Msanii wa filamu na muziki anayekuja kwa kasi, Taiya Odero.
MSANII wa filamu na muziki anayekuja kwa kasi, Taiya Odero amedai kuponzwa na filamu za usaliti anazocheza kwa kuwa wanaume wengi wanamuogopa kumtongoza wakimuhofia kuwasaliti katika mapenzi.
Akizungumza na Amani, Taiya alisema kuwa anapokuwa katika uhusiano na mtu huwa inampa wakati mgumu sana kwa kuwa mtu huyo anakuwa na hofu ya kusalitiwa kila mara.
“Wakati mwingine najuta hata kwa nini nacheza filamu za kuwasaliti wanaume. Maana kila ninapopata mchumba, wakati wote anakuwa na wasiwasi wa kusalitiwa,” alisema Taiya.