Quantcast
Channel: DUNIA KIGANJANI BLOG | Ifanye Dunia Kuwa Yako
Viewing all 2674 articles
Browse latest View live

NEC YAONYA VYAMA VYA SIASA VITAKAVYOKIUKA RATIBA ZA KAMPENI

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, kuhakikisha vinafuata na kuheshimu ratiba ya uchaguzi waliyojiwekea.

Katika taarifa kwa njia ya video iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani amesema kuwa vyama vyote vilishiriki katika kuandaa ratiba hiyo na kuwa viliiridhia hivyo hawana budi kuhakikisha wanaifuata.

“Tulikaa na vyama, mimi sikuamua hii ratiba, wao walipendekeza na wakakubaliana na wakatoa ratiba hii, cha kwanza kabisa vyama vya siasa wazingatie waliyoyaweka humu,” alisema Kailima.

Aliongeza kuwa utaratibu huo upo kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Uchaguzi ya 2015 na kuwa wakikiuka, sheria itawakamata.

“Kwenye maadili (Sheria ya Maadili ya Uchaguzi 2015) kuna eneo ambalo vyama vya siasa na wagombea wanakubaliana kuzingatia muda wa kuanza kampeni na muda wa kumaliza kampeni,” alisema.

Aliongeza kwa chama au wanasiasa watakaokiuka wataitwa kwenye kamati ya maadili na kuhojiwa na wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Agizo hilo la NEC linakuja siku chache baada ya CCM kuzindua kampeni zao siku ya Jumapili katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam ambapo shughuli hiyo ya uzinduzi ilihitimishwa majira ya saa 12.34 jioni, ikiwa ni nusu saa zaidi ya muda unaotakiwa kisheria.



Mpekuzi blog

PITIA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 26,2015, KWA HABARI ZOTE ZA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

$
0
0
Pitia hapa headline mpya kwenye magazeti mbalimbali ya Udaku, Michezo na Hardnews. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele na nyuma za magazeti ya leo.







.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

KESHO HAPATOSHI JANGWANI!! RAIS WA UKAWA EDWARD LOWASSA KUWAHUTUBIA WATANZANIA

$
0
0
 
MRATIBU wa Maandalizi ya Kampeni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Deogratia Munishi amesema maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa kampeni yamekamilika kwa asilimia 90.


Akizungumza na waandishi wa habari leo katika viwanja hivyo vya Jangwani, Munishi amesema kila kitu kipo tayari katika maandalizi hayo na wanachosubiri ni mkutano.

Munishi amesema mkutano huo wa ufunguzi wa kampeni umepangwa kuanza saa 4 asubuhi na kumalizika saa 12 jioni.

Amesema, mkutano utahudhuliwa na watu kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwemo wanachama kutoka nje ya nchi kama Zambia na sehemu nyingine duniani.

Aidha, amewataja viongozi watakaohutubia katika mkutano huo kuwa, Mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji, viongozi wakuu wa UKAWA na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali.

Kuhusu uwepo wa wasanii katika mkutano huo amesema:
 
“Wasanii watakuwepo lakini hawatapamba mkutano kama kule kwa wenzetu, sisi tunakuja kutangaza sera na sio tamasha la wasanii.”

Naye Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene ametoa ratiba ya Mgombea urais na mgombea mwenza kuwa, mara baada ya uzinduzi wa kampeni hizo wataanza ziara mikoani.

Amesema Lowassa, Jumapili ataanza ziara yake Mkoani Iringa na kufanya mikutano ya hadhara minne ambapo ataanzia Mufindi, Kilolo, Karenga, na Iringa Mjini kila sehemu mkutano mmoja.

Kwa Upande wa Babu Duni, amesema ataanzia Mtwara katika wilaya ya Newala, Tandahimba, Mtwara vijijini na Mtwara mjini.

Aidha, kuhusu tetesi za uwepo wa Katibu mkuu Chadema, Dk. Willbrod Slaa viwanja vya jangwani Makene amesema: “Hizo ni tetesi tu. Hakuna ukweli wowote. Dk. Slaa (Willbrod) amepumzika acheni kumzushia maneno.”

Ameongeza, mkutano utakuwa laivu katika televisheni na radio zisizopungua tano kuanzia saa 9 hadi 12 jioni.

chanzo:Mwanahalisionline

ANGALIA HAPA MAJINA YA WAHITIMU WA KIDATO CHA 4 NA 6 2014 NA JKT 2015 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA

ANGALIA PICHA- NYUMBA ILIYOUNGUA NA MAHALI WALIPOZIKWA WATU 9 WA FAMILIA MOJA WALIOTEKETEA KWA MOTO DAR,UKAWA WAFIKA ENEO LA TUKIO

$
0
0



Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad na umoja wa UKAWA leo wamewatembelea na kuwapa pole ndugu wa marehemu waliofariki kwenye ajali ya moto hapo jana maeneo ya Buguruni Malapa.

Baba wa Familia iliyoteketea kwa moto (Masoud) amesema majina ya marehemu yalikuwa ni Samira Juma ambaye alikuwa mke wake. Ahmed Masoud, Aisha Masoud , Abilah masoud, Ashraf Masoud, hawa walikuwa watoto wake, mama yake mzazi, mfanyakazi wa ndani, na mwanamke aliyejukana kwa jina la Wadh hat akiwa na mtoto wake mdogo wa mwaka mmoja na nusu.

Baadhi ya picha zikionesha nyumba iliyoungua na sehemu waliyozikwa jana wale watu 9 wa familia moja wakiwemo watoto watano waliofariki kwa moto baada ya nyumba yao kuungua moto na wao kuungulia ndani eneo la Buguruni Malapa, Ilala jijini Dare es salaam.




UMEIPATA HII MPYA YA DAVID KAFULILA KUHUSU DR SLAA?? IKO HAPA

$
0
0

Mbunge wa Kigoma Kusini anaye maliza muda wake, David Kafulila amefunguka na kusema anaamini Katibu Mkuu wa chama cha Chadema Dk. Willibrod Slaa hawezi kuwasaliti watanzania wakati huu wa ukombozi wa pili.




Akichat Live kupitia ukurasa wa facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni, Kafulila amesema Dk. Slaa bado kampumzika na anaendelea kutafakari, ingawa kwa mtazamo wake anaamini hatawaangusha watanzania katika ukombozi huu wa pili.
"Dk. Slaa bado kapumzika, anaendelea kutafakari. Naamini hatawaangusha watanzania katika ukombozi huu wa pili. pengine tumpe muda tu, " alisisitiza Kafulila katika moja ya posti yake.



Katika hatua nyingine Kafulila amesema anamtazama Lowassa kama kiongozi jasiri na mwenye malengo na uwezo wa kusimamia masuala hivyo kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) anaweza kufanya mambo makubwa zaidi kuliko angepitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama alivyotaka kufanya awali.



Mbali na hilo Kafulila amesema baada ya Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba anaamini CCM itaunda kambi ya upinzani Bungeni kwa kuwa chama cha upinzani baada ya Ukawa kuchukua dola lakini pia anaamini kutakuwa na uwiano mzuri wa wabunge jambo ambalo kwa miaka mingi halikuwezekana.



"Bunge lijalo baada ya uchaguzi litakuwa bunge lenye uwiano mzuri wa wabunge wa chama tawala na watakaokuwa wapinzani, bila shaka CCM wataunda kambi rasmi ya upinzani," alisema Kafulila.



Jina la David Kafulila lilikuwa kubwa baada ya mbunge huyo kuibua bungeni kashfa ya akaunti ya Tegeta Ecsrow ambayo ilipelekea baadhi ya mawaziri kung'oka kwenye nyazifa zao na wengine kupelekwa katika tume ya maadili, lakini Mbunge huyo anayemaliza muda wake amesema baada ya kufichua uchafu huo wa serikali hana uhakika na usalama wake lakini amemkabidhi Mungu maisha yake.



"Baada ya kufichua skendo ya Escrow nilipata vitisho na nimendelea kupata vitisho, hakuna uhakika wa usalama na yote nimeshamkabidhi Mungu na nilikwenda kuhiji Israel mwaka jana," alisema Kafulila.



Kafulila alimaliza kwa kutoa maoni yake juu ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 25 na kusema kuwa utakuwa ni uchaguzi wa kihistoria kwa maana ya ukombozi wa awamu ya pili baada ya ule wa kumtoa mkoloni, na akakumbushia kauli ambayo baba wa taifa aliambiwa na wakoloni.

NI BALAA SANA!!! ANGALIA PICHA MHESHIMIWA LOWASSA ALIPOKUTANA NA WAJASIRIAMALI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mgombea urais wa vyama hivyo Mh Edward Lowassa na mgombea mwenza Mh Duni Haji wamekutana na makundi mbalimbali ya wajasiriamali na wanafunzi wa elimu ya juu ambao licha kutumia fursa hiyo kuelezea matatizo yanayowakabili wametoa mapendekezo yatayolenga kuwawezesha watanzania kunufaika na rasilimali zanchi yao.

Wawakilishi wa makundi hayo wamesema hatua ya kuviunganisha vyama vya siasa na kupatikana UKAWA imewapa matumaiani makubwa ya kuondokana na uonevu na umaskini mkubwa unaowakabili.

Akizungumza na makundi hayo Mh Lowassa na viongozi wengine wa UKAWA wamesema wamejipanga ipasavyo kuleta na kusimamia mabadiliko ya kweli yatakayotatua kero za wananchi na kuondoa uonevu uliokidhiri matatizo ambazo serikali ya ccm imeshindwa kuyapatia ufumbuzi kwa miaka yoyte 50 iliyokuwa madarakani.

Msanii Juma Nature A.k.a Kibla akiongoza wasanii wenzake kuwasalimia viongozi wa UKAWA leo Ijumaa 28/08/2015 ikiwa ni majumuisho ya ziara ya Mgombea Urais Mhe. Lowassa kwa jiji la Dar es salaam








Mhe. Edward Ngoyai Lowassa awasili katika viwanja vya Msimbazi Center



Mhe. Edward Lowassa akiwasili katika viwanja vya Msimbazi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuongea na wawakilishi wa vikundi mbalimbali kutoka Dar es salaam leo Ijumaa 28/08/2015


Mhe. Edward Lowassa akiwasili katika viwanja vya Msimbazi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuongea na wawakilishi wa vikundi mbalimbali kutoka Dar es salaam leo Ijumaa 28/08/2015



M/kiti wa CHADEMA Mhe. Mbowe akiwasili Msimbazi Centre kufanya mjumuisho wa ziara ya mgombea Urais Dar

Meza kuu kwenye mkutano

USIPIME!!! SHUHUDIA PICHA JINSI DKT MAGUFULI ALIVYOKINUKISHA MBEYA ,AAHIDI KUANZISHA MAHAKAMA YA MAFISADI NA WALA RUSHWA TANZANIA

$
0
0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jioni ya leo Agosti 28,2015,kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano.

 

Dkt Magufuli amesema kuwa serikali atakayoingoza atakapopata ridhaa ya kuingia Ikulu,itazifanya huduma za Afya kuwa bora na kuwabana wahudumu wa afya wenye tabia ya kuchukua dawa na kuziuza kwa watu binafsi.


Magufuli ambaye yupo katika mikoa ya Nyanda za juu kusini katika kampeni ya kusaka nafasi ya kuwa raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema suala la afya litakuwa moja ya ajenda zake muhimu atakapoingia madarakani.


Katika hatua nyingine Dkt Magufuli amewaleza wananchi kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuiongoza Tanzania,atahakikisha anaanzisha mahakama maalumu ya Mafisadi na Wala rushwa.


PICHA NA MICHUZI JR-MBEYA.

Mbunge wa zamani wa jimbo la Kyela Mzee John Mwakipesile akimpigia debe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli wakati mgombea huyo alipofika jimboni humo kuomba kura za wananchi ili wamchague kuwa rais.Mzee Mwakipesile amesema kuwa anamuunga mkono Dkt Magufuli na atahakikisha anashiriki kikamilifu kuhakikisha mgombea huyo anaibuka na ushindi kwa kishindo.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela Dkt Harrison Mwakyembe akimpigia debe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jionu ya leo.

Naibu Waziri wa Fedha Mh Mwigulu Nchemba akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya,ambapo Mwigulu aliwaomba wananchi hao waliojitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na hatimae aweze kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano kwa sababu ana sifa zoto za kuongoza nchi.

Maelfu ya Wananchi waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya Nzovwe Mbeya jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao.

Naibu Waziri wa Fedha Mh Mwigulu Nchemba akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya,ambapo Mwigulu aliwaomba wananchi hao waliojitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na hatimae aweze kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano kwa sababu ana sifa zoto za kuongoza nchi.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano,Magufuli amewaambia wananchi hao kuwa atahakikisha huduma za afya zinaimarishwa ipasavyo,katika suala la Elimu Magufu aliwaeleza Wananchi kuwa iwapo watamchagua katika nafasi hiyo ya Urais atahakikisha elimu kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne itatolewa bure,aidha pia amewataka Watanzania kuwa wamoja katika kuhakikisha wanailinda na kuitunza amani iliyopo nchini.


Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya.

Wafuasi na wapenzi wa chma cha CCM wakishangilia

Maelfu ya Wananchi waliokusanyika katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo.

Jicho la samaki katika ubora wake kwenye mkutano wa kampeni za CCM katika viwanja vya Nzonvwe mjini Mbeya.

Mmoja wafuasi wa chama cha chadema ambaye aliikabidhi kadi yake kwa Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli na kutanganza kuhamia chama cha CCM,katika mkutano wa kameni uliofanyika katika uwanja wa Tandale,Tukuyu mjini wilayani Rungwe

Baadhi ya Wananchama kadhaa wa Chadema wakiwa katika picha ya pamoja na Dkt Magufuli mara baada ya kutangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na ccm

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi waliokuwa wamefika katika uwanja wa Tandale mjini Tukuyu kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.

Baadhi ya wananchi wa mji wa Kiwila wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsikiliza na kumuona mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli aliyekuwa akipita kuelekea wilayani Kyela kwenye mkutano wa kampeni.


Heka heka za wafuasi wa CCM

Wananchi wa Kyela wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa John Mwakangale mjini Kyela,kwa ajili ya kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye mkutano wake wa kampeni mjini humo.

Dkt Magufulia akiwahutubia wananchi wa Kyela mjini Ipinda



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa jimbo la Kyela kwa wananchi wa mji wa Ipinda wilayani Kyela wakati alipofika katika mji huo kufanya mkutano wa kampeni, Dr. John Pombe Magufuli amewaomba wananchi wa Kyela kumpa kura za ndiyo Dr. Harrison Mwakyembe ili aweze kumtumia mara atakapochaguliwa na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania



Dkt Magufuli akiwapungia wananchi wa Tukuyu mjini alipowasili mjini humo kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni.

Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni

Mh.David Mwakyusa akimwombea kura mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wananchi ili apate ridhaa ya kuwatumikia wananchi akiwa Ikulu.

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tukuyu mjini kwenye kutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tandale mjini gumo jioni ya leo.

MSANII JUMA NATURE AKA KIBRA AIBUKIA KWA LOWASSA,UKAWA MWENDO MDUNDO

$
0
0



Msanii Juma Nature A.k.a Kibra akiongoza wasanii wenzake kuwasalimia viongozi wa UKAWA leo Ijumaa 28/08/2015 ikiwa ni majumuisho ya ziara ya Mgombea Urais Mhe. Lowassa kwa jiji la Dar es salaam

USIPITWE NA KILICHOANDIKWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMAMOSI,AGOSTI 29,2015- YAKO HAPA YA UDAKU,MICHEZO NA HARD NEWS

MWAKYEMBE AMSHAMBULIA LOWASSA KUHUSU RICHMOND,MWIGULU NAYE ADAI LOWASSA NI MPIGA- DILI TANGU AKIWA KIJANA

$
0
0

Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati teule ya bunge ya kuchunguza kashfa ya mkataba tata wa Richmond iliyomuondoa madarakani aliyekuwa waziri mkuu Mh Edward Lowassa, Mh Harrison Mwakyembe amewahakikishia watanzania kuwa walijiridhisha pasipo shaka kuhusika kwa Edward Lowassa katika sakata la Richmond na kwamba hawakumsingizia kama anavyojitetea hivi sasa.



Mwakyembe aliyasema hayo mbele ya maelfu waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli katika viwanja vya Luandanzovwe jijini Mbeya, jana.

Akizungumzia madai ya kwa nini baadhi ya wahusika hawakupelekwa mahakamani kama kuna ushahidi, mhadhiri huyo wa sheria alisema kosa la jinai, halina ukomo na wakati wowote linaweza kufunguliwa mashitaka, huku akiapa kuwa anaweza kumfungulia mtu mashitaka hata kesho.

Alionya viongozi na makada wa Chadema na vyama vinavyowaunga mkono katika umoja wa Ukawa wanaozindua kampeni zao leo jijini Dar es Salaam, kwamba wasithubutu kujibu hoja zake.

Dk Mwakyembe alisema ikilazimika kusema ukweli, ataweka hadharani uchafu wote uliofanyika, ambao alisema bungeni kuwa asingeuanika na kuifanya Richmond hoja ya kila siku mpaka Watanzania waelewe kilichofanyika.

“Tunao ushahidi. Hawa walitakiwa kuwa jela badala ya kuimba nyimbo za ajabu,” alisema Dk Mwakyembe katika mkutano huo uliorushwa moja kwa moja nchi nzima na kuongeza kuwa Dk Magufuli akiingia madarakani, anakwenda kuanzisha Mahakama ya Ufisadi.

Alisema yeye na wenzake walipewa kazi ya Bunge kuchunguza ilikuwaje viongozi waandamizi wakaamua kuipa kampuni hewa zabuni ya mabilioni ya fedha, ambayo imesababisha mpaka leo kuna shida ya umeme nchini.

Dk Mwakyembe alikumbusha kuwa walikwenda mpaka Marekani kuchunguza uwepo wa kampuni hiyo iliyodaiwa kutoka katika nchi hiyo, na kukutana na kampuni ya kuchapisha kadi za harusi.

Kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, baada ya kubaini ubadhirifu huo, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alishinikizwa kujiuzulu na kumaliza suala hilo na hivyo hatua ya kiongozi huyo kutaka kwenda Ikulu, wazalendo hawawezi kuikubali.

“Hatutaruhusu watumie demokrasia kuingia Ikulu na hiyo ndiyo shida ya kuazima wagombea,” alisema Dk Mwakyembe akimaanisha kuwa chama cha Chadema, kimeazima mgombea bila kumfahamu.

Dk Mwakyembe alisema suala hilo lilishafungwa bungeni, lakini anashangaa kusikia linarejeshwa kinyemela.

Mwigulu

Naye Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba, alisema mgombea wa Ukawa, Lowassa, tangu akiwa kijana alikuwa ‘mpiga-dili’.

Kwa mujibu wa Mwigulu, Rais Kikwete alipoingia madarakani, alidhani kuwa Lowassa alikuwa ameonewa, akamteua kuwa Waziri Mkuu, lakini kabla ya kumaliza miaka miwili, akaendeleza tabia yake ya ‘kupigadili’.

Mwigulu alionya kuwa, Watanzania wakimpeleka ‘mpiga-dili’ Ikulu, shida yake na wenzake si changamoto za watu wa Mbeya wapate maji, huduma bora za afya na nyingine bora za umma, bali kurejesha fedha walizotumia wakati wa kutafuta urais.

“Mkimpeleka mpiga dili Ikulu, ‘wapiga-dili’ wenzake hawatalipa kodi, mtalipa nyie wanyonge ili wale ‘wapigadili’ warejeshe fedha zao,” alisema na kufafanua sababu za vyama vya Chadema, CUF, NCCRMageuzi na NLD kuungana pamoja katika Ukawa.

Kwa mujibu wa Mwigulu, kilichowaunganisha ni maslahi ya aina mbili; moja aliyetoa fedha kwa ajili ya kwenda Ikulu, ambaye anatafuta nafasi hiyo ili arejeshe madeni yake na wengine ni waliouza vyama ambao ‘wameshakunja’ chao.

“Nawaambia mwisho wa mbwembwe na maigizo, ni Oktoba 25 na baada ya hapo ni kazi tu,” alisema Mwigulu na kuhoji iweje Lowassa apande daladala leo, ambalo hakulipanda miaka 40 iliyopita?

Mwigulu alisema Watanzania wana siku 60 za kujadili hatima ya taifa lao na katika hilo, hakuna namna zaidi ya kuelezana ukweli mtupu.

Chanzo-Udakuspecially.com

LULU, MAMA KANUMBA WAPIGANA VIKUMBO

$
0
0
lulu mungu (3)
Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.

MAKUBWA! Mama wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa amejikuta kwenye simanzi nzito baada ya kukutana na mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye alikuwa mpenzi wa mwanaye kumpita bila kumsalimia.

Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar kulipokuwa na fainali za shindano la vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT 2015) ambapo Lulu alimpita mama huyo kama hawajuani kitendo ambacho kilisababisha minong’ono ukumbini hapo.
FrolaMtegoa“Inastaajabisha sana yaani huyu Lulu ndiyo kafikia hatua ya kumdharau mama Kanumba kiasi hiki, siyo siri hamtendei haki huyu mama sijui ni kitu gani kikubwa ambacho alimkosea,” alisikika mmoja wa mashabiki.
Mama Kanumba alipohojiwa na paparazi wetu ukumbini hapo, alisema anashindwa kumuelewa Lulu kwani hata ukiondoa undugu wake, bado kiumri ni mtoto anayepaswa kuheshimu wakubwa.

“Nimestaajabu sana kuona Lulu hanisalimii na isitoshe alijifanya kama hana habari na mimi utasema kuna kitu nimemkosea, wakati yeye ndiye anatakiwa ajishushe kutokana na yale yaliyotokea, ni dharau kubwa amenionyesha wakati aliwahi kuniomba msamaha huko nyuma kuhusu matukio yake hayahaya ya kuninunia,” alisema mama Kanumba.
Alipotafutwa Lulu, simu yake haikuwa hewani na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

MAFURIKO YA LOWASSA YAIPONZA TBC1, WAPEWA ADHABU NA TCRA KWA UBAGUZI HABARI ZA UKAWA,MAGIC FM NAO WAANGUKIA PUA

$
0
0


MAMLAKA ya mawasiliano nchini (TCRA) imekipa onyo kali kituo TBC1 kwa kosa la kubagua kusoma taarifa zinazohusiana na UKAWA.

Hukumu hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Walter Bugoya wakati wa mkutano na waandishi wa habari.



Bugoya alisema kamati hiyo imebaini TBC one imekiuka sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 pamoja na sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 kwa kufanya upendeleo wa vyama katika taarifa zake kwenye kipindi.

Alidai katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa tarehe 15 mwezi huu majira ya saa 12 asubuhi hadi saa tatu, katika kipingele cha uchambuzi wa magazeti mtangazaji wa kipindi hicho alikuwa anayasoma magazeti huku akiruka kusoma habari kuu husika.

Alisema Mtangazaji huyo alipokuwa anachambua gazeti la Majira na Nipashe alidanganya umma jambo ambalo amedai ni kosa.

Bugoya alitaja makosa hayo kuwa ni wakati mtangazaji huyo alipokuwa anasoma Gazati la Majira ukurasa wake wa mbele alisema habari kubwa ni “CCM yazidi kuwaumbua wanaomfuata lowassa” wakati habari kubwa ilikuwa inasomeka hapo ni ile inayosema “Mbeya kwafurika”, huku picha ya gazeti hilo likionyesha picha ya umati watu pamoja na mgombea wa Urais wa chadema Edward lowassa akihutubia.

Alisema mtangazaji huyo pia alifanya kosa lingine kama hilo pia wakati akisoma Gazeti la Nipashe ambapo alisema Habari iliyopewa uzito wa kipekee ni “Mbalawa atoa sheria ya mitandao” ambapo habari iliyopewa uzito ilikuwa ni ile “Mafuriko Mbeya” na sio aliyokuwa anaisoma yeye.

Alisema baada ya Kamati yake kubaini makosa hayo waliwasiliana na mkurugenzi wa TBC one Bwana Mshana.

Mkurugenzi huyo alitoa utetezi wake kwenye kamati hiyo akisema mtangazaji huyo hakufanya kosa kwakuwa alikuwa hajaridhika na taarifa zilizokuwa zimeandikwa kwenye magazeti hayo.

Sanjari na hayo Mshana alizidi kujitetea akidai kuwa hata mtangazaji huyo asingesoma habari ile lakini picha iliyokuwa inaonekana kwenye magazeti hayo tayari mtazamaji alikuwa ashajua kwahiyo amedai haikuwa na ulazima wa kusomwa.

Bugoya alisema baada ya kusikiliza upande wa TBC one ndio wakabaini kituo hicho kilikiuka sheria ya utangazaji ya Mwaka 2005 ambayo inavitaka vituo vyote vya utangazaji nchini kuripoti taarifa kwa kutokuwa na upendeleo wowote.

Alisema Kamati imefikia uamuzi wa kuipa onyo kali TBC one na endapo wataendelea basi Mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali zaidi.

NI ZAIDI YA TSUNAMI!! UKAWA WAWEKA HISTORIA DAR ES SALAAM,SHUHUDIA KILICHOJIRI LEO JANGWANI NI BALAA TUPU

$
0
0

Mafuriko ya Lowassa leo Dar








9:31 Mchana: Edward Lowassa akiwa na mgombea mwenza Haji Duni wanaingia kwenye viwanja vya Jangwani wakiwa kwenye gari la wazi.


9:43 Mchana: Lowassa amefika meza kuu na kuketi, meza kuu pia wamo Maalim Seif, Duni, Mbowe, Mbatia, Sumaye, Salum Mwalim na wengineo.


9:48 Mchana: Sasa ni muda wa viongozi wa dini kuomba dua, Said Riko kwa niaba ya dini ya Kiislam anaomba dua na atafata mchungaji Gwajima kwa upande wa dini ya kikristo kuongoza sala kwa niaba ya wakristo.


9:56 Mchana: Baada ya dua, kilichopo kwa sasa ni wimbo wa taifa


Salum Mwalimu(9:59): Tunakutana hapa kwa sababu ya mambo mawili, jambo la kwanza kuzindua rasmi kampeni zetu. Jambo la pili ni kuzindua ilani yetu ya uchaguzi mkuu, japokuwa inazinduliwa na CHADEMA inaungwa mkono na vyama vyote vilivyo kwenye UKAWA.


Imani yenu kamwe haitapotea bura, mnaiweka mahali sahihi na sisi tutaisimamia. Natangaza rasmi sasa mkutano wetu umezinduliwa na tusubiri nondo zenye hoja.


Lawrence Masha: Waheshimiwa viongozi, watanzania wenzangu, sisi sote ambao tumehama CCM tuna akili timimu, sio wapumbavu, sio makapi. Kutokana na mambo yaliyotutokea mimi na vijana, wale wote wanaofanya kazi katika serikali yetu, magereza, polisi mahakama kuu, niwapongeze wote waliofata maadili yao ya kazi lakini wapo wachache wasiofata maadili yao ya kazi. Mabadiliko yanakuja na ndugu zangu msiogope na tarehe 25 mpige kura tuingize serikali mpya ya UKAWA.


Mdee: Niseme mambo machache, kwa kipindi kirefu wanawake wa nchi tumekuwa wateja wa chama cha mapinduzi, kwa kipindi kirefu sana sisi ambao ni wahanga kwenye huduma za afya, tunaojifungulia chini.

2010 CCM waliahidi kununua bajaji kwa ajili ya wanawake wajawazito, Kikwete amejitengea bilioni 50 kwenda mamtoni, pesa hizo pekee zingetosha kununulia ambulance 300, wakati ni huu, imetosha. Tumalizie kwa kupiga kibwagizo.


Nimeambiwa niombe kura za Kawe, wanakawe mpoo, mtanipaa, asanteni sana


Mama Regina: Wakinamama mpo! Kwangu Mungu ametenda, mimi juzi nimeongea na wanawake wenzangu Tanzania nzima kupitia wanawake wa Dar, matatizo ya mwanamke nayafamu japokuwa sio yote.

Nachowaomba wanawake wenzangu tushirikiane, mabadiliko haya tutayaleta sisi kwa umoja wetu. Mungu awabariki sana.


Mbowe: Dar es Salaam Oyeee, DJ tafadhali naomba utupe utulivu. Kwa sababu ya muda nizungumze kwa kifupi sana, ukiona hicho kidude kinaruka juu ni mtambo wa kupigia picha. Kwa sababu ya muda niende kwenye tukio la kuzindua Ilani. Tunazindua ilani kama CHADEMA lakini ilani hii pia ni ilani ya CUF, NLD na NCCR.

Niwatambulishe wagombea wetu wa ubunge kwa Dar es Salaam. (Sasa ni tukio la kukabidhi ilani na nakala za ilani zinakabidhiwa Lowassa Lowassa, Duni na Hamad Sharif)


Sasa ni zoezi la kutambulisha wabunge watakaowania ubunge katika majimbo ya Dar es Salaam kasoro majimbo mawili ya Segerea na Kigamboni yana wagombea wawili wa UKAWA kila moja


Mbowe: Majimbo yote tunasema tunasimamisha mgombea mmoja, lakini majimbo mawili bado taratibu hazijakamilika lakini naamini yatakamilika


Wanaowania ubunge Dar es Salaam
Mtulia Said, Mwita Mwaitabe, Said Kubenea(Ubungo) Halima Mdee(Kawe) Julius Mtatiro(Segerea ushind Shaaban Nkumbi Kigamboni John Mnyika Kibamba Naotrapia (CHADEMA jimbo la Segerea) Kondo (Mbagala) na Asanali (Lofa wa Ilala)


Makaidi(NLD): Zamani mimi nilikuwa mwanamichezo mpiga mpira na mwenyekiti wa SImba kwa miaka mingi, Simba huu ndio mwaka wao na Yanga, mpira hauwezi kuwa mzuri kama siasa ni mbaya, tuhakikishe tunachague sera nzuri ya UKAWA, hivi haiwezekani kutengeneza picha yenye sura ya Lowassa, sura yake nzuri yenye nywele nyeupe.

Miaka 50 iliyoputa nilisema ipo siku TANU itapata jambajamba, mwaka huu TANU na CCM yake imepata jambajamba.


Taslima(CUF): Kinachosemwa hapa ni mabadiliko, tunatoka mahali pabaya, tunaingia mahali pazuri. Mabadiliko hayazuiliki isipokuwa waliodhani mabadiliko yanaweza kuletwa na CCM peke yake, hayo mawazo wayaondoe.


Mbatia(NCCR): Lowassa amesomea digrii ya pili Uingereza, degree ya maendeleo. Serikali atakayoiunda tutashirikiana kwa pamoja. Lowassa tunahakikishia umma wa watanzania utakulinda. Biblia inasema pasipo na kuni hakuna moto, pasipo na uchochezi hakuna vita.

Wao wanachochea vurugu, sisi tunaleta matumaini yenye heri kwa watanzania, matusi na uchochezi huo kuna maandiko kwenye bibilia yanasema heri kijana masikini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambae hasikii tena maonyo na Mtume amesema ukiona uovu kemea, ukiona huwezi basi weka chuki. (Anamalizi kwa kuimba wimbo)


Mbowe(CHADEMA): Asanteni sana Dar es Salaam, nitaongea kifupi sana kwa sababu ya muda, leo hii tunazindua rasmi kampeni za mgombea wa Urais, mgombea mwenza na wagombea wote wa UKAWA kwa nchi nzima.


Tunataka mabadiliko haya yakalete maisha mapya, nawashukuru sana viongozi viongozi wenzangu na zaidi waliopata ujasiri wa kuondoka CCM wakiongozwa na Lowassa, akafatiwa na mzee Sumaye na wengine ambao sitawataja kwa sababu ya muda.


Mzee Warioba umasikini sio sifa, wala sisi katika umoja wa UKAWA hatuutamani umasikini, wakati wa kuamini viongozi masikini hapana. Tunataka Tanzania iondoke katika umasikini kwa sababu umasikini ni laana.


Nimalizie kusema kwa nini Lowassa, sisi tulifanya tafiti, kwa sababu taifa letu limeendeshwa kwa propaganda kwa muda mrefu, Lowassa kwa muda wa miaka 10 amekuwa muhanga wa propaganda za CCM.

Nawashukuru sana Dar, niwaahidi tutafanya kampeni za kistaarabu, hataibiwa mtu simu, sadaka ya mabadiliko itafanywa katika kampeni nyingine. Nimkaribishe mheshimiwa Sumaye.


Sumaye: Kwa ajili ya muda nitasema kwa kifupi sana, nimetoka chama cha mapinduzi, katibu mkuu alisema sisi ambao hatukuteuliwa hatukuwa na maadili, mimi nasema kama kipimo cha maadili ni mheshimiwa Kinana, mimi nitakuwa mtakatifu, CCM wamekuwa wakiongoza siasa ya chama kimoja kwa ngozi ya vyama vingi, mmekunjika kwa miaka yote.

Tulitaka kufanya mabadiliko kulekule, kukawa na tatizo ndani ya CCM, ukitaka kufanya lolote wanakuzingira. Wanawajaza watanzania uoga wa usilolijua, mkiwapa wapinzani wataharibu nchi, kila binadamu ana uoga wa asilolijua.


Lowassa kwa kuliona hilo, kwa kuwa watanzania wanamfahamu aliona uoga wa aina hiyo haitakuwepo, na mimi nimekuja kwa sababu hiyo. Watanzania leo elimu yetu inashuka sana, tunashusha alama za kufaulu wanafunzi ionekane wamefaulu wengi, pia ukienda katika afya. Tunataka tubadilishe hali hiyo.


Leo Lowassa ametoka CCM ameonekana hafai, lakini ni KIkwete aliemfanya waziri mkuu wake, kuna Rais anaweka kiongozi ambae hafai? Lakini ni LOwassa huyuhuyu ndie aliemuingiza KIkwete Ikulu, Kwamba watanzania wanampenda Lowassa, halina mjadala.


Mmewasikia kwenye kampeni zao, fisadi mkubwa huyo amechukua fedha za matajiri, Lowassa amechukua ustaarabu wa kuwajibika. Waziri anachukua mzigo ili kumuokoa Rais na serikali yake. Asanteni sana.


Nyerere wakati anastaafu, kwenye kikao kimoja nafikiri cha halmashauri kuu. Alisema hajaona mtu mvumilivu kama Kawawa, alibeba mizigo aliyostahili kubeba yeye, ndiyo kazi aliyofanya Lowassa.

Vichwa vya treni vinavyonunuliwa, Lowassa alikuwepo? Wajenzi wa barabara nchi hii wanaidai serikali trilioni 1.4, kudai si tatizo katika hizo bilioni 900 ni pesa za adhabu, huo si ufisadi, mbona hawasemi? Serikali hii ni dhaifu sana na alituthibitishia katibu mkuu, mwenyewe kusema kuna mawaziri mizigo.


Mwisho wanalomsema nalo, Escrow Lowassa alikuwepo, kile kipande cha Lugemalira tulijua waliokula, kile kipande cha Habinder ni nani aliekula, tangu lini benki ikaruhusiwa kutoa cash kwa mabilioni. Wamejenga kibr, hawajali tena maumivu ya wananchi, naomba mwaka huu msikubali, watanzania mfurahie mabadiliko ya ndani ya vyama vingi.


Wanasema mgonjwa, mimi nataka niwaulize, kwani Magufuli mzima? Wanaenda kufanya nini Ulaya kama ni wazima, mtu yeyote ukishavuka miaka 50 hauwezi kuwa wazima kwa asilimia 100, hivi Rais mkapa alipokuwa madarakani hakwenda kufanyiwa operashi Ulaya, nchi ilidorora? Alienda akarudi akaikuta nchi usalama.


Kwani KIkwete alivyokuwa madarakani hakwenda kufanyiwa upasuaji mkubwa Markani??

Rais si kazi ya kubeba zege Ikulu, anatakiwa kuwake timu nzuri ya kazi, yeye ni meneja tu, naomba sana tumchague itakapofika tarehe 25 Oktoba. Asanteni sana, nawashukuru.

Maalim Seif(11:20): Kwa sababu ya muda mimi sitaki nizungumze leo, namkaribisha babu Duni ili azungumze na nyinyi

Duni(11:21): Na mimi kwa kuzingatia muda sina haja ya kusema sena, mimi natakiwa kumsaidia Lowassa atakapokuwa Ikulu. Katika mambo ambayo yametokea kwa miaka 50 ni watanzania kuonewa, Tanzania hakuna haki, tangu 95, wanaoonewa ni wapinzani tu, wanafunguliwa kesi za jabu ajabu, kunamajitu yanayoitwa mijanja weed, kuna majitu yanaitwa zombi, huku bara TV zinazuiliwa, mazikoni hatutakiwi, G/Mboto tabu.

Unapoonea watu wanajenga chuki, pamoja na kuambiwa Tanzania ina amani haina amani, wenye amani ni wanyonge kwa ajili ya stahamala zao, tumeonewa vya kutosha, sasa tunasema basi, tunataka mageuzi.

Nini tutafanya tukiwa IKulu, Hakuna kitu muhimu kama kuwa na katiba ya wananchi wote, miaka hamsini hatujawahi kuwa na katiba yenye ridhaa kwa pande mbili. Lazima tufanye kama Afrika kusini, tutaunda tume kama ya Afrika kusini, tume ya maridhiano tusameheane na tutafunga kitabu cha uhasama mabadiliko yatakapotoka.

Mdee amekuja kuzungumza matatizo ya kina mama, umma wote hapa huu umezaliwa na mwanamke, kitu muhimu tunachohitaji kufanya ni kuwaheshimu wakina mama. Sasa ni Lowassaaa.

Tambwe Hizza: Peoples, kwanza naomba mnisamehe, mwenzanu nilienda kuongeza ulofa kwenye kiwanda cha ulofa.

Watu wazito wameamua kukiacha chama cha mapinduzi, na mimi nimeamua na wapo wengi wameogopa eti watasema ana tamaa, hivi nani hana tamaa, hata Magufuli aliacha ualimu.

Napenda sana Lowassa na Sumaye, juzi nilimuona Rais akifanya utani na bosi wake, Kikwete akiwa waziri, Sumaye alikuwa waziri mkuu, eti anasema hajamuelewa, hivi ukishindwa kumuelewa bosi wako utaweza kuwaelewa watanzania.

Mwakyembe wakati akiwa mwenyekiti wa NBC, Mkapa alipotaka kuuza benki, Mwakyembe kwa mdomo wake alisema sikubali, leo anatumiwa kuja kumchafua mheshimiwa Lowassa.

Edward Lowassa(11:41): Peoples, Bwana Yesu asifiwe, tumsifie yesu Kristo, kuna tatizo kidogo muda umeenda wasije kupata sababu ya chama ipo kwenye maandishi, kwenye tovuti ya chama.

Niwashukuru waliopita kwa kunisemea, niliahidi kampeni safi lakini wameanza lakini wakianza ndio hivyo watavyopata. Kipengele cha kwanza elimu, cha pili elimu na cha tatu elimu.

Maneno haya nimeyaazima kwa waziri mkuu wa Uingereza. Cha kwanza elimu itakuwa gharama ya serikali kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu. Eneo la pili la kilimo ili tuweze kutengeneza ajira za kutosha.

Tatu tumeweka umuhimu sana kwenye afya iwe bora kwa akina mama na watoto wadogo. Wanokwenda nje ya nchi ni watu wakubwa, eneo jingine ni mawasiliano, ni muhimu sana tuwekeze.

Kwa hio jambo la kwanza nitakalofanya ni kujenga upya reli ya kati iende Kigoma na Mwanza. Tutafufua Air Tanzania, nisme mambo matatu ya mwisho.

Mashehe wa Zanzibar wako jela muda mrefu sasa, nasikia habari ya babu Seya, nimeisikia. Naelewa hisia zenu kuhusu babu Seya, Tutatumia utawala bora kuwatoa muda ukifika.

ANGALIA PICHA 41 ZA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM SHINYANGA,MHESHIMIWA SAMWEL SITTA,LUSINDE WAUNGURUMA

$
0
0


Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga mjini leo kimezindua rasmi kampeni zake za Uchaguzi mkuu ujao katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga,ambapo wabunge wa majimbo yote ya Shinyanga wamehudhuria uzinduzi huo .

Uzinduzi huo umeongozwa na waziri wa Uchukuzi mheshimiwa Samweli Sitta na mbunge wa Mtella aliyemaliza muda wake Livingstone Lusinde ambao walitumia fursa hiyo kumnadi mgombea urais wa CCM Dkt John Magufuli na kumponda mheshimiwa Edward Lowassa wakidai kuwa hafai kuwa rais kutokana ufisadi wake na kwamba Ukawa wamekurupuka kwani hawamjui vizuri Lowassa.

Makada hao wa CCM pia walisema Lowassa hana lolote zaidi ya mbwembwe na visingizio vya hapa na pale-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog 

Wanachama wa CCM na wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa CCM katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga leo 
Makada wa CCM wakiwa eneo la tukio 

Mjumbe wa NEC taifa Gasper Kileo akizungumza katika mkutano huo ambazo aliwataka wanaccm kuwapuuza watu wanaozusha kuwa atahamia Chadema/Ukawa kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni rafiki yake na Lowassa,ambapo Kileo alisisitiza kuwa hajawahi na wala hafikiria kuhama CCM na kwamba CCM lazima ishinde katika uchaguzi mkuu ujao 


Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za CCM wilaya ya Shinyanga mjini 

Mheshimiwa Samweli Sitta akizungumza katika mkutano huo,ambapo aliwatambulisha wagombea ubunge majimbo yote 6 ya uchaguzi mkoa wa Shinyanga ambayo ni Ushetu,Msalala,Kahama mjini,Kishapu,Shinyanga mjini,Kishapu na Solwa na kusisitiza kuwa lazima CCM ishinde katika majimbo hayo. 

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal akiwasalimia wakazi wa Shinyanga na kuwaomba wananchi kuchagua wagombea wa CCM kwani ndiyo watawaletea maendeleo 

Wanachama wa CCM wakifuatilia kilichokuwa kinajiri uwanjani 

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wananchi kuwapa kura wagombea wa CCM 

Mgombea ubunge jimbo la Msalala mheshimiwa Ezekiel Maige akiwasalimia wakazi wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga 
Mgombea ubunge jimbo jipya la Ushetu mheshimiwa Elius Kwandikwa akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo ajigamba kuwa katika jimbo lake wameshamaliza kufanya uchaguzi wanachosubiri ni utaratibu tu tarehe 25 Oktoba mwaka huu. 


Mgombea ubunge wa jimbo la Kishapu mheshimiwa Suleiman Nchambi akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wanaShinyanga kuwapa kura wagombea wa CCM kwani ndiyo watakaowaletea maendeleo watanzania 

Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wakazi wa Shinyanga kutochagua mbunge ambaye siyo mzawa wa Shinyanga na badala yake wampe yeye kura ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Shinyanga huku akijisifu kuwa amefanya mambo mengi ya kimaendeleo kwa wananchi katika sekta mbalimbali kama vile afya,elimu,michezo n.k 

Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wakazi wa Shinyanga leo 

Mheshimiwa Samweli Sitta akiwahutubia wakazi wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini ambapo alisisitiza kuwa mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa anahusika na sakata la Richmond na utajiri wake haueleweki 
Msanii wa nyimbo za asili Madebe Jinasa akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga mjini 

Wafuasi wa CCM na wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa CCM leo mjini Shinyanga 
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea

Mheshimiwa Livingstone Lusinde akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alitumia muda mwingi kumponda mgombea urais kupitia Ukawa Edward Lowassa hasa kuhusu afya yake kwamba ni mgonjwa bila kutaja ugonjwa anaougua/anaoumwa 

Wanachama wa CCM wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kwenye mkutano 

Mheshimiwa Livingstone Lusinde akizungumza mjini Shinyanga 

Wafuasi wa CCM wakiwa eneo la tukio 

Mheshimiwa Lusinde akiwaombea kura wagombea wa CCM na kumpa sifa kem kem mheshimiwa John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM 

Mkutano unaendelea 

Mkutano unaendelea 
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano wa CCM leo 

Mkutano unaendelea 
Mkutano unaendelea 
Wananchi wakifurahia jambo kwenye mkutano 
Mkutano unaendelea 
Mheshimiwa Lusinde akiwahutubia wakazi wa Shinyanga 
Tunafuatilia kinachoendelea hapa..... 

Mheshimiwa Lusinde akiwa na wagombea ubunge majimbo yote ya Shinyanga,ambapo mmoja pekee wa jimbo la Solwa mheshimiwa Ahmed Salum hakuwepo kwenye mkutano huo kutokana na kuwa katika shughuli zingine za kichama 
Wabunge watarajiwa majimbo ya Shinyanga wakiwa jukwaani 
Wa tatu kutoka kushoto ni mgombea ubunge jimbo la Kahama mjini mheshimiwa Jumanne Kishimba 
Wanachama wa CCM wakicheza uwanjani 
Baada ya mkutano kila mmoja akaendelea na shughuli zake wengine wakapanda kwenye magari yao kurudi makwao 
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano 
Wazee wa CCM wakiwa eneo la tukio 
Vijana wa Greenguard wakiwa eneo la tukio 
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

NOMA SANA!! ANGALIA PICHA MAGUFULI AZIDI KUCHANJA MBUGA,AWATAKA WANANCHI WAWEKE IMANI KUBWA KWAKE NA KUMPA KURA NYINGI ZA USHINDI

$
0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Njombe mjini katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa saba saba.Magufuli amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataendeleza juhudi zake za kujenga barabara kwa kiwango cha lami,amesema dhamira yake aliokuwa nayo ya Uwaziri wa Ujenzi katika kujenga barabara za lami katika maeneo yote hapa nchini.
Amesema tangu kupewa kuwa waziri wa ujenzi ameweza kujenga barabara zaidi kilomita 7000 nchi nzima,ambapo ilipelekea kuongeza kuongeza pato la mfuko wa barabara kutoka bilioni 73,3 hadi kufikia bilini 866 kwa mwaka huu hivyo ameahidi akiwa rais atajenga zaidi barabara za lami.
Dkt MAGUFULI ambae anaendelea na mikutano ya kampeni za Urais mikoa ya nyanda za juu kusini , amelalamikia udanganyifu wa baadhi ya mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali ya mkoa wa mbeya wakati sio kweli.
Aidha pia Magufuli amewaomba wananchi waweke imani kubwa kwake kwa kumpa kura nyingi zitakazomwezesha kuwa raisi wa awamu ya tano,na kIsha alipe fadhira hizo kwa kutatua kero zinazowakabili hasa wananchi wenye kipato cha chini
Mgombea Urais wa CCM Dkt Joh Pombe Magufuli akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Ndugu Phillip Mangula mara baada ya kumkaribisha mgombea huyo jukwaani kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Ndugu Phillip Mangula akiwashukuru wananchi wa Njombe waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa sabasaba mjini humo,ambapo pia Ndugu Mangula alimkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano
Wananchi wa Njombe wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa sabasaba mjini Njombe.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na Mgombea Ubunge wa jimbo la Kyela,Mh Harrison Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Njombe jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
Waanchi wakishangilia jambo kwenyemkutano wa kampeni wa CCM.
Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Mh. Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe
Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Mh. Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe kwa ajili ya kuwaambia wananchi ni namna gani wataiongoza Tanzania katika awamu ya tano. 
Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Makete Dkt Norman Msigala kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe
MKutano wa Kampeni ukiendelea. 
Wananchi wakisikiliza sera za mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,hayupo pichani alipowahutubia jioni ya leo mjini Njombe. 
Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni
Wananchi wakiwa na mabango yao ya kumsifu na kumkaribisha mgombea Urais wa CCM Ndugu John Pombe Magufuli,mara baada ya kufunga barabara alipokuwa akipita katika kijiji cha Mgagala akielekea mkoani Njombe kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi na Mabango yako
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Makoga katika wilaya ya Wanging'ombe mapema leo mchana.
Wananchi wa kijiji cha Ikonda wakimsikiliza Dkt Magufuli 
Bango

HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU

$
0
0







HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU
Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015

Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu
  1. Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka ishirini na tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.
  2. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za CCM na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio hodhi madaraka na mali za nchi.
  3. Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
    1. Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.
    2. Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama elimu, afya, maji na makazi.
    3. Mabadiliko ya kuondoa umaskini.
    4. Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za maisha.
  4. Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa linakuwa.
  5. Lakini Watanzania wanachotaka siyo takwimu bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na barabara bora zinajengwa.
  6. Wanataka kupata maji safi na salama ya kunywa. Wanataka makazi bora.
  7. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu uhuru ya kuondoa umaskini, maradhi,na ujinga inahitimishwa.
  8. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na utendaji.
  9. Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo ya sera za utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini. Sote ni wahanga wa siasa na sera hizi.
  10. Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka
  11. Tusidanganyike, CCM hawana jipya
  12. Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha ya wananchi.
  13. Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia maendeleo kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma. Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na sasa wananchi wa kanda ya ziwa wanapata maji safi.
Ndugu watanzania
  1. CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.
  2. Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa mikakati sahihi na siyo nadharia.
  3. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa sekta bali wa sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na utekelezaji wa sera za kila sekta utakao leta maendeleo.
  4. Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini utakuwa na nguzo tano:-
    1. Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji.
    2. Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika sekta muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji
    3. Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa wanyonge.
    4. Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji na makazi, na mazingira
    5. Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na sheria chini ya Katiba ya Wananchi.
  5. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.
Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu itatayogharamiwa na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia:-
  1. Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika soko la ajira.
  2. Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata.
  3. Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini.
  4. Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule.
  5. Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za wanafunzi.
  6. Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu ikiwa ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia, usafiri na zana za teknolojia.
  7. Kufuta michango ya maabara ya shule za kata

AFYA 
  1. Afya na tiba ya kila Mtanzania itagharamiwa kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi ya jamii
  2. Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na kinga kupunguza gharama za tiba.
  3. Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki.
  4. Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na kujenga hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii na pia kuepukana na tiba za nje ya nchi.
  5. Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na nyumba na usafiri.
  6. Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma za afya bila kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile serikali na hospitali za sekta binafsi.

ARDHI, MAJI NA KILIMO

  1. Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa ardhi kwa Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na wafugaji.
  2. Tutapima ardhi yote ya Tanzania na kumilikisha vijiji na wakulima kwa hati za serikali ili kuipa thamani.
  3. Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa kuimarisha elimu, ufundi na teknolojia ya kisasa na kumkomboa mkulima kutoka jembe la mkono.
  4. Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa na kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.
  5. Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na kulinda vyanzo vya maji.
  6. Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa kuwapa wakulima elimu na mikopo ya riba nafuu ya kuvuna maji na kujenga miundombinu husika.
  7. Tutaweka mazingira rafiki yatakayomhakikishia kwa kila Mtanzania kupata maji safi na salama. Kumaliza kero za maji nchini kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kuchota maji kwa kichwa
  8. Nitafuta kodi zote za mazao na mifugo kwa wakulima na wafugaji.
  9. Tutasimamia kilimo cha biashara kinachozingatia maslahi ya nchi na ya Watanzania.
  10. Tutaanzisha programu maalum ya kufufua mazao asilia ya Tanzania hususan mkonge.
  11. Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na Uvuvi.

MIUNDOMBINU
  1. Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.
  2. Tutajenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
  3. Tutajenga reli ya kati kwa viwango vya kisasa
  4. Tutajenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
  5. Tutajenga miundombinu ya kisasa na kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha
  6. Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano ya Watanzania

VIWANDA

  1. Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu
  2. Tutajenga viwanda vipya vya kusindika mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
  3. Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano mali ghafi zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili kuongeza mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.
  4. Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa Viwanda

UCHUMI
  1. Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa soko-kijamii ambapo nguvu za soko zitatumikia jamii kwa serikali kuweka uwiano wa mapato unaohakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa ufanisi.
  2. Tutalinda sekta binafsi na bidhaa za ndani kwa kuwapa Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi cha mpito ili waimarike na waweze kuhimili ushindani. Tutawapa wafanyabiashara wetu upendeleo katika manunuzi ya serikali na kuwajengea mazingira mazuri ya biashara na kodi endelevu.
  3. Tutawawezesha Watanzania kupata mitaji ya biashara kwa masharti nafuu kabisa.
  4. Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala maslahi kwa Taifa.
  5. Tutaimarisha sera ya ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi kwenye maeneo muhimu ya kiuchumi na kibiashara. Pia, kuwawezesha Watanzania kuwekeza kwa njia ya ubia na wawekezaji wenye mitaji mikubwa bila kujali wanapotoka.
  6. Tutaimarisha usimamizi kwa kubadilisha mfumo wa Vyama vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na wakulima wenyewe ikiwa na pamoja na kuwawezesha kuboresha makazi kwa mpango wa kushirikiana kujenga nyumba bora
  7. Tutaanzisha na kuwezesha uanzishaji wa viwanda vidogovidogo vinavyotoa ajira kwa wingi kwa kuvihusisha na vyuo vya ufundi na benki maalum kwa lengo hilo.
AJIRA
  1. Tutasimamia swala la ajira hasa kwa vijana kwa kukuza elimu ya ufundi ili waweze kujiajiri
  2. Tutazipa kipaumbele sekta zinazozalisha ajira kwa wingi hasa za viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na utalii na kuzipa unafuu wa kodi ili zikue kwa haraka.
  3. Tutawapa wawekezaji wakubwa katika sekta hizi upendeleo maalum na viwango vya kodi nafuu.
NISHATI NA MADINI 
  1. Serikali itashiriki kikamilifu katika uzalishaji wa nishati
  2. Itatengeneza mazingara mazuri ya kisera yatakayovutia na kuwezesha ushiriki wa Watanzania na ubia kati yao na wageni.
  3. Serikali yangu itaupa uzalishaji mkubwa wa umeme wa maji kipaumbele namba moja, umeme wa makaa ya mawe kipaumbele namba mbili, umeme wa gesi asilia kipaumbele namba tatu na umeme wa urana kipaumbele namba nne.
  4. Serikali itatoa vipaumbele muhimu kwenye usambazaji wa huduma kubwa ya umeme sehemu za uzalishaji uliyolenga masoko ya ndani, ya nchi jirani na ya nchi za kigeni.
  5. Itapitia upya mikataba yote mikubwa ya nishati na madini ili kubaini iliyo mibovu na kuifanyia maboresho.
  6. Serikali yangu itatumia sehemu ya hisa zake kwenye raslimali kubwa ya gesi asilia iliyopatikana hapa nchini kama rehani kwenye kujichukulia mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya mabomba ya gesi.
  7. Serikali itatoza kodi na ada ndogo zaidi kwa wazawa wenye ubia kati yao na wageni kuliko zitakazotozwa kwa wageni wasiowekeza kwa kushirikisha wazawa.

  1. Serikali itasitisha utoaji wa misamaha ya kodi isiyo lazima kwenye sekta ya madini, na badala yake itawekeza kwenye kuongeza thamani ya raslimali zake za madini.
  2. Tutakuza nishati mbadala kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kukata kuni

MALIASILI NA UTALII
  1. Tutasimamia uvunaji na matumizi ya rasilimali za Taifa kwa manufaa ya kila Mtanzania wa kizazi hiki na kijacho
  2. Tutapiga vita ujangiri na kuimarisha utunzanji wa hifadhi za taifa na mazingira
  3. Tutachochea ujenzi wa miundombinu ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli na kuimarisha mafunzo
  4. Tutaongeza idadi ya watalii kufikia milion mbili ifikapo 2020.




UTAWALA BORA, ULINZI WA NCHI NA USALAMA WA RAIA
  1. Tutasimamia Katiba mpya inayolinda haki za msingi za wananchi na kuweka bayana mipaka ya madaraka ya serikali na viongozi, Bunge na Mahakama.
  2. Tutasimamia haki za raia na kuangalia upya sheria kandamizi ili wananchi kama Masheik wa Zanzibar hawasoti jela kwa sababu za kisiasa.
  3. Tutaimarisha mafunzo ya vyombo ya Polisi hasa wapelelezi na waongoza mashtaka ili wapate uwezo wa kusimamia utoaji wa haki.
  4. Tutavipa vyombo vyote vya ulinzi na usalama nyenzo na kuboresha mazingira yao ya kazi na maslahi
UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI
  1. Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania aweze kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku
  2. Tutaimarisha nidhamu, utendaji na uwajibikaji katika Sekta ya Umma
  3. Tutaimarisha mchango wa Wataalam wetu, wanawake na vijana katika kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira stahiki ya kazi pamoja na mafao.
  4. Tutapiga vita rushwa na ubadhirifu katika sekta ya Umma na binafsi
  5. Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa muhimu pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku matumizi ya mashangingi serikalini.
  6. Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza na ukaguzi wa madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
  7. Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri katika shughuli za serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni pamoja na ile ya mafuta, madini na gesi asilia
KUKUZA PATO LA SERIKALI
  1. Tutadhibiti mapato kutokana na raslimali kwa kupitia upya viwango vya mirabaha kutokana na madini na gesi asilia ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gawio stahiki.
  2. Serikali itaanzisha Wizara maalum itakayosimamia nishati ya gesi na mafuta.
  3. Tutaimarisha ofisi ya Msajili wa Hazina ili kusimamia vema uwekezaji wa Serikali katika mashirika na mapato yake.
  4. Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma yanaendeshwa kwa misingi ya faida na uadilifu.
  5. Tutadhibiti ukwepaji kodi za ushuru wa forodha na kupiga marufuku misamaha ya kodi holela ili kuokoa mabilioni ya fedha yanayopotea kila wiki.
  6. Sambamba na hilo tutarahisisha utaratibu wa kulipa kodi ili kuondoa kero na mazingira ya rushwa. Kwa kudhibiti makusanyo ya kodi tutakusanya fedha za kugharimia huduma za msingi kama afya na elimu kikamilifu.
KUIMARISHA MUUNGANO 
  1. Tutaimarisha umoja, usalama na udugu wa Watanzania na Muungano kwa misingi ya haki na usawa
WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE
  1. Wanawake watapewa fursa na haki sawa katika elimu na uchumi ili waweze bila kuwezeshwa.
  2. Tutahakikisha wazazi wanapata fursa ya kuwa walezi na wafanyakazi kwa kuongeza urefu wa likizo ya uzazi
  3. Tutaimarisha elimu ya watoto hasa wasichana na kukuza fursa zao na kukomesha ndoa za watoto wadogo.
  4. Tutaongeza uwakilishi wa akina mama katika ngazi zote serikalini na mashirika yake kufikia asili mia hamsini ifikapo 2020.
  5. Wazee na wasiojiweza watapewa posho ya kujikimu inayokidhi mahitaji ya msingi itakayowawezesha kuishi kwa heshima na kulinda utu wao ndani ya familia na jamii zao.

SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO

  1. Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya sanaa na michezo
  2. Tutarudisha viwanja vya michezo vilivyovamiwa
  3. Tutafuta kodi zote za vifaa vya michezo.
  4. Tutadhibiti viwango na maadili ya bidhaa za nje zinazoingizwa nchini na kuzitoza kodi halisia
  5. Tutajenga taasisi na vyuo vya kukuza michezo ili kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania inashiriki kwa ushindi katika mashindano ya kimataifa ya soka na riadha
  6. Tutalinda Hakimiliki za sanaa nchini
  7. Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii chipukizi ili kuwapa muda kwa kujijenga.
SERA YA MAMBO YA NJE YENYE TIJA KWA TAIFA
  1. Tutakuza ushirikiano wa Kimataifa wenye tija na Ujirani mwema.
  2. Tutatetea haki za binadamu, usawa wa nchi na kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika diplomasia ya kimataifa.
  3. Tutakuza umoja na ushirikiano wa Umoja wa Afrika, Jumuia ya Afrika Mashariki, SADC na Umoja wa Mataifa.
  4. Tutaimarisha Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kudai mabadiliko ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi shiriki.
Ndugu Watanzania
Naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo
  1. Natambua kuwa uongozi ni dhamana. Mkinichagua nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka.
  2. Nawaahidi Watanzania kuwa kwa uwezo, akili, uzoefu na nguvu zangu zote nitawatumikia. Nawaomba nanyi mniahidi jasho lenu na uwezo wenu wote ili kwa pamoja tuvuke. Tutajikomboa toka utawala wa CCM unaodumaza uchumi na maendeleo. Tutaanza safari ya uhakika kuondoa umaskini.
  3. Mabadiliko pia ni kuthamini utu na kukataa hadaa ya hongo ili kuuza haki yako ya kuchagua. Msikubali rubuni za uchaguzi kwa kupewa pesa au vitu. Rushwa ya uchaguzi ndiyo sera ya CCM. Ukikubali basi umeuza pia haki na sauti yako ya kuwalalamikia walio madarakani. Imetosha. Tukatae. Tulinde utu na haki zetu. Tuchague mabadiliko.
  4. Mabadiliko ni fikra. Ni kufikiri na kutenda tofauti. Hatuwezi kuendelea kufikiri na kutenda kama kwamba hatuna dharura ya maendeleo. Kwanza tuanze kwa kufanya mabadiliko na tujiamini kuwa sisi kama Taifa tunaweza. Tunaweza kujitegemea na kuleta maendeleo yetu wenyewe bila kutegemea wafadhili. Hii si ndoto. Nchi nyingi zimefanikiwa kuondoa umaskini katika kizazi kimoja. Tujifunze kutoka kwao.
  5. Tuwe taifa linalotumia raslimali zake kujiendeleza na siyo kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania watwana katika nchi yao. Inabidi tuache kuwa taifa ombaomba. Tuache kuukubali na kuvaa umaskini kama joho la fahari.
  6. Mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na CCM. Tusitegemee kuwa leo wana jipya. Ndiyo maana ahadi walizotoa miaka thelathini iliyopita ndizo wametoa juzi. Tukatae hadaa. Miaka hamsini ya CCM imetosha.
  7. Tunaamani kwamba tutashinda kwa sababu Watanzania mpo nyuma yetu. Watanzania mmeamua kuleta mabadiliko. Kura yako ndiyo itakayokuwa mkombozi wako. Hakikisha unapiga na kuilinda kura yako. Wakati wa mabadiliko ni sasa.
Mungu ibariki Tanzania. Asanteni sana

ZIKO HAPA SENTENSI 12 ZA WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRICK SUMAYE KWENYE MKUTANO WA UKAWA JANGWANI DAR ES SALAAM

$
0
0


Sumaye: "Kama kipimo cha uadilifu ni Kinana Katibu mkuu wa CCM, basi mimi nitakuwa mtakatifu" Serikali hii ni dhaifu sana na alituthibitishia katibu mkuu, mwenyewe kusema kuna mawaziri mizigo.


Sumaye: "Lowassa angekuwa mbaya asingeteuliwa kuwa waziri mkuu, hakuna Rais anayemteua mtu mbaya kuwa waziri mkuu " Leo Lowassa ametoka CCM ameonekana hafai, lakini ni Kikwete aliemfanya waziri mkuu wake, kuna Rais anaweka kiongozi ambae hafai?

Sumaye: "Lowassa ndiye aliyemuingiza Kikwete madarakani, kama angekuwa mla rushwa asingekuwa bado yupo nchini"

Sumaye: "Lowassa alijiuzulu kumuokoa Kikwete , waziri siku zote anabeba mzigo kumuokoa "Nyerere wakati anastaafu, alisema hajaona mtu mvumilivu kama Kawawa, alibeba mizigo wa kubeba yeye, ndiyo kazi aliyofanya Lowassa.Mmewasikia kwenye kampeni, fisadi mkubwa huyo amechukua fedha za matajiri, Lowassa amechukua ustaarabu kuwajibika ili kumuokoa Rais.

Sumaye: "Lowassa ametoka madarakani miaka 8 iliyopita, hivi twiga walipopandishwa ndege Lowassa alikuwepo??"

Sumaye: "Serikali hii ni dhaifu sana, aliyethibitisha hilo ni katibu mkuu wa CCM aliposema kuna mawaziri mizigo"

Sumaye: "Wanasema eti Lowassa ni mgonjwa, kwani huyo Magufuli ni mzima??" Wanasema mgonjwa, kwani Magufuli mzima? Wanaenda kufanya nini Ulaya, mtu yeyote ukishavuka miaka 50 hauwezi kuwa wazima kwa 100%

Sumaye: "Kwani Rais Kikwete akiwa madarakani hakwenda Marekani kufanyiwa upasuaji mkubwa wa tezi dume???

Sumaye: Rais si kazi ya kubeba zege Ikulu, anatakiwa kuwake timu nzuri ya kazi, yeye ni meneja tu.
Watanzania leo elimu inashuka sana, tunashusha alama za kufaulu wanafunzi ionekane wamefaulu wengi, pia ukienda ktk afya

Sumaye: Tulitaka kufanya mabadiliko kulekule, kukawa na tatizo ndani ya CCM, ukitaka kufanya lolote wanakuzingira. 

Sumaye: Wanawajaza watanzania uoga wa usilolijua, mkiwapa wapinzani wataharibu nchi, kila binadamu ana uoga wa asilolijua.

NIMEKUSOGEZEA MAGAZETI YOTE YA TANZANIA LEO JUMAPILI,AGOSTI 30,2015,KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZIKO HAPA

$
0
0
.
Kutoka Dar es Salaam Tanzania leo Jumapili Agosti 30,2015 tayari nimeyakusanya Magazeti yote na stori zake kubwakubwa kukusogezea hapa, headlines baada ya headlines kwenye Magazeti ya Michezo na Hardnews, zote ziko hapa
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Chanzo-Millardayo.com

LULU KACHUMBIWA?? PICHA HII IMEZUA UTATA

$
0
0
Elizabeth Michael aka Lulu amewaacha mashabiki wake njia panda baada ya kuweka picha inayoonesha amevaa pete ya uchumba.

Picha aliyoweka Lulu na kuibua maswali kibao kutoka kwa mashabiki wake

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mrembo huyo aliweka picha ya mitego ikiwa na caption ‘N.U.D.I’ na hivyo kuwaweka njia panda mashabiki wake.

Hizi ni baadhi ya comments za mashabiki:

Aubrey_bittoria. Is she engaged?

Ms_gikaro. Engagés or?

Richi_manyota. Ww lulu unatuuwa bhna
Viewing all 2674 articles
Browse latest View live