Quantcast
Channel: DUNIA KIGANJANI BLOG | Ifanye Dunia Kuwa Yako
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2674

WATUMISHI WANNE WA SERIKALI WALIOSAFIRI KWENDA NJE YA NCHI BILA RUHUSA YA RAIS MAGUFULI WAFUKUZWA KAZI

$
0
0

Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.
 
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.

Agizo hilo la Rais Magufuli  lilitolewa jana na Balozi Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.
 
Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuonya kuwa atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2674

Trending Articles