Quantcast
Channel: DUNIA KIGANJANI BLOG | Ifanye Dunia Kuwa Yako
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2674

CHAMA CHA WAHASIBU TANZANIA (TAA) CHAAHIDI KUPAMBANA NA WAHASIBU WALA RUSHWA, WEZI NA MAFISADI

$
0
0
CHAMA cha Wahasibu Tanzania (TAA) kimetishia kuwaondoa wahasibu waliokuwepo kwenye daftari la chama hiko endapo watakiuka taratibu na maadili ya kazi kulingana na matakwa ya chama hicho ikiwemo ya rushwa, wizi na ufisadi.

Hayo yalisemwa jana  jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho, Fred Msemwa katika mazungumzo yake na wanahabari wakati akitoa pongezi na kuunga mkono kwa jitihada za serikali ya awamu ya nne juu ya ukusanyaji wa mapato.

Msemwa alisema kuwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu, wanatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa taaluma zao kwa kufuata miongozo ya sheria Na.33 ya 1973 inayosimamia taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu Tanzania.

Amesema kuwa chama hicho hakitasita kumundoa mhasibu yoyote atakayeshiriki katika wizi na mambo mengine kinyume na matarajio ya wananchi ataondolewa haraka.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2674

Trending Articles