Quantcast
Channel: DUNIA KIGANJANI BLOG | Ifanye Dunia Kuwa Yako
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2674

TASAF Mkoa Wa Shinyanga Yaomba Msaada Kuhakiki Kaya Zilizoingizwa Katika Mpango Wa Kunusuru Kaya Masikini Kimakosa

$
0
0
Jamii imeombwa kutoa ushirikiano kwa wasimamizi wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF III mkoani Shinyanga, katika kuhakiki kaya zisizo na sifa ambazo ziliingizwa katika mpango huo kimakosa.

Akizungumza jana na Dunia Kiganjani Blog kwa njia ya simu, Mratibu wa TASAF mkoa wa Shinyanga MALIGISA DOTTO, amesema kukosekana kwa ushirikiano miongoni mwa jamii ni changamoto ambayo pia husababisha kupatikana taarifa zisizo sahihi.

DOTTO amesema endapo viongozi wa ngazi ya kata na vijiji watatoa ushirikiano wa kutosha itasaidia kuchambua kaya hizo na kufanya tathimini kwa kina kugundua kaya zinazostahili kubaki na ambazo ziliingizwa kimakosa.

Amesema uhakiki uliofanyika umebaini kwamba baadhi ya watu walioingizwa kwenye mpango huo ni viongozi wa serikali ambao hawastahili kuwemo kulingana na waraka wa kutambua kaya masikini.

Amesema kuwa kutokana na waraka huo kutoruhusu watumishi wa serikali kuandikishwa imesababisha baadhi ya viongozi wa vijiji kuandika barua za kujiuzulu nyadhifa zao hali ambayo husababisha usumbufu kwa wananchi kuanza kutenga muda wa kuchagua viongozi wengine.

Mkoa wa Shinyanga umebaini kuwepo kwa kaya masikini hewa 949 katika mpango huona kuziondoa katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei mwaka huu kati ya kaya masikini 34,833 zilizotambuliwa katika mkoa huo.

Kwa upande wa Kaya zilizoingizwa kimakosa katika mpango huo, Halmashauri ya Kahama Mji imebainika kuwa na kaya 113, huku Halmashauri ya Msalala ikiwa na Kaya 94 na Ushetu kaya 137.

Na. Amina Mbwambo, Dunia Kiganjani Blog - Kahama


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2674

Trending Articles