Quantcast
Channel: DUNIA KIGANJANI BLOG | Ifanye Dunia Kuwa Yako
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2674

LHRC: POLISI WANAENDELEA KUSHIKILIA VIFAA VYETU VYA KAZI

$
0
0

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.  Hellen-Kijo Bisimba, amesema vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na kituo  hicho kukusanya taarifa za uchaguzi vilivyochukuliwa na polisi,  havijarudishwa.

Alisema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi jana na kufafanua kuwa  kwa mujibu wa taarifa walizopewa na polisi, bado uchunguzi dhidi ya  vifaa hivyo unaendelea na vitarudishwa baada ya shughuli hiyo  kukamilika.

Aidha, alisema anasikitishwa na kitendo hicho kilichofanywa na polisi  kwani walikuwa wakifanya kazi hiyo kisheria na kwa haki bila kuegemea  upande wowote na kwa maslahi ya taifa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2674

Trending Articles