Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imemteua aliyekuwa naibu Spika wa Bunge la 10 Job Ndugai, kuwa mwakilishi wa chama hicho atakayegombea nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye atapigiwa kura na wabunge wa hapo kesho kuwania nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Dodoma kupitia Katibu wa Itikadi na Unezi, Nape Nauye, amesema Dkt. Tulia Mwansasu na Mbunge wa Afrika Mashariki, Abdulla Ally Mwinyi waliamua kujitoa katika nafasi hiyo hivyo kumpa nafasi Job Ndugai kupita bila kupingwa.