
Mkuu wa wilaya ya Kahama FADHILI NKULU amewaweka mahabusu afisa afya wa halmashauri ya mji wa Kahama JOHANNES MWEIBESA na Afisa mtendaji wa kata ya Nyasubi INNOCENT EPHRAIM kwa kushindwa kusimia zoezi la usafi katika kata hiyo.
Afisa habari wa halmashauri ya mji huo CHARLES MNYANI ameiambia Dunia Kiganjani Blog jana kwamba, watumishi hao wamekamatwa jana jioni na kuachiwa saa tatu usiku, kwa lengo la kuwawajibisha kwa kushindwa kusimamia uzoaji wa taka kama walivyoagizwa.
MNYANI amesema hatua hiyo ni kuwakumbusha viongozi na watumishi wote wilayani Kahama kwamba zoezi la usafi linastahili kusimamiwa kwa umakini mkubwa na wala sio la muda maalum kama baadhi ya watu wanavyodhania.
Dunia Kiganjani Blog inamtafuta mkuu huyo wa wilaya ili kupata ufafanuzi zaidi juu ya mikakati aliyoiandaa katika kutekeleza zoezi la usafi wilayani humo.
Na. Marco Mipawa, Dunia Kiganjani Blog - Kahama