Quantcast
Channel: DUNIA KIGANJANI BLOG | Ifanye Dunia Kuwa Yako
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2674

MKAPA AMPA WASIA DKT MAGUFULI NA KUSEMA MANENO HAYA

$
0
0
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amempa wasia Rais Dk John Magufuli, akitaka Serikali yake ikae na wadau ili kuinua kiwango cha taaluma kinachotolewa nchini.
Mkapa alitoa kauli hiyo jana wakati wa harambee ya kuchangia Mfuko wa Dhamana ya Elimu (CDM-ETF) unaomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi.
Mkapa alisema tangu astaafu mwaka 2005, amekuwa akisita kuzungumzia sera na maendeleo ya nchi kwa kuogopa kuambiwa anaingilia shughuli za Serikali za awamu zilizomfuata.
Alisema kwa kuwa awamu ya tano chini ya Dk Magufuli ndiyo imeingia madarakani na bado Baraza la Mawaziri halijaundwa, ameona atoe mchango wake kuhusiana na sekta ya elimu.
“Mimi ningeishauri Serikali mpya na hasa Wizara ya Elimu ingejitahidi kukutana na wamiliki wa shule binafsi, viongozi wa shule za Serikali ili kuweka mipango ya pamoja ya kuwezeshana,” alisema.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, Issac Aman, alisema mfuko huo unahitaji zaidi ya Sh1 bilioni na katika harambee alichangia Sh10 milioni, huku Mbunge mteule wa Vunjo (NCCR- Mageuzi), James Mbatia akichangia Sh5 milioni.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2674

Trending Articles