
Kwa mujibu wa Dr. Fredrick Mashili kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) amesema sababu kubwa inayopelekea watu kupata magonjwa hayo ni kukaa muda mrefu maofisini au kwenye foleni na kutofanya mazoezi baada ya kutoka makazini.
Akitolea mfano wa ripoti ya hivi karibuni kutoka Shirika la Moyo la Marekani lilichapisha makala yenye kichwa cha habari “International Cardiovascular Desease Statistics” limeeleza kuwa kutofanya mazoezi na kula vyakula visivyofaa ni moja ya mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa magonjwa hayo.
Dr. Mashili ameeongeza kuwa kukua kwa Teknolojia kumechangia watoto kukosa muda wa kucheza badala yake hupendelea kukaa na kucheza michezo ya kwenye kompyuta na video (Gaming), tatizo ambalo ni kubwa kwao kwasababu hupelekea watoto kutojiheshimu, kuwa na wasiwasi mwingi na kufadhaika kila wakati.