Serikali imewataka watanzania kutokuwa na mashaka juu ya utekelezazaji wa mradi wa Bomba la mafuta baina ya Tanzania na Uganda wenye urefu kwa kilomita 1,443 kwani utakamilika kabla ya mwaka 2020.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar-es-salaam na waziri wa nishati na madini Prof. SOSPETER MUHONGO kwenye mdahalo wa wakuu wa mikoa na Makatibu wakuu wa kujadili mradi huo utakaogharimu jumla ya shilingi Billioni 3.5.
Prof. MUHONGO amewataka Makatibu wakuu na wakuu wa mikoa kusimamia utekelezaji huo kabla ya muda uliopangwa kulingana na agizo la rais Dkt JOHN POMBE MAGUFULI na Rais wa Uganda YOWERI MUSEVEN.
Hatika hatua nyingine Prof. MUHONGO amewataka wananchi kuwa makini katika ununuaji wa ardhi katika mikoa inayopitiwa na bomba hilo ikiwemo Shinyanga na Geita kwani huenda wakauziwa maeneo ambayo tayari ni ya mradi huo.
Prof. MUHONGO amewatahadharisha wanaotaka kununua maeneo katika eneo litakapopita bomba hilo na kujenga majengo yao ili kulipwa fidia, kuachana na dhana hiyo kwani serikali itaangalia majengo yaliyojengwa kabla ya Agosti mwaka jana.
Prof. MUHONGO amesema KATIKA kikao kilichofanyika nchini Uganga wamepitisha Bomba hilo kuitwa “The East African Crude Oil Pipe Line”, na kutaka wataalum kutumia jina hilo ili endapo kukitokea hitilafu popote duniani iweze kufahamika kwa urahisi.