Headlines za Tanzania kwa sasa ni kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu2015,Wagombea wa nafasi mbalimbali wanapita kila sehemu,kila Mkoa,kila Wilaya kunadi sera zao ambapo leo Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi kwenye nafasi ya Urais John Magufuli ameongea na wapiga kura wa Mtwara.
Kwenye hotuba yake Mheshimiwa Magufuli kuna maeneo ambayo aliamua kuyazungumzia kwamba akifanikiwa kuwa Rais wa nchi hii ni miongoni mwa mambo atakayoyashughulikia,mambo hayo ni pamoja na mikopo ya Wanavyuo,Kuporwa na kuuwawa kwa Polisi,nimekurekodia pia mtu wangu.