Hayo yamesemwa jana na Kamanda mpya wa Jeshi hilo mkoani humo ACP MULIRO JUMANNE MULIRO mjini Shinyanga alipokutana na waandishi wa habari mkoani humo kwa lengo la kujitambulisha.
Akielezea baadhi ya mikakati yake Muliro amesema hatakuwa tayari kufanyakazi na askari wanaobambikizia watu wasio na hatia kesi kwa lengo la kujipatia rushwa na atahakikisha upelelezi wa mashauri yote unakamilika kwa muda mfupi.
Muliro ametaka askakri polisi kutenda haki, kuepuka matumizi ya lugha chafu na vitendo vya rushwa ambavyo vimekuwa vikilitia doa jeshi la polisi na kwamba tathmini ya mambo hayo itafanyika kila mwezi.
Amesema atahakikisha analiongoza jeshi hilo kwa weledi akishikisha wananchi pamoja na vyombo vya habari katika kufukia malengo hayo.