Mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Coastal Union (kulia).
Muonekano wa X-Ray ya kichwa ya Nsa Job baada ya kupigwa jiwe mjini Moshi juzi Usiku.
UCHUNGUZI wa mwanzo wa madaktari katika Hospitali ya KCMC mjini Moshi, unaonyesha Nsa Job ameumia sana.
Rafiki yake wa karibu leo amesema bado hali ya kiungo huyo na mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Coastal Union si nzuri.
“Walifanya kipimo cha CT Scan kuangalia kuhusiana na fuvu lake. Inaonekana limeumia sana kwa kweli na hali yake si nzuri,” alisema rafiki huyo.
Nsa alipigwa jiwe kubwa juzi usiku karibu na nyumba na Davis Mosha ambaye ni mgombea wa ubunge Moshi Mjini kupitia CCM.
Alikuwa akitokea kwa Mosha ambaye ni rafiki yake, watu wanaosadikiwa ni wafuasi wa Ukawa ndiyo walipiga jiwe lililopasua kioo cha gari alilokuwamo na kumjeruhi vibaya.
(CREDIT: SALEHJEMBE)