhili baadaye wakasusia kutoa fedha za kumalizia miradi ya barabara tuliyoianza,”alisema.
Msafara wasimamishwa
Msafara wa mgombea huyo ulilazimika kusimamia mara nyingi baada ya wananchi kukaa barabarani kumtaka ajibu kero zinazowakabili, nyingi zikiwa ni za maji, barabara, umeme na afya.
Tangu alipoanza safari Songea Mjini, Dk Magufuli alisimama kwenye maeneo yasiyopungua 12, safari hii akitumia dakika chache tofauti na alivyofanya katika safari ya Vwawa-Tunduma mkoani Mbeya.
Dk Magufuli alivuta hisia za wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi wa Barabara ya Matemanga-Liuli aliposimama katika Kijiji cha Huria wilayani Tunduru kusikiliza kero zao zikiwamo za mishahara na kumuomba aendeshe mtambo wa kusawazisha udongo barabarani.
Baada ya kuujaribu mtambo huo kwa takriban dakika tano, aliwahakikishia kuwa mkandarasi SRBG atawalipa malipo yao yote kwa kuwa Serikali imeshamlipa fedha zote za mradi.
Akiwa Matemanga, aliwaahidi wananchi kujenga kiwanda cha kuongeza thamani za korosho kwa kuwa utawala wake utakuwa ni wa viwanda.
Huku akitumia historia ya utendaji wake katika Wizara ya Ujenzi, Dk Magufuli aliahidi kuwa Barabara ya Namtumbo-Masasi itakamilika mwakani na kuwa kuna makandarasi wanane wanaoendelea na kazi za ujenzi.
Katika mkutano wake Mjini Tunduru, Dk Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti mtarajiwa wa CCM, aliwapokea makada wapya 16 waliodai kuitosa Chadema.
Kutokana na kusimama mara kwa mara njiani kuzungumza na wananchi, Dk Magufuli alilazimika kufanya mikutano mifupi zaidi mjini Masasi huku akiwaomba radhi wakazi wa mji huo kwa kuchelewa.
“Ninafahamu wananchi wa Masasi mna masikitiko makubwa ya mazao, korosho, stakabadhi ghalani, ninataka niwaahidi hili nitalighulikia,”aliuambia umati mkubwa wa wananchi katika Uwanja wa Boma na kuongeza:
“Waziri wangu nitakayemteua wa kilimo hili lazima alifanyie kazi.”
Aliwaahidi wakazi wa mji huo kuwa atajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Masasi hadi Mtwara kupitia Newala yenye urefu wa kilomita 200.
Alisema tayari upembuzi yakinifu na usanifu wa barabara hiyo vimeshafanyika na kilichobaki ni kuanza tu kujengwa kwa kuwa tenda ilishatangazwa.
Alisema kujengwa kwa barabara hiyo na nyinginezo kuiwezesha Tanzania kuwa ya kisasa.
Aliendelea kutoa ahadi ikiwamo ya mikopo ya Sh50 milioni kwa vikundi vya vijana na wanawake katika kila kijiji, kujenga reli ya kisasa ya Mtwara-Mbamba Bay na kuwasomesha bure, watoto kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
Kutokana na ufupi wa muda, Dk Magufuli aliahidi kurejea Masasi endapo atachaguliwa ili kufanyia kazi masuala mbalimbali yakiwamo ya maji na mengineyo.
“Ni bahati mbaya ndugu zangu nimefika jioni nisameheni sana nitakuja tena na Mungu awabariki sana,” alimaliza kwa salamu ya Masasi “hoyee”, “Masasi kucheleeee.”
↧
LOWASSA: UJINGA, UMASIKINI NA MARADHI VITAKUWA HISTORIA KWENYE SERIKALI YANGU
Mgombea urais wa Chadema kwa mwamvuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amesema akiwa rais wa Awamu ya Tano atafuta maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umasikini waliodumu tangu nchi ipate uhuru mwaka 1961.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Lembuka katika Kijiji cha Madaba mkoani Ruvuma, Lowassa aliyekuwa akitumia staili ya kuwauliza wananchi matatizo yanayowakibili na kisha kuwajibu atakavyoyatatua, alisema tangu nchi ipate uhuru maisha ya Watanzania ni duni na kuahidi kuwaondoa katika umasikini.
Wakati Lowassa akisema hayo, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye aliwataka wananchi kuipa Chadema na Ukawa miaka mitano tu ili iweze kuwaletea maedeleo na kama wakishindwa, warudi tena CCM.
“Jambo kubwa ni kupiga kura na kuzilinda na ikiwezekana akina mama mpike chakula kabisa nyumbani ili waume zenu wakifika nyumbani wajipakulie wenyewe. Tusipoitoa CCM madarakani hatutaweza kuwatoa tena na lazima wang’oke safari hii. Hata wana-CCM wenzangu nawashauri waondoke huko na kujiunga na sisi. Ondokeni huko nyumba inawaka moto,” alisema Lowassa.
Katika mkutano huo, wananchi walieleza kuwa wanakabiliwa na ukosefu wa maji na umeme, migogoro ya ardhi, ada na michango iliyokithiri katika shule pamoja na ushuru katika mazao.
“Tutamaliza tatizo la umeme ndani ya mwaka mmoja, tutamaliza suala la kuporwa ardhi,” alisema Lowassa huku akiwahoji wananchi wa kijiji hicho kwanini wakubali kuporwa ardhi.
Wananchi hao walisema katika vituo vya afya wagonjwa wanaruhusiwa kurudi majumbani kutokana na vituo hivyo kukosa maji sambamba na kutozwa ushuru wa mazao usiokuwa na kichwa wala miguu.
Akizungumza katika mkutaano huo, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye alisema maendeleo ya Tanzania hayafanani na rasilimali zilizopo nchini, akiwataka wananchi kuyakubali mabadiliko ili kuepuka matatizo mengine.
“Nilikuwa waziri mkuu kwa miaka 10 lakini nchi haikuwa na vita. Mkichagua upinzani kutakuwa na amani kama kawaida,” alisema Sumaye huku akitolea mfano yaliyotokea Masasi ambapo wananchi walichoma moto vituo vya polisi na Halmashauri baada ya bodaboda kugongana na gari la polisi.
“Hali hiyo inatokana na wananchi kuchoka kuona viongozi waliowachagua wananeema na wao wanaendelea kuwa masikini.”
↧
↧
MAASKOFU WAMJIBU DR. SLAA BAADA YA KUWATUHUMU KUHONGWA NA LOWASSA......GWAJIMA NAYE AMPA MAKAVU, ASEMA SLAA AMETUMWA NA CCM
Baadhi ya viongozi wa dini na wananchi wamesema shutuma za aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa kuwa baadhi yao walihongwa na Mgombea Urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa, ni upuuzi mtupu.
Wamemtaka atoe ushahidi wa madai hayo kwa kutaja majina ya viongozi na kiasi walichohongwa, wakisisitiza kuwa hizo ni siasa za majitaka na kwamba anaifanyia kazi CCM ili apate njia ya kurudi katika chama hicho.
Rais wa TEC azungumza
Akizungumzia shutuma hizo, Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, amemtaka Dk. Slaa kutoa ushahidi wa madai yake kuwa maaskofu wa kanisa hilo wamehongwa na Edward Lowassa.
“Hizo taarifa ndiyo nazisikia kwako, lakini kama kweli amesema hivyo kwa nini hakuweka ushahidi kuanzia majina ya maaskofu hao waliopewa fedha, kiasi na zilikopokelewa. Lakini kwa upande wangu binafsi sijapokea kiasi chochote kutoka kwa mtu yeyote." Amsema askofu huyo
Askofu Niwemugizi alimtaka Dk. Slaa kutoa uthibitisho wa maaskofu wa kanisa hilo kupokea fedha kutoka kwa Lowassa waweze kutoa uamuzi.
“Lowassa nimewahi kukutana naye nilimwalika kwenye shule yangu ya seminari kule Biharamulo… shule yenyewe inaitwa Katoke na nilimuweka wazi sababu za kumwalika na sikupokea kiasi chochote cha fedha kutoka kwake,”alisema askofu huyo na kuongeza:
“Athibitishe hilo aonyeshe kiasi cha fedha na majina ya maaskofu, mimi sijapata kiasi chochote labda kama nimetupiwa kwenye akaunti yangu bila mimi kujua lakini nasisitiza atoe ushahidi.”
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekosti, William Mwamalanga alisema kauli za Dk. Slaa zina dalili ya kuleta kisasi fulani.
“Angekuja mapema kabla ya taratibu hizi kuanza tungemwelewa lakini kwa sasa yupo nyuma ya wakati. Kwanza ameonekana amesukumwa afanye aliyofanya na hilo haliwezi kuwabadilisha Watanzania walioamua kutaka mabadiliko,”alisema na kuongeza:
“Hotuba yake haina mashiko na taifa halihitaji watu wabinafsi,”alisema Mchungaji Mwamalanga.
Askofu Gwajima azungumza
Naye Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekana kuwa mshenga wa Edward Lowassa kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendelea (Chadema) .
Pia amekana kuhusika kuwarubuni kwa fedha maaskofu 30 wa Kanisa Katoliki ambao wanadaiwa kumuunga mkono Lowassa katika mbio zake za urais baada ya kuhongwa fedha.
Askofu Gwajima amesema Dk. Slaa ndiyo risasi ya mwisho iliyokuwa imebakia ndani kati ya bunduki ya CCM ili kuwaokoa.
Amesema yote yaliyosemwa na Dk. Slaa ni tuhuma za uongo hivyo wananchi wazipuuze kwa kuwa mwanasiasa huyo anatafuta uungwaji mkono kwa wananchi aelekee CCM.
“Yaani ni uongo kabisa tena uongo mweupe, imedhihirisha wazi kuwa huyu mtu asingefaa kuwa rais. Ni dhahiri ameona akiwasema wanasiasa wenzake watamjibu kwenye majukwaa yao ya siasa, lakini sasa amewasema maaskofu kwa kuwa wao hawana majukwaa.
“Kwa hiyo namshauri hayo mambo ya kuwahusisha maaskofu na uchaguzi aache uongo wa namna hiyo. Nafikiri awaseme wanasiasa wenzake kuzungumzia mambo ya siasa ila kuwahusisha maaskofu si mambo ya busara,” alisema.
Akizungumzia suala la kuwa mshenga wa Lowassa na Chadema, Askofu huyo amesema anafikiri Dk. Slaa ametumwa na waliomtuma, hivyo anawafanyia kazi watu.
“Kwa kawaida inashangaza kwamba kama watu wawili wanagombana, inatakiwa awepo mtu wa kuwaunganisha, ila anaposema maaskofu 34 haileti maana, haiingii akilini… ameingiza Gwajima, Rostam (Aziz) na maaskofu, haeleweki anachozungumza. Lakini ninachosema kuna waliomtuma ni watu ambao anawafanyia kazi.
“Kikubwa ni kwamba baada ya Lowasaa kuchaguliwa kugombea urais kwa Chadema alichukia, alifikiri Lowassa hataendelea kuwa na umaarufu, sasa anaona Lowassa anakwenda, hiyo imemtia hasira anataka kumchafulia Lowassa, ndiyo maana anaongelea Lowassa Lowassa tu.
“Kwa mfano alisema Lowasa angekuja na wabunge wenyeviti wa CCM, ina maana angemkubali Lowassa aje nao, sasa angekuja nao asingekuwa fisadi? Ni swali zuri ila amekwepa kulijibu.
“Nafikiri Dk. Slaa ndiyo risasi ya mwisho iliyobakia ndani ya bunduki ya CCM. Natoa wito kwa waumini wangu wafahamu kuwa hizi tuhuma ni za uongo na namsihi huyo daktari asihusishe maaskofu na uongo wake abaki nao mwenyewe,” alisema Askofu Gwajima.
↧
SERIKALI YALIKANA DENI LA WALIMU
Sakata la madeni ya walimu limezidi kuchukua sura mpya baada ya serikali kusema haidaiwi na kwamba imebaini kuwapo kwa majina hewa ya walimu zaidi 4,000 yaliyowasilishwa kwa ajili ya malipo.
Imesema imegundua hivyo baada ya kufanya uhakiki wa deni la Sh. bilioni 19.6 lililowasilishwa na walimu baada ya kuwalipa madai yao kwa mara ya mwisho mwaka 2013.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile, baada ya kuhakiki madeni hayo mwaka jana, serikali imegundua deni halisi inalodaiwa na walimu ni Sh bilioni 5.6 tu.
Alisema endapo serikali isingefanya uhakiki wa deni hilo na kulilipa ingeingia hasara ya Sh. bilioni 14.
Alisema katika uhakiki huo, wizara hiyo imebaini kulikuwa na deni hewa kubwa la mwalimu mmoja wa Halmashauri ya Tunduru Mkoani Lindi Sh. milioni 500 na kwamba baada ya kuhakiki imegundua deni lake halali ni Sh. 500,000 tu.
Dk. Likwelile alisema kwa madeni ya mwaka jana, serikali imelipa walimu Sh. bilioni 5.6 baada ya kufanya uhakiki.
“Katika uhakiki tumebaini kuwapo udanganyifu wa fedha kwa walimu kujiongezea huku wengine wakidai deni la aina moja mara nne,”alisema.
Dk. Likwelile alitaja sababu za serikali kukataa kulipa baadhi ya madai ya walimu yaliyowasilishwa ni pamoja na kukosa vibali au vielelezo, madai mengine kuwa yameshalipwa, mishahara iliyowasilishwa kama madai yasiyo ya mishahara, baadhi ya walimu kutotambuliwa na halmashauri, baadhi ya walimu kutokuwa na madai katika majalada na makosa ya ukokotoaji na uandishi.
↧
TUNDU LISSU: DR SLAA NI MUONGO WATANZAIA MPUUZENI.....KINACHOMSUMBUA NI TAMAA YA URAIS. TUNAMTAKA ARUDISHE MALI ZOTE ZA CHAMA
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, jana alitangaza rasmi kuachana na siasa baada ya kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa na hatimaye kumfanya mgombea urais wa chama hicho chini ya mwamvuli wa UKAWA.
Dr. Slaa alitoa uamuzi huo jana mbele ya waandishi wa habari ambapo pia mbali na kutangaza kuachana na siasa aliwatuhumu Lowassa na Sumaye kuwa ni MAFISADI wa kutupwa na kwamba hawastahili kupewa nchi .
Akijibu tuhuma za Dk. Slaa mwansheria wa CHADEMA Tundu Lissu amesema anashangaa kwamba Dr. Slaa anadai hakubaliani na uteuzi wa Lowassa kwa ajili ya kiti cha rais wakati yeye ndiye aliyepanga na kumleta Lowassa katika chama hicho.
Lissu amesema kinachomsumbua Slaa ni tamaa ya Urais maana CHADEMA walikuwa wamekwisha mteua kugombea urais tangu mwezi mwezi wa kwanza.
"Kamati kuu ilimteua kugombea urais kwa tiketi ya chadema tangu mwezi january na ilipofika mwezi April kamati ilimthibitisha tena kuwa yeye ndo mgombea wetu.
"Ilipofika mwezi wa tano, Dr. Slaa mwenyewe akaanzisha mazungumzo ya kumleta Lowassa Chadema.
"Amesema mshenga ni Gwajima,hajasema mposaji ni nani. Nani aliyemfuata Gwajima kumwambia tunamtaka Lowassa, ni Dr. Slaa mwenyewe.
"Yeye ndiye aliyemwambia Gwajima halafu ndo akamwambia Mwenyekiti wa chama kuwa Lowassa akikatwa tumchukue, na tumchukue kwa sababu ana nguvu kubwa na ataipasua CCM katikati.
"Mbowe alipoambiwa hivyo alikubali na Dr. Slaa ndiye aliyeunda timu ya majadiliano ya Chadema yenye wajumbe watatu ambao ni Benson Kigaila, John Mrema, Reginald Munishi.
"Walikaaa na kufanya mazungumzo ya kina na Dr. Slaa alishiriki kila hatua.Majadiliano hayo yalikamilika tarehe 22.7.2015 ambapo Slaa aliitisha kikao cha kamati kuu cha dharura chenye ajenda moja tu ya kumkaribisha Lowassa ili awe mgombea urais wa Chadema." Amesema Lissu
Kwa nini Dr. Slaa amewasaliti?
Tundu Lissu amesema kilichomfanya Dr. Slaa awageuke ni First Lady, kwa maana ya mke wake ambaye hakukubaliana na kitendo cha Slaa kumpisha Lowassa
Lissu amedai kuwa wakati Lowassa anapokelewa tarehe 27 July kwenye Kamati Kuu, Dr.Slaa hakulala nyumbani, aliporudi nyumbani mchumba wake alimtupia mabegi nje na DR. alilala kwenye gari.
"Aliporudi nyumbani, Slaa alitupiwa mabegi nje, akalaa kwenye gari. Kesho yake akaja na kusema anataka kujiuzulu." Amesema Lissu na kuongeza:
"Slaa anasema hana chama na hajihusishi na chama chochote, lakini cha ajabu ni kwamba mwezi huu amepokea mshahara wa katibu mkuu wa chama, bado anatembea na gari ya katibu mkuu wa chama.
"Japokuwa amekitukana chama, lakini bado anatembea na magari ya chama, nyumba anayokaa alinunuliwa na chama na inalindwa na walinzi wa chama.
".....Ajitokeze atuambie ni nani aliyemwandalia huu mkutano wa serena hoteli? hizo gharama zimelipwa na nani? na kwa nini ametamka leo?
"....Kwa kuwa Slaa amekitukana chama, litakuwa ni jambo la busara sana kama atarudisha mali zote za chama."
Akizungumzia tuhuma zilizotolewa na Dr.Slaa dhidi ya Lowasaa, Lissu amesema CHADEMA walimhoji Lowassa kuhusu sakata la Richmond na aliwaambia kuwa aliyeruhusu mkataba wa Richmond uendelee ni Rais Kikwete.
Nimeweka Audio ya Lissu Akiongea hapo chini.Bofya play umsikilize.
↧