
Good news mtu wangu, ile collabo ya kundi la Mafikizolo kutoka South Africa na mtu wetu Diamond Platnumz imetoka!
‘Tell Everybody’ ndio njia la wimbo, na ni wimbo ambao ni sehemu ya project ya Umoja wa Mataifa iitwayo UN Sustainable Development Goals (SDGs) yenye dhamira ya kupambana kutokomeza umasikini, kurekebisha tabia nchi na kuhamasisha usawa kufikia mwaka 2030.
Diamond Platnumz.
Wimbo huu umeshirikisha pia wasanii kutoka nchi nyingine za Kiafrika, wapo wakina Yemi Alade kutoka Nigeria, Sauti Sol kutoka Kenya, Toofan kutoka Togo, Becca na Sarkodie kutoka Ghana na Diamond Platnumz ndiye staa aliyewakilisha +255 Tanzania pamoja na Mafikizolo kutoka South Africa!
Kuna mchanganyiko pia wa lugha mbalimbali ikiwemo Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili na Kizulu... kizuri zaidi ni kwamba kila verse utakayoisikia kwenye wimbo huu basi ujue imeandikwa na msanii mwenyewe!
Hapa ninazo baadhi ya picha za wasanii walioshiriki kufanikisha hii project mtu wangu…

Becca Kutoka Ghana

Diamond Platnumz, Tanzania.