Quantcast
Channel: DUNIA KIGANJANI BLOG | Ifanye Dunia Kuwa Yako
Viewing all 2674 articles
Browse latest View live

NEWS ALERT!!!! "DILI LIMEBUMBURUKA".....MAGOGO YA MILIONI 300 YAKAMATWA BANDARINI YAKIPELEKWA NCHINI CHINA KINYEMELA

$
0
0
Kontena 37 zenye shehena ya magogo aina ya mninga yenye thamani zaidi ya Sh. milioni 300 zimekamatwa zikiwa zinasafirishwa kuelekea nchini China bila kibali.

Katika shehena hiyo, kontena 31 zimekamatiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kati ya hizo mbili zimekamatwa mkoani Mbeya, na mikoa ya Rukwa na Pwani katika maeneo ya Kibaha na Kongowe, kontena moja kila sehemu na Mbezi ya jijini Dar es Salaam, pia imekamatwa kontena moja na kufanya idadi ya kontena zilizokamatwa kufikia idadi 37.


Kontena hizo zinazodaiwa kutoka nchini Zambia, zimekutwa hazina kibali cha usafirishwaji na kusababisha serikali kupoteza mamilioni ya fedha. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Adelhelm Meru, alisema kontena hizo zimeonyesha kupitishwa mpaka wa Tunduma ili zionekane zimetokea nchini Zambia.


Alisema kuna uhalifu wa ukataji wa magogo ambao unafanywa na baadhi ya watu kwa ajili kuharibu maliasili ya nchini.

Dk. Meru alisema vyombo vya upelelezi vya wizara hiyo, vilipata taarifa ya kuwepo na magogo bandarini ambayo yalitakiwa kusafirishwa nje ya nchi.


Alisema mara baada ya kupata taarifa hizo, walizifanyia kazi na kufanikiwa kuzikamata kontena 31 ambazo hazikuwa na kibali cha usafirishaji.


"Baada ya kuzikamata tulichokifanya tulienda kuonana na balozi wa Zambia tukawaeleza na wenyewe wanasema hawawezi kutoa kibali kwa kuwa wanakataza ukataji wa magogo nchini kwao, " alisema.


Aliongezea kuwa ; "Inawezekana magogo hayo wameyakata nchini na kufanya udanganyifu wa kwenda kuzunguka katika mpaka wa Tunduma kuonyesha kuwa yametokea Zambia, lakini balozi ameahidi kushirikiana na sisi."

Dk. Meru alionya yoyote atakaye bainika kuhusika katika suala hilo atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria ili na wengine wajifunze kupitia tukio hilo.


Alisema Serikali ya Zambia na Tanzania zimeingia makubaliano ya kudhibiti biashara haramu ya ukataji wa magogo.


Naibu Balozi wa Zambia, Elizabeth Phiri, alisema sheria inazuia usafirishaji wa magogo, hivyo hana uhakika kama ni kweli vibali vimetolewa nchini kwake. Tunasubiria tupatiwe document (nyaraka) zinazoonyesha tumeruhusu usafirishaji wa magogo hayo ndipo tutalitolea taarifa, alisema Phiri

Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala za Huduma za Misitu, Zawadi Mbwambo, alisema jumla ya kontena 37 zilizokamatwa zikiwa na magogo hayo na nyingine zipo kwenye vituo vyao vya ukaguzi.


Alisema hakuna uhakika kama kontena hizo zimesafirishwa kihalali kwa kuwa walipewa taarifa kuwa yalikuwa yanapelekwa China kwa ajili ya kutengeneza samani na dawa.


Aidha, alisema kampuni tatu zimeonekana kuagiza mzigo huo ambazo ni Pan Atlantic, Best Ocean Air na Dar Global.

BREAKING NEWZZZZ!!!! PAPA FRANCIS KUMFUFUA NYERERE.....MAMA MARIA NYERERE ATANGULIA UGANDA

$
0
0
ZIARA ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis nchini Uganda imetajwa kuwa itafufua mchakato wa kumtangaza Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mtakatifu.


Kwa mujibu wa mtandao wa ETN wa nchini Uganda, ziara hiyo ya kitume ya Papa Francis itamfikisha katika eneo la Namugongo ambalo mashahidi wa imani ya dini ya Kikristu walichomwa moto.


Ni katika eneo hilo la Namugongo ambako Hayati Nyerere alitangazwa kuwa Mwenyeheri huku mchakato wa kumtangaza mtakatifu ukiwa ulianza miaka tisa iliyopita.


Namugongo ndiko ambako pia waumini wa dini ya Kikristu wa Afrika Mashariki na sehemu nyingine duniani hufika kuhiji.


Taarifa ya ETN imeeleza kuwa ziara ya Papa Francis Namugongo itasaidia kufufua mchakato uliodumu kwa miaka tisa sasa wa kumtangaza Hayati Baba wa Taifa kuwa mtakatifu.


Tayari mjane wa Hayati Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere yuko nchini Uganda ambako amekwenda kujumuika na waumini wengine wa dini ya Kikristu kumpokea na kushiriki ibada itakayoongozwa na Papa Francis.


ETN imemkariri Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, akisema kuwa mchakato wa kumtangaza Hayati Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu umetokana na mchango wake wa kuhimiza heshima na usawa kwa binadamu ambao aliutoa wakati akiwa kiongozi.


Kwa mujibu wa ETN, Rais Museveni amesifu mchango wa Hayati Mwalimu Nyerere ambao haukuwa tu wa kuunganisha Watanzania bali alifanya kazi kwa kujali utu wa Waafrika.


“Hayati Julius Nyerere alikuwa mwanaharakati wa Afrika ambaye alimpenda Mungu na alijali utu, aliwaunganisha Watanzania wa dini zote na alisaidia ukombozi wa mataifa mengine ya Afrika kama vile Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika Kusini na Uganda,” alisema Museveni.


Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini, jana alisema mchakato wa kumtangaza Hayati Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu unaendelea vizuri.


Alisema suala la kuendesha mchakato huo ni jukumu la Tanzania na si Uganda hivyo jina la Hayati Mwalimu Nyerere linaweza kuibuka katika ziara ya Papa nchini Uganda kwa kutajwa tu, kwa sababu Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, amekuwa na mazingira ya karibu na familia ya Hayati Mwalimu Nyerere.


“Jukumu la kuendesha mchakato wa kumtangaza Hayati Baba wa Taifa kuwa Mtakatifu ni letu na linaendelea vizuri. Kuna mambo mengi ya kuchunguzwa mpaka mtu kutangazwa kuwa mtakatifu, inawezekana Papa akamzungumzia Mwalimu kwa sababu ya Rais Museveni mara kwa mara ameonyesha kuguswa na mwenendo wa mchakato huo,”alisema Askofu Kilaini.


Papa Francis aliwasili nchini Uganda jana jioni saa 4:50 na kulakiwa na Rais Museveni na viongozi wa Kanisa Katoliki nchini humo.


Kwa mujibu wa ziara yake nchini humo iliyotolewa na Kanisa Katoliki la Uganda leo anatarajiwa kufanya ziara ya kitume katika miji ya Munyonyo, Nikiyanja, Nalukolongo, Namugongo, Kalolo na Rubaga na kesho atamaliza ziara yake nchini humo na kusafiri kwenda nchini Afrika ya Kati (CAR).


Taarifa kutoka nchini Uganda zinaeleza kuwa ulinzi umeimarishwa na Serikali imeandaa wahudumu wa afya 400 na magari 38 ya kubebea wagonjwa ambayo yamepelekwa maeneo yote ambayo Papa atayatembelea.


Papa Francis atakuwa Papa wa tatu kutembelea taifa hilo ambapo mwaka 1969, Papa Paul VI alitembelea nchi hiyo akifuatiwa na Papa Paul II mwaka 1993.


Kampeni za urais zasimama
Katika hatua nyingine wagombea urais wa vyama vyote wamelazimika kuahirisha mikutano yao ya kampeni kwa ajili ya kupisha ziara ya Papa Francis nchini humo.


Rais Museveni ambaye anawania urais kwa muhula mwingine, aliwaambia wafuasi wa chama chake kuwa atamuomba Papa asaidie kutangaza utalii wa taifa hilo.


Akemea ukabila na rushwa nchini Kenya
Awali kabla hajaondoka nchini Kenya, Papa Francis alihutubia maelfu ya vijana katika Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi ambapo aliwahimiza vijana wa taifa hilo wasijihusishe na ukabila.


Alisema vijana wanaweza kuchangia katika kukabiliana na changamoto za ukabila ambazo zimekuwa zikikwamisha maendeleo ya mataifa ya Afrika.


Aliwashauri viongozi wa Serikali kuhakikisha vijana wanapata elimu na ajira kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee ya kuwazuia kujiingiza katika makundi yenye itikadi kali za kigaidi.


Kabla ya kuhutubia vijana katika Uwanja wa Kasarani, Papa Francis, alitembelea Mtaa wa Kangemi ambako wanaishi watu masikini na kukemea dhuluma ya huduma bora ambazo wanatakiwa wapatiwe masikini.


“Ninafahamu kuhusu tatizo kubwa linalosababishwa na wawekezaji wasio na sura ambao hujitwalia ardhi na hata kujaribu kunyakua viwanja vya kuchezea watoto wenu shuleni. Hili ndilo hufanyika tunaposahau kwamba Mungu aliwapa watu wote ardhi waitumie kwa maisha yao bila kutenga au kupendelea yeyote,” alisema Papa Francis.

NEWS ALERT!!! MAJIPU MATANO SUGU ANAYOTAKIWA KUYATUMBUA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Wasomi, wanasiasa na watu kutoka makundi mengine ya jamii wamesema Rais John Magufuli atapimwa katika miaka mitano ijayo kwa mambo makubwa matano yaliyoonekana kuwa ‘majipu sugu’ na changamoto kwa mtangulizi wake, Jakaya Kikwete.


Majipu (mambo matano) hayo ni;
1.Kudhibiti mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya. 
2.Kukomesha rushwa na ufisadi. 
3.Kufumua mtandao wa majangili. 
4.Kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana na 
5.Kuua ‘mchwa’ unaoitafuna fedha za Serikali.


Maoni yaliyotolewa na wasomi, wanasiasa na wananchi wa kawaida yanaonyesha kwamba kufanikiwa kwake kutategemea aina ya ushirikiano atakaoupata kutoka kwa wananchi na wanasiasa na hasa wa kutoka chama chake.


Mhadhiri kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Elijah Kondi alisema Dk Magufuli anahitaji kupigana vita kali kufanikisha ahadi zake na akaonya kuwa hawezi kusimama mwenyewe na kushinda vita hiyo bila kuungwa mkono na wananchi hasa chama chake, CCM.


“Vigogo wengi ndani ya chama chake wamekuwa wakihusishwa na majipu hayo. Hivyo, kufanikisha azma hiyo, kutategemea wingi wa wanaCCM watakaomuunga mkono, lakini kama watakuwa wachache, itakuwa vigumu. Hilo hata yeye (Magufuli) analifahamu ndiyo maana anasema vita hiyo ni kubwa,” alisema Kondi.


Pia, alisema kushughulikia mtandao wa dawa za kulevya, ujangili na kuanzisha mahakama ya mafisadi kutategemea ushirikiano atakaoupata kutoka kwa watendaji na baraza lake la mawaziri.


Kondi alisema kushindwa kwa Rais mstaafu Kikwete katika mambo hayo kulitokana na udhaifu wa baraza lake la mawaziri na watendaji wa taasisi za Serikali. 

“Rais anaweza kuwa na dhamira njema, lakini je, atapata mawaziri wazuri wa kumsaidia? Hao mawaziri watakuwa na ari gani ya kushiriki vita hiyo?” alihoji na kuongeza:


“Kwa sababu anaweza kuanzisha mahakama ya mafisadi lakini ikashindwa kuonyesha uhai kama anavyotarajia. 

"Jaribio la kutumbua majipu hayo itategemea ushirikiano wa chama chake, mawaziri atakaowateua na watendaji wa Serikali.”


Mhadhiri wa Idara ya Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda alisema kilichosababisha marais waliomtangulia kushindwa kutumbua majipu hayo ni utofauti mkubwa ulioonekana kati yao.


“Utofauti katika uwezo wao ukoje? Dhamira zao zinatofautianaje? Lakini hata kiwango cha utashi wa kushughulikia hilo jipu kinatofautianaje na uongozi uliopita. Ukisikiliza kauli ya Rais Magufuli anaonyesha matumaini,” alisema Mbunda.


Meneja wa Soko la Machinga Complex, Nyamsukura Masondore alisema kupandishwa mahakamani kwa vigogo wa Serikali katika kashfa ya EPA ni sehemu ya juhudi zilizoonekana kwa uongozi uliopita.

“Hivyo, hakuna kitakachoshindikana kwa Rais Magufuli endapo watendaji wa chini watakuwa tayari kubadilika na kutoa ushirikiano wa kushinda vita ya majipu hayo,” anasema


Profesa George Shumbusho wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema ana imani Rais Magufuli anaweza kushughulikia changamoto hizo sugu ambazo ameziita majipu kutokana na historia ya utendaji wake. 

“Rais Magufuli atafanikiwa kazi hiyo kutokana na historia yake ya kutojihusisha kwa karibu na mtandao wa wafanyabiashara wakubwa hapa nchini na nje,” alisema.


Profesa Shumbusho alisema kuwa endapo ataendelea na msimamo huo, changamoto ya ukwepaji kodi, misamaha ya kodi, biashara haramu ikiwamo ya dawa za kulevya zitakoma.


Dawa za kulevya
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alinukuliwa Agosti 2013 bungeni akikiri kuwapo baadhi ya majina ya wabunge miongoni mwa watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini alisema Serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa haraka.


Hata Kikwete wakati wa awamu yake ya kwanza, aliwahi kusema anawajua wauza dawa za kulevya lakini tatizo hilo limeendelea kuwa sugu hadi anamaliza kipindi chake cha pili.


Mwaka huohuo, Umoja wa Mataifa (UN) ulitoa ripoti inayobainisha Tanzania kuwa kinara wa kupitisha dawa za kulevya katika nchi za Afrika Mashariki. 

Kuanzia 2010 hadi 2013 ilipitisha tani 64 za dawa za kulevya aina ya heroine na ikitaja Bandari ya Tanga kuwa njia kuu ya upitishaji huo.


Je, baada ya kuanzishwa kwa Sheria ya Kupambana na Kuthibiti Dawa za Kulevya ya mwaka 2015, Rais Magufuli ataweza kusimamia mapambano dhidi ya vinara wa biashara hiyo?


Ujangili wa tembo
Kabla ya kuondoka madarakani, Rais Kikwete aliwahi kunukuliwa Februari 2014 na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) akikiri kuwatambua majangili 40 wa meno ya tembo na kwamba kiongozi wao anaishi Arusha. Pia, alikiri kuwa vita dhidi ya ujangili ni tatizo sugu.


Vilevile, Mei 2014, ripoti iliyoitwa ‘Ivory’s Curse: The Militarization and Professionalization of Poaching in Africa’, ilieleza kuwa tangu mwaka 2000 wizara inayohusika na utalii ilikuwa imetawaliwa na kashfa za rushwa. Ripoti hiyo ilifafanua jinsi vikundi mbalimbali vya waasi barani Afrika vinavyoendesha shughuli za ujangili.


Katiba ya Jaji Warioba
Oktoba 2014, Bunge Maalumu la Katiba lilipitisha Katiba Inayopendekezwa kwa tofauti ya kura mbili tu zilizonusuru kukwamisha Katiba hiyo kwa upande wa Zanzibar. Mvutano kati ya CCM na upinzani wakati wa upitishaji wa Katiba hiyo ulitokana na tofauti za itikadi na sera kuhusu muundo wa Muungano.


Wajumbe wa CCM walipigania sera yao ya muungano wa Serikali mbili wakati wenzao wa wapinzani walipigania muundo uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji mstaafu, Joseph Warioba wa Serikali Tatu. Hadi sasa haijapigiwa kura ya maoni.


‘Mchwa’ Serikalini
Kila mwaka, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amekuwa akikagua na kuibua ufisadi mkubwa katika Serikali Kuu, Idara za Serikali na mashirika ya umma. 

Ripoti iliyotolewa mwaka huu inaonyesha ukaguzi ulifanyika katika taasisi 176 za Serikali kuu, halmashauri 163 na mashirika ya umma 109. 

Kikwete amewahi kupangua baraza lake la mawaziri na kuwafukuza kazi watendaji lakini bado ufisadi umeendelea katika nyanja tofauti kama ulipaji mishahara hewa na ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo.


Mahakama ya mafisadi
Moja ya ahadi kubwa za Rais Magufuli wakati wa kampeni na Novemba 20 alipozindua Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano ni kuanzisha Mahakama Maalumu ya kushughulikia mafisadi.

Tayari mchakato umeanza lakini wachambuzi wanasema kinachotakiwa ni kuipa meno Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili iweze kufanya kazi zake bila kuogopa mtu.

KWELI HAPA KAZI TUUUUUU!!!!! WATUMISHI WENGINE WATATU WASIMAMISHWA KAZI TRA

$
0
0
SERIKALI imewasimamisha kazi watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao jana iliamriwa kwamba watahamishiwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.


Uamuzi huo umetolewa leo (Jumamosi, Novemba 28, 2015), na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ili kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazowakabili.

Kama ilivyo kwa wenzao sita waliosimamishwa kazi jana (akiwemo aliyekuwa Kamishna Mkuu), nao pia hawaruhusiwi kusafiri kwenda nje ya nchi hadi uchunguzi utakapokamilika.


“Kazi ya kuwachunguza ilianza jana ileile na sasa, tumeona hawa watu wanapaswa kuwa nje ya utumishi ili kupisha uchunguzi ufanyike kwa uhuru zaidi,” alisema Waziri Mkuu.


Pia Waziri Mkuu amemuagiza Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Philip Mpango atekeleze maagizo hayo kwa kuwaandikia barua watumishi hao.


Jana mchana, Waziri Mkuu alifanya ziara ya kushtukiza kwenye bandari ya Dar es Salaam akiwa na nia ya kukagua namna shughuli zinavyoendelea kwenye bandari hiyo hasa kwenye maeneo ya kupokelea mizigo kutoka nje ya nchi.


Katika kikao kilichofanyika bandarini hapo na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Serikali, Waziri Mkuu aliamua kuwasimamisha kazi maafisa watano na TRA kutokana na ‘upotevu’ wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.


Waziri Mkuu alisema upotevu huo unasababishwa na mchezo unaofanyika baina ya wafanyabiashara na watumishi wa TRA ambao wanaruhusu makontena kupita bila kulipiwa ushuru na hivyo kuikosesha Serikali mapato.

UPDATE!!!! ZITTO KABWE 'AKAABWA KOO' ZANZIBAR......APEWA SIKU 14 ZA KUOMBA RADHI KWA KUMHUSISHA DR. SHEIN NA MAKOSA YA UHAINI

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amepewa siku 14 kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa kumhusisha rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na makosa ya uhaini. 


Msimamo huo ulitolewa na wagombea wawili wa nafasi ya urais wa Zanzibar, Juma Ali Khatib (Tadea) na Soud Said Soud, walipokuwa wakizungumzia kauli ya Zitto kudai haikuwa sahihi kwa Rais wa Zanzibar kubakia madarakani wakati serikali yake imefikia ukomo wake Novemba 2, mwaka huu. 

Soud alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar Kifungu cha 28 (1)(a), Rais Shein ni Rais halali wa Zanzibar na atabakia madarakani hadi atakapochaguliwa rais mpya kwenye uchaguzi wa marudio. 

Alisema kuwa Dk. Shein alichaguliwa na wananchi wa Zanzibar na haikuwa haki kwa Zitto kumhusisha na makosa ya uhaini kwa kuendelea kubaki madarakani kwani yuko kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. 

"Zitto Kabwe afute kauli yake na kuwaomba radhi wananchi wa Zanzibar ndani ya siku 14 na asipofanya hivyo tutamfungulia mashitaka." alisema Soud pia Mwenyekiti wa Chama cha AFP. 

Katika sakata hilo, Juma Ali Khatib, alisema tayari ameanza kutafuta namna ya kuwasiliana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Zitto kwa kumhusisha na makosa ya uhaini Rais wa Zanzibar. 

Alisema iwapo Bunge litashindwa kumchukulia hatua za kinidhamu Zitto, yeye atalazimika kufungua kesi kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar kupinga kauli ya Zitto. 

Khatib alisema Zanzibar ni nchi na Rais wa Zanzibar lazima apewe heshima yake kwa sababu kuendelea kuwepo kwake madarakani ni matakwa ya Kikatiba. 

"Kumdhalilisha Rais wa nchi ni sawa na kutudhalilisha wananchi wake, rais anashauriwa na vyombo vingi vya sheria hivyo hawezi kuvunja Katiba," alisema Khatib 

Viongozi hao si wa kwanza kujitokeza kumtetea Rais wa Zanzibar kwani walitanguliwa na aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Rais ya Mabadiliko ya Katiba, Simai Mohamed Said, tangu Zitto alipotoa kauli kuwa Zanzibar haina rais na kuendelea kubakia madarakani Rais Shein ni sawa na kufanya uhalifu wa uhaini. 

Katika mkutano wake na wandishi wa habari hivi karibuni, Zitto alisema kwa sasa Zanzibar haina serikali na mtu yoyote anayejiita rais wa Zanzibar kikatiba amepindua nchi na katika hali ya kawaida anapaswa kushitakiwa kwa uhaini.

WARAKA WA KUFUTA ADA ELIMU YA SEKONDARI ( KIDATO CHA 1 HADI 4) NA MICHANGO YOTE ELIMU YA MSINGI

$
0
0
Serikali imeamua kutoa elimu pasipo malipo kwa elimumsingi kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne,kuanzia mwaka wa masomo wa 2016.

Azima hii ya serikali ni katika kutekeleza sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ina lengo la kuhakikisha kwamba watoto wote wa Tanzania wanapata Elimu bila kikwazo ikiwemo ada au malipo.


Katika kutekeleza maamuzi hayo,ada zote zilizokuwa zikilipwa kwa ajili ya elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne zimefutwa.Pia, waraka wa Elimu namba 8 wa mwaka 2011 kuhusu michango shuleni nao pia umefutwa.


Aidha, mwongozo wa elimumsingi bila malipo unaandaliwa na utatumwa kwa wamiliki wa shule ifikapo au kabla ya tarehe 15 Disemba 2015.

Waraka huu umeanza kutumika tarehe 21 Novemba 2015




SERIKALI KUDHIBITI UCHAPISHAJI WA KALENDA NA VITABU VYA KUMBUKUMBU KATIKA OFISI ZOTE ZA UMMA

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ametoa ufafanizi wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuhusu kupunguza matumizi yasiyo ya lazima katikaWizara,idara na Taasisi za serikali.


Katika ufafanuzi huo,Balozi Sefue amemtaka kila Mtendaji Mkuu ama Afisa Masuhuli wa serikali kujiuliza mwenyewe ni kwa kiasi gani anatekeleza kwa vitendo nia ya Rais ya kuepuka matumizi yasiyo ya lazima


"Rais ameonesha njia, sasa kwa wakati huu ni vema kila mtendaji mkuu wa serikali,ajiulize endapo Rais atafika katika eneo langu la kazi,ni kwa kiasi gani atakuta nimetekeleza maagizo yake?" Amesisitiza Balozi Sefue


Kutokana na ufafanuzi huo, Blozi Sefue pia amezungumzia uchapishaji wa kalenda na vitabu vya kumbukumbu yani "Diaries" akisema kila mtendaji mkuu wa Serikali ama Afisa Masuhuli apime mwenyewe kama ni lazima kutengeneza au kuchapisha kalenda na Diary? na kama ni lazima achapishe kwa kiasi gani?


"Ni matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kila wizara,Idara na Taasisi za serikali kuchapisha idadi kubwa ya kalenda na Diaries ambazo wakati mwingine hata hazitumiki mpaka mwaka unakwisha."Ameongeza Balozi Sefue


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam Novemba 28,2015

THROUGH HERE NEWSPAPER TODAY SUNDAY NOV, 29.2015 FOR STORY INFORMATION,GOSSIP SPORTS HARD NEWS

$
0
0

THROUGH HERE NEWSPAPER TODAY FRIDAY NOV, 27.2015 FOR STORY INFORMATION,GOSSIP SPORTS HARD NEWS




















.


.

UPDATES!!!! MAAMUZI MAPYA YA RAIS MAGUFULI KUHUSU SERIKALI KUPUNGUZA MATUMIZI YA FEDHA..

$
0
0


Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue ametoa ufafanuzi wa maagizo ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuhusu kupunguza matumizi yasiyo yalazima katika Wizara, idara na taasisi za serikali.

Katika ufafanuzi huo Balozi Sefue amemtaka kila mtendaji mkuu ama Afisa Masuhuli wa Serikali kujiuliza mwenyewe ni kwa kiasi gani anatekeleza kwa vitendo nia ya Rais ya kuepuka matumizi yasiyo ya lazima.

“Rais ameonesha njia, sasa kwa wakati huu ni vema kila mtendaji mkuu wa Serikali, ajiulize endapo Rais Magufuli atafika katika eneo langu la kazi, ni kwa kiasi gani atakuta nimetekeleza maagizo yake??” amesisitiza Balozi Sefue.

Kutokana na ufafanuzi huo Balozi Sefue pia amezungumzia uchapishaji wa kalenda na vitabu vya kumbukumbu yaani “Diaries” akisema kila Mtendaji mkuu wa Serikali ama Afisa Masuhuli apime mwenyewe kama ni lazima kutengeneza na kuchapisha kalenda na Diary? Na kama ni lazima achapishe kwa kiasi gani?

“Ni matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kila Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuchapisha idadi kubwa ya kalenda na Diaries ambazo wakati mwingine hata hazitumiki mpaka mwaka unakwisha” ameongeza Balozi Sefue.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam, Novemba 28, 2015

Na hii ndio nakala halisi ya barua toka Ikulu>>



KAMA ULIPITWA NA TUKIO HILI LA KUAGWA KWA MWILI WA MAREHEMU ALPHONCE MAWAZO...NIMEKUWEKEA HAPA KILA KITU JINSI ILIVYOKUA JIJIN MWANZA

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mhe. Freeman Mbowe akiaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.


Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Mh. Edward Lowassa akitoa heshima zake kwa mwili wa Mawazo.


Mawazo enzi za uhai wake.


Baadhi ya makamanda wa Chadema wakishiriki zoezi la kumuaga Mawazo leo.

MAELFU ya wananchi wa mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Mhe. Freeman Mbowe wameuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo, huku baadhi ya viongozi wa chama hicho, wakiwemo mawaziri wakuu wastaafu wakilitaka Jeshi la Polisi mkoani Geita kuhakikisha watu waliohusika na mauaji ya kiongozi huyo wanakamatwa na kufikishwa mahakamani mara moja.

Tukio la kuuaga mwili wa marehemu Alphonce Mawazo katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza limetanguliwa na ibada iliyoongozwa na Mchungaji Bernard Swai wa Kanisa la Winners.

Waziri Mkuu Mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu, Fredrick Sumaye pamoja na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Mh. Edward Lowassa wakatoa angalizo kwa Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha linatenda haki katika kushughulikia kifo cha marehemu Alphonce Mawazo.

Mtoto wa marehemu Alphonce Mawazo, Precious Mawazo mwenye umri wa miaka tisa naye ametokea mbele ya halaiki kuelezea majonzi ya kufiwa na baba yake mzazi.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe naye akatoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Alphonce Mawazo, aliyeuawa kikatili kwa kukatwa na mapanga na watu wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu katika Kijiji cha Katoro wilayani Geita.

Mwili wa marehemu Alphonce Mawazo tayari umewasili mjini Geita ambako utalala usiku huu ili kutoa nafasi kwa wananchi wa mkoa huo kutoa heshima zao za mwisho kesho Jumapili asubuhi ya Novemba 29, kabla ya kupelekwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Chikobe kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya Jumatatu Novemba 30.

Credit: ITV

IKULU: KATIBU WA WIZARA AMBAYE NI GOIGOI AJIONDOE MAPEMA

$
0
0
Joto la utawala wa Rais John Magufuli limebadili utendaji kazi wa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali waliozoea kukaa ofisini na sasa wanafanya kazi nje ya ofisi na kusikiliza kero za wananchi kwenye maeneo yao.


Wakati hilo likifanyika, Ikulu jijini Dar es Salaam imesema katibu mkuu au mtumishi yeyote wa umma atakayeshindwa kwenda na kasi na mabadiliko ya utendaji kazi katika serikali ya awamu ya tano ajiondoe.


Tamko hilo linalotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alipohojiwa jana kuhusu kutokuwapo kwa makatibu wakuu wa wizara kadhaa kwenye ofisini zao wiki iliyopita. 

Makatibu wakuu wa Wizara kadhaa wamelazimika kuzifunga ofisi zao na kuelekea mikoani kusikiliza kero za wananchi.


Hali ya viongozi hao kuhama jiji na kwenda mikoani imeleta mabadiliko ya utendaji kazi wao baada ya miaka ya nyuma kuzoeleka kutumia muda mwingi ofisini na kuacha kazi za nje kufanywa na waziri, naibu au watendaji wengine.


Baadhi ya wizara ambazo zilitembelewa na kukuta ofisi za katibu mkuu zikiwa zimefungwa ni Uchukuzi, Tamisemi, Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano na Ujenzi.


Baadhi ya wafanyakazi wa wizara hizo ambao hawakutaka majina yao yatajwe, walisema mabosi wao kwa sasa inakuwa nadra kuonekana ofisini wakifanya kazi kwa kuogopa kuonekana wazembe.


"Hatujawahi kuona katibu anakwenda mikoani kama ilivyo sasa, kila siku anakwenda huku na kule kuangalia miradi na kero za wananchi,"alisema mmoja wa wafanyakazi wa moja ya wizara hizo.



Hatuna Muda na Katibu Mkuu Goigoi-Sefue

Akitoa kauli ya serikali, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema kuanzia sasa katibu Mkuu na mtendaji wa serikali ambaye anafanya kazi kwa kusuasua ajiondoe mwenyewe.


Alisema tayari amefanya kikao na makatibu wote kuwaeleza suala hilo na atakayerudi nyuma hatakuwa na nafasi katika serikali ya awamu ya tano.


"Jambo hilo tumekubaliana kwenye kikao, serikali ya awamu ya tano haitakuwa na utani kwa wale watakaoonekana hawaendi na kasi ya Rais, sasa wanatakiwa kuchagua kama wanataka kuendelea na nafasi zao au la," alisema Sefue

VIONGOZI WALIOJIUZULU CHADEMA WAREJEA TENA

$
0
0
Viongozi wa Chadema Mkoa wa Rukwa waliotangaza kujiuzulu nyadhifa zao ndani ya chama hicho hivi karibuni, wamesitisha uamuzi wao na kurejea madarakani.


Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Frank Mwaisumbe alisema hayo juzi wakati akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu kutoka mkoani Mbeya.


Mwaisumbe alisema wamekubaliana na viongozi hao kurejea katika nyadhifa zao za kisiasa ndani ya chama hicho.


Alisema kikao baina ya viongozi wa Chadema wa kanda hiyo na waliotangaza kujiuzulu kilidumu kwa zaidi ya saa 11 juzi na kufikia uamuzi wa kurejea madarakani kwa viongozi hao.


Akizungumzia sababu za kujiuzulu kwa viongozi hao ambazo ni kutolipwa fedha mawakala wa wagombea wa chama hicho mkoa na kutoridhishwa na uteuzi wa mgombea ubunge wa viti maalumu, Aida Kenan, alidai zina mashiko lakini kabla ya kutangaza katika vyombo vya habari kuachia ngazi walipaswa kuwasiliana na uongozi wa juu wa chama.


Aliongeza kuwa, mathalan katika suala la mawakala kulikuwa na fomu maalumu ambazo wagombea walizijaza kuonyesha kuwa wanaweza kubeba gharama zote za mchakato wa uchaguzi au la.


Alisema wagombea waliojaza fomu kuonyesha hawana uwezo wa kuwalipa mawakala, chama kilibeba gharama hizo na fedha zilitolewa kwa kila mgombea kwa kuwa wao ndiyo walijua nani ni wakala na fedha hizo hazikupelekwa kwa viongozi wa mkoa kama inavyodaiwa.


Kuhusu uteuzi wa Kenan katika nafasi ya ubunge wa viti maalumu, alisema jina lake lilitokana na maombi ya Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) ambao walikuwa na nafasi mbili, lakini hakutokana na kura ambazo wagombea wa Chadema walipata kwenye Mkoa wa Rukwa.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa mkoa ambao awali walijiuzulu, Mwenyekiti Zeno Nkoswe na Katibu Ozem Chapita walikiri kukubali kurejea madarakani baada ya kufanya kikao na viongozi wa chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.


“Nimeafiki kurejea katika wadhifa wangu wa uenyekiti wa mkoa, lakini bado nawasubiri na viongozi wa kitaifa kuna mambo tuyaweke sawa. Si unajua wao wanatutuhumu kwamba tulikimbilia kwenye vyombo vya habari na sisi tuna hoja zetu,” alisema Nkoswe.


Baada ya makubaliano na viongozi hao walifanya kikao na madiwani waliochaguliwa kupitia chama hicho, ili kuhakikisha wanaongoza Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Chadema ina viti 10 kati ya 19 vya udiwani.

LOWASSA ACHARUKA : POLISI WASIPOCHUKUA HATUA KWA WALIOMUUA MAWAZO TUTACHUKUA HATUA WENYEWE

$
0
0
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua watuhumiwa wanaodaiwa kumuua aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo, likishindwa kufanya hivyo, chama kitachukua hatua chenyewe.


LOWASSA
Akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya kuuaga mwili wa Mawazo katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chadema na kuungwa mkono na vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, alisema polisi wasipochukua hatua kwa waliomuua mwenyekiti huyo, watachukua hatua wenyewe.


“Polisi wanafanya mambo yao ki-imra-imra, kwani magari ya washawasha yaliyonunuliwa kwa dola za Kimarekani milioni 282, hawana namna ya kuyatumia hivyo kuamua kuwachokoza wananchi ili waweze kuyatumia, sasa inabidi wachukue hatua kwa waliomuua Mawazo ama watachukua hatu wenyewe, “alisema.


Alisema baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kutoa haki kwa familia na chama hicho kumuaga Mawazo, imeonekana jeshi la polisi halina intelijensia wanayodai wanafanya.


Lowassa alisema hukumu ya Jaji Lameck Mlacha wa Mahakama Kuu, iwe somo kwa polisi wa Tanzania kutokana na kujawa wivu usiofahamika.


MBOWE
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alisema chama hicho kinajiandaa kumfungulia mashitaka ya madai Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, baada ya kuweka zuio la mwili wa Mawazo kutoagwa jijini Mwanza hadi Mahakama Kuu ilipotupilia mbali zuio hilo.


“Kamanda Mkumbo lazima alipe gharama zote za siku nane za kumweka Lowassa, Sumaye, Mbowe na wabunge zaidi ya 50 jijini Mwanza wakisubiri mahakama itende haki na hatimaye kushinda kesi, ”alisema mwenyekiti Mbowe.


Alisema haki imepatikana mahakamani na kuwaumbua polisi.
“Wananchi wamechoka kuuliwa kama ilivyotokea kwa wafuasi wa Chadema tangu mwaka 2011 mpaka sasa wakati huu wa Mawazo tumechoka kufa, mwenye akili na afahamu,ö alisema Mbowe.


Hata hivyo, alisema wapo baadhi ya askari polisi wema na wenye kutekeleza weledi wa kazi zao kiufasaha, lakini wapo ambao hawafai kuwatumikia na kuwaongoza wananchi.


Aliwashukuru watu waliojitolea kuisaidia familia ya marehemu Mawazo hasa mtoto wake Precious Mawazo (9) anayesoma darasa la nne akiwamo Lowassa pamoja na wabunge 113 wanaotoka vyama vya Ukawa, kwa kila mmoja kujitolea Sh. 300,000 na kupatikana milioni 36.


SUMAYE
Waziri Mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye, alisema Tanzania awali ilikuwa inasifiwa kwa amani na utulivu, lakini inawaua watu wanaodai haki.


“Hii ni kama ilivyokuwa Afrika Kusini wakati wa utawala wa Makaburu, mpigania haki Steve Bicco, aliuawa kama alivyouawa Mawazo, lakini mwisho wake makaburu hao walitoa haki kwa waliowengi licha ya kuwa na bunduki na polisi wengi kuliko kwetu, “alisema Sumaye.


Sumaye alisema marehemu Mawazo alikuwa akidai haki majukwaani, lakini watu waliotaka kudaiwa haki waliamua kumuua huku vyombo vya dola vikipindapinda ili haki isipatikane kwa amani.


MTOTO WA MAWAZO
Mtoto wa marehemu Mawazo, Precious (9), alisema waliomuua baba yake hawajakatisha ndoto yake ya kuwa mwanasiasa kwani siku moja atakuwa mwanasiasa mkubwa.


“Wakati wa uhai wa baba, ndoto yangu ilikuwa niwe mwanasiasa, lakini nitaendelea na hiyo ndoto hadi niwe mwanasiasa mkubwa nchini katuacha na mdogo wangu akiwa na miaka miwili tunaamini Mungu atatusaidia, “alisema Precious.


LEMA
Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, akitoa salamu za rambirambi uwanjani hapo, alisema marehemu Mawazo alikuwa rafiki yake wa damu tangu akiwa jijini Arusha na kumshawishi kuingia kwenye siasa, lakini aliuawa kinyama na watu wasiopenda haki.


Lema alisema ukimya wa wananchi katika mauaji wanayofanyiwa, si uoga bali unatokana na uchungu walionao, kwani wauaji wakiwa huru hakuna atakayekuwa salama.


MCHUNGAJI SWAI
Mchungaji Bernard Swai wa kanisa la Winners jijini Mwanza, akihubiri katika misa ya kumuaga, alisema wanadamu hawajumbwa na Mungu kwa ajili ya kuuana bali kupendana.


“Lazima wanadamu wajiulize kwanini vijana wengi wanatumiwa ili kuwaua wengine, tunaiomba serikali iliyopo madarakani isimamie na kukomesha kabisa mauaji yasiyo na hatia, “alisema Mchungaji Swai.


CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

JAMAA AUA WATU WATATU AKIWEMO MKE WAKE KISA MKE KUDAI AMEOKOKA HATAKI TENA MAPENZI

$
0
0

Polisi mkoani Ruvuma inamshikilia Amani Hyera (42), mkazi wa kijiji cha Kikunja wilayani Songea kwa tuhuma za kuwaua watu watatu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela, alisema tukio hilo limetokea juzi.

Alisema siku ya tukio Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Songea akiwa ofisini kwake, alipokea taarifa ya mauaji ya watu watatu.

Alisema anayedaiwa kufanya mauaji hayo ni Hyera, mkazi wa kijiji cha Kikunja.

Alisema mtu huyo anadaiwa kuwaua watoto wawili na mama yao kwa kuwakatakata mapanga kwa kile kilichosadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Alisema baada ya kufanya mauaji hayo, alijaribu kujiua kwa kujikata na panga shingoni, lakini hakufanikiwa kutokana na wananchi kufika kwenye eneo hilo la tukio na kumdhibiti. 

Kamanda Msikhela alisema mtuhumiwa anaendelea kupata matibabu na taratibu za kisheria zinafuata mara tu baada ya afya yake kuimarika.

Aliwataja waliouawa katika tukio hilo kuwa ni Ester Kadege (48), ambaye ni mama mzazi wa watoto waliouawa, Edson Msuha (6) na Kazed Kadege (13).

Alisema marehemu Ester alikuwa na watoto wawili ambao walizaliwa kwa baba tofauti ambapo uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa mtuhumiwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ester na baadaye waliachana kufuatia Ester kudai kuwa ameokoka na kwamba hataki tena masuala ya kimapenzi.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

UPDATES!!!! WALIOMUUA MAREHEMU ALPHONCE MAWAZO, TUZO YA MO, MTIKISIKO TRA, BABA ATEKETEZA FAMILIA..#MAGAZETINI

$
0
0

NIPASHE

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji maarufu kama MO, ameshinda tuzo ya “Mtu wa Mwaka” wa jarida maarufu la Fobes katika hafla zilizofanyika jijini, Johanesburg nchini Afrika Kusini.

Katika shindano hilo, Dewji alishindanishwa katika hatua ya mwisho na mke wa Rais wa Afrika Kusini ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Nkosazana Dlamini Zuma, Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari( aliyeanzisha vita dhidi ya rushwa).

Wengine waliokuwamo katika shindano hilo ni pamoja na Mwandishi maarufu wa vitabu wa Nigeria, Chimanda Ngozi Adichie, ambaye moja ya vitabu vyake vinaelezea picha halisi ya Afrika inavyofikiriwa duniani na Arumna Otei wa Nigeria pia ambaye ni makamu wa Rais wa benki ya Dunia.

Mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Dewji alisema tuzo hiyo anaielekezea kwa vijana wote wa Kitanzania kwani ndio nguvu kazi ya nchi katika kuubeba uchumi wa nchi.

Alisema tuzo hiyo si ya mkewe, baba, mama wala familia yao bali ni kwa Watanzania ambao wengi wao, wana ajira kupitia kampuni yake ama mashambani.

“Heshima yangu kubwa haitokani na utajiri, maana kama utajiri wako hauna msaada wala kugusa watu maskini hauna maana yeyote, hivyo basi heshima hii ni kutokana na kwanza bidhaa zangu kugusa maisha ya watu kila siku kuanzia sukari na majani ya chai asubuhi pamoja na unga wa ngano, lakini pia chakula cha mchana kwa unga wa sembe, mafuata ya kupikia na maji ya kunywa, bidhaa zote hizo za Mohammed Enterprises zinagusa maisha kila nyakati katika siku,” Dewji.

Alisema utajiri wake unaoonekana, umekuwa kwa kasi kubwa katika kipindi kifupi na hiyo ni kutokana na kufanya kazi sana tena kwa kisasa zaidi na kwamba kampuni zake zimekuwa zikifanya kazi kwa teknolojia ya juu ili kuendana na ushindani wa kibiashara unaobadilika kila siku.

NIPASHE

Polisi mkoani Ruvuma inamshikilia Amani Hyera, mkazi wa kijiji cha Kikunja wilayani Songea kwa tuhuma za kuwaua watu watatu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela, alisema tukio hilo limetokea juzi.

Alisema siku ya tukio Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Songea akiwa ofisini kwake, alipokea taarifa ya mauaji ya watu watatu.

Alisema anayedaiwa kufanya mauaji hayo ni Hyera, mkazi wa kijiji cha Kikunja.

Alisema mtu huyo anadaiwa kuwaua watoto wawili na mama yao kwa kuwakatakata mapanga kwa kile kilichosadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Alisema baada ya kufanya mauaji hayo, alijaribu kujiua kwa kujikata na panga shingoni, lakini hakufanikiwa kutokana na wananchi kufika kwenye eneo hilo la tukio na kumdhibiti.

Kamanda Msikhela alisema mtuhumiwa anaendelea kupata matibabu na taratibu za kisheria zinafuata mara tu baada ya afya yake kuimarika.

Aliwataja waliouawa katika tukio hilo kuwa ni Ester Kadege (48), ambaye ni mama mzazi wa watoto waliouawa, Edson Msuha (6) na Kazed Kadege (13).

Alisema marehemu Ester alikuwa na watoto wawili ambao walizaliwa kwa baba tofauti ambapo uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa mtuhumiwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ester na baadaye waliachana kufuatia Ester kudai kuwa ameokoka na kwamba hataki tena masuala ya kimapenzi.

NIPASHE

Serikali imesema bado wanakabiliwa na tatizo la uvuvi haramu hali inayosababisha samaki kutoweka katika maeneo yenye uvuvi.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Yohana Budeba, wakati wa mkutano wa utoaji tuzo kwa wajasiriamali wanaofanya shughuli za uvuvi na usindikaji salama wa bidhaa zao.

Alisema kuwa matumizi ya uvuvi haramu umeongezeka kwa kasi licha ya kwamba kuna sheria ambayo inakataza.

Dk. Budeba alisema sheria ya uvuvi inaelekeza nyavu zinazotakiwa kutumika katika kuvua samaki, lakini matokeo yake wavuvi hao wamekuwa wakitumia nyavu ambazo haziruhusiwi.

Alisema wavuvi hao wamekuwa wakivuna hadi mazalia ya samaki hali ambayo inasababisha kupotea kwa samaki katika maeneo yanayotumika kwa shughuli za uvuvi.

“Uvuvi haramu umeongezeka sana kwani wanatumia nyavu ndogo sheria ya uvuvi inaelekeza nyavu ziwe na macho ya aina gani hawa wanatumia chandarua ya kuzuia mbua kuvulia samaki, “alisema.

Aidha alisema mbali na changamoto hiyo, kumekuwa na idadi kubwa ya wavuvi wa samaki ambao hawaendani na hali halisi ya samaki waliopo.

Alisema kila anayepata mkopo anataka kuwekeza kwenye uvuvi bila kufikiria biashara nyingine na kusababisha idadi ya wavuvi kuongezeka.

“Wavuvi kuwa wengi nayo ni changamoto kwa upande wetu waliopo hawaendani na wingi wa samaki unajua mtu akipata mkopo wake ama akistaafu kazi wanakimbilia kuwekeza kwenye uvuvi, “alisema.

Alisema kupotea kwa dagaa wa Kigoma imesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa kwani maeneo mengine ya uvuvi yamekuwa makame.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo, Hosea Mbirinyi, alisema kukosekana kwa sheria inayowaongoza katika nchi nne ambazo zinaizunguka ziwa Tanganyika ni chanzo cha kuendelea kuwapo kwa uvuvi haramu.

Alisema wavuvi haramu huama kutoka eneo moja na kwenda eneo jingine wakifanya uvuvi kwa kukiuka sheria.

Aidha alisema kuna wavuvi ambao huvua dagaa kwa kutumia jenereta kwa ajili ya kuwasha taa ili wapate samaki wengi jambo ambalo halitakiwi.

Alisema nchi hizo nne zikikaa kwa pamoja na kuweka mikakati itasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti uvuvi haramu pamoja na kuwapo kwa ulinzi.

Naye Fatuma Katula ambaye anajishughulisha na ujasiriamali wa kuuza dagaa, alisema changamoto kubwa ambayo inawakabili ni upatikanaji wa vifaa pamoja na masoko.

Alisema mkutano huo umewawezesha kujifunza mbinu mbalimbali wanazotakiwa kuzitumia katika uvuvi wao.

MWANANCHI

Mamia ya wakazi wa Mwanza na mikoa ya jirani jana walijitokeza kwa wingi kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo, huku aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa akisema waliomuua mwanasiasa huyo wanajulikana na endapo polisi hawatawakamata, Chadema watachukua hatua wenyewe.

Heshima za mwisho za kuaga mwili wa Mawazo aliyeuawa Novemba 14 mkoani Geita kwa kushambuliwa na watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM, zilitolewa jana katika Uwanja wa Furahisha kuanzia saa tano asubuhi hadi saa tisa alasiri.

Utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa Mawazo ziliongozwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyekuwa ameambatana na Waziri Mkuu mstaafu,Frederick Sumaye, Lowassa na viongozi waandamizi wa chama hicho wakiwamo wabunge zaidi ya 50 wa Ukawa.

Akizungumza wakati wa kutoa salamu za rambirambi, Lowassa alisema; “Mawazo ameuawa kinyama, polisi wasipochukua hatua kwa watu waliyofanya mauaji hayo tutachukua hatua wenyewe.” Aliongeza: “Imeshaelezwa kwamba wahusika wanajulikana tena kwa majina, sasa watu hawawezi kusubiri haki kama wanaona vyombo husika vya kutenda haki vinashindwa kufanya kazi yao.”

Akizungumzia tukio la kuzuiwa kuaga mwili huo hadi kwa amri ya Mahakama, Lowassa alisema kinachofanywa na polisi ni kutafuta uhalali wa kutumia fedha za wananchi walizozitumia kununua silaha ambazo zilishindwa kufanya kazi wakati wa uchaguzi.

“Hapa kulitolewa sababu za kipindupindu ili watu wasiage mwili wa Mawazo, lakini sababu hizo zilikuwa ni uongo mtupu.. hakuna cha kipindupindu wala nini.

Mahakama imetenda haki, hata Biblia inasema waacheni watu wazike wafu wao, uamuzi wa Mahakama Kuu itakuwa somo kwa nchi nzima, mimi nampongeza jaji aliyeruhusu watu kumuaga Mawazo,” alisema Lowassa.

Wakati Lowassa akisema hayo, Sumaye alisema haki isipopatikana kwa amani itapatikana kwa njia nyingine, huku akitoa mfano wa askari wa makaburu walivyowakandamiza watu wa Afrika Kusini, lakini walipoamua kutafuta haki walifanikiwa kuwatoa.

“Mimi ni mgumu sana kutoa machozi, hata baba yangu alipofariki sikutoa machozi, lakini leo nimetoa machozi kwa sababu nchi ambayo ilikuwa na misingi ya amani, leo tunashuhudia watu wanaodai haki wanauawa, ni jambo la kusikitisha,” alisema Sumaye.

Aliwataka waombolezaji wasimamie amani lakini wasikubali kuonewa, kwa kuwa ni lazima wapinge dhuluma.

HABARILEO

Wazee wanaoishi katika kituo cha kulea wazee kinachomilikiwa na serikali kilichoko Kilima Bukoba Vijijini, wanalazimika kulala katika bweni moja wanaume na wanawake baada ya jengo la wazee wanawake kuezuliwa na upepo miaka minane iliyopita.

Wakizungumzia hali hiyo wazee wanaoishi katika kituo hicho walisema kuwa tangu jengo la wazee wanawake lilipoezuliwa na upepo hadi sasa wanalazimika kukaa katika jengo moja.

Mwenyekiti wa Wazee kambini hapo, Evarister Kayogera alisema kuwa nyumba ya kulala wazee wanawake iliezuliwa muda mrefu, serikali haijairekebisha na kwamba huwa wanakuja wanaangalia tu wanaondoka hawarudi, hivyo hawafahamu lini serikali italirekebisha ili wanawake wahamie katika jengo lao ili waache kubanana sehemu moja.

Mbali na tatizo hilo mzee Kayogera alisema wamekuwa wakikosa usafiri wa kupelekwa hospitali na wakati mwingine wakipelekwa wanapimwa na kuandikiwa dawa na kuambiwa kuwa hazipo waende kununua mitaani wakati wao hawana kipato chochote.

“Wahudumu wetu wakiwa na fedha ndiyo huwa wanachanga na kutununulia dawa, na wakati mwingine wakiwa hawana fedha wanatafuta dawa za kienyeji mbugani wanachemsha wanatupa tunakunywa ili tuone kama tutaendelea kuishi,” alisema.

Mzee mwingine John Rwiza alisema kuwa ni muda mrefu sasa kituo hicho hakina mafuta ya taa hali inayosababisha kula na kulala gizani, kutokana na kutokuwa na umeme.

Rwiza alisema chakula cha usiku wanalia gizani hawana mafuta ya taa na kwamba wanapika chakula mfano wali usio na mafuta wanachemsha tu na maharage hayawekwi chochote, wanakunywa uji usio na sukari na hawana pa kujisaidia.

HABARILEO

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ametoa ufafanuzi mpya kuhusu maagizo ya Rais John Magufuli, kwa watendaji wakuu na maofisa masuhuli wote wa wizara, idara na taasisi za Serikali, katika suala zima la kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma.

Katika ufafanuzi huo uliotumwa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Balozi Sefueametaka kila mtendaji wa Serikali kujihoji mwenyewe, kwamba endapo Rais Magufuli ataamua kufika katika eneo lake la kazi, ni kwa kiasi gani atakuta ametekeleza maagizo yake.

“Rais ameonesha njia, sasa kwa wakati huu ni vyema kila Mtendaji Mkuu wa Serikali, ajiulize endapo Rais Magufuli atafika katika eneo lake la kazi, ni kwa kiasi gani atakuta nimetekeleza maagizo yake,” ameeleza Balozi Sefue katika ufafanuzi huo.

Akiingia kwa ndani, Balozi Sefue ametoa mfano wa uchapishaji wa kalenda na vitabu vya kumbukumbu (diaries) na kutaka kila Mtendaji Mkuu au Ofisa Masuhuli wa Serikali, apime mwenyewe kama ni lazima kutengeneza na kuchapisha vitu hivyo na kama kuna ulazima, wachapishe kwa kiasi gani.

“Ni matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kila wizara, idara na taasisi za Serikali kuchapisha idadi kubwa ya kalenda na diaries ambazo wakati mwingine hata hazitumiki mpaka mwaka unakwisha,” alisema Balozi Sefue.

Kadi, sherehe Ufafanuzi huo umekuja baada ya hatua mbalimbali kuchukuliwa na Dk Magufuli katika kubana matumizi ya fedha za Serikali yasiyokuwa ya lazima, ikiwemo kupiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Magufuli wiki hii alipiga marufuku wizara, idara au taasisi za umma kuchapisha kadi hizo kwa kutumia fedha za Serikali.

Badala yake, aliagiza fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji wa kadi hizo, zitumike kupunguza madeni ambayo wizara, idara na taasisi hizo zinadaiwa na wananchi, wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine ya kipaumbele.

Mbali na kadi, pia alizuia kufanyika kwa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyotarajiwa kufanyika Desemba mosi mkoani Singida, na badala yake fedha za sherehe hizo zitumike kununulia dawa za kupambana na makali ya virusi vya Ukimwi kwa wagonjwa.

Safari za nje Ukiacha kuzuia uchapishaji wa kadi, Novemba saba mwaka huu, Rais Magufuli, alitangaza kuzuia safari za watumishi wa umma nje ya nchi, kutokana na ukweli kuwa safari hizo zimekuwa zikigharimu mabilioni ya fedha pasipo kuzingatia umuhimu kwa maslahi ya Taifa.

Kutokana na hatua hiyo, Rais aliamuru mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania, watumike kwenye mikutano ya kimataifa au shughuli zilizokuwa zikitakiwa kufanyika nje ya nchi.

Kwa waliokuwa na ulazima wa kwenda safari za nje, Rais Magufuli alitaka wafuate kibali kwake mwenyewe au kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue. Sherehe ya wabunge Jitihada za kuzuia matumizi ya Serikali za Dk Magufuli, zilifika mpaka kwa wabunge baada ya kuagiza fedha zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla ya kuwapongeza, zipelekwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda vya wagonjwa.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa, wadau mbalimbali walikuwa wamechanga Sh milioni 225 kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge katika siku ya uzinduzi wa Bunge. Alitoa maagizo kuwa kiasi kidogo tu cha fedha ndicho kitumike kwenye hafla hiyo na sehemu kubwa ipelekwe Muhimbili, ili zikatumike kununulia vitanda vya wagonjwa.

Siku chache baada ya uamuzi huo, fedha hizo zilitolewa na Katibu wa Bunge kwenda Bohari ya Dawa (MSD), ambao walinunua vitanda 300, viti maalumu vya wagonjwa 30, vitanda maalumu vya kubebea wagonjwa 30, mashuka 1,695 na mablanketi 400 kwa ajili ya wagonjwa. Sherehe za Uhuru Eneo lingine ambalo limekumbwa na hatua za kupunguza mapato ya Serikali, ni sherehe za miaka 54 ya Uhuru, ambazo zimekuwa zikifanyika Desemba 9, kila mwaka.

Rais Magufuli amezuia kufanyika kwa sherehe hizo mwaka huu na kuamuru siku hiyo itumike kufanya kazi ikiwemo usafi kwenye maeneo mbalimbali nchini, ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, wananchi hawapaswi kusherehekea miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara, huku wakiendelea kufa kwa ugonjwa huo unaosababishwa na uchafu.

Aidha, fedha zilizokuwa zitumike kugharamia sherehe hiyo, sasa zitapangiwa matumizi mengine ya maendeleo hususan kuboresha huduma za afya.

Vikao kwa televisheni Hatua zingine za kupunguza matumizi zilizochukuliwa na Serikali ni pamoja na katazo la maofisa wa Serikali kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kwa ajili ya vikao vya kazi, ambalo limewahusu wakurugenzi, makatibu tawala wa mikoa na wilaya pamoja na wafanyakazi wengine wa umma.

Badala yake watumishi hao wametakiwa kufanya mikutano kwa kutumia mfumo wa mawasiliano kwa njia ya video, ili kupunguza gharama za kuendesha vikao hivyo, kwa sababu washiriki wataunganishwa kwa mfumo wa video wakiwa kwenye vituo vyao vya kazi. Maofisa wa TRA Katika hatua nyingine, maofisa watatu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) ambao Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, aliagiza juzi wahamishwe kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa mingine, jana aliwabadilishia maelekezo na kupewa adhabu ya kusimamishwa kazi.

Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, iliwataja maofisa hao kuwa ni Anangisye Mtafya, Nsajigwa Mwandengele na Robert Nyoni.

“Kazi ya kuwachunguza ilianza jana ileile na sasa, tumeona hawa watu wanapaswa kuwa nje ya utumishi, ili kupisha uchunguzi ufanyike kwa uhuru zaidi,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa katika taarifa hiyo.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Philip Mpango atekeleze maagizo hayo kwa kuwaandikia barua watumishi hao.

Kwa hatua hiyo, watumishi waliosimamishwa kazi mpaka jana, wamefikia tisa kutokana na kashfa ya kupotea kwa makontena 349 yaliyopita bandarini, lakini hayakulipa kodi ya Serikali yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 80.

Wengine waliosimamishwa kazi juzi ni pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade, aliyechukuliwa hatua hiyo na Rais Magufuli na nafasi yake kukaimiwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dk Mpango.

Waliowekwa mahabusu Mbali na hao wanne ambao wamesimamishwa kazi tu na kuzuiwa kusafiri nje ya nchi, kwa kunyang’anywa hati zao za kusafiria, Waziri Mkuu Majaliwa pia juzi aliwasimamisha vigogo wengine kazi, lakini adhabu yao ikawa kubwa kidogo baada ya kukabidhiwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu.

Vigogo hao waliosimamishwa na kuwekwa rumande ni Kamishna wa Forodha, Tiagi Masamaki, Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja, Habibu Mponezya, Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Haruni Mpande, Hamisi Ali Omari (hakutaja ni wa idara gani) na Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu (ICD In-Charge), Eliachi Mrema.

MTANZANIA

Mkazi wa Ngulelo, Arusha Neema Obedi amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kumtukana Zubeda Efasi kuwa ni mgumba, hana kizazi na alichonacho hakina faida, hivyo angemwazima chake ilia pate watoto.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na hakimu Smathon Joseph wa mahakama ya mwanzo ya Maromboso Mkoani Arusha.

Hakimu alisema mshtakiwa huyo alimfuata mlalamikaji na kumtolea matusi hayo huku akijua ni kinyume na sharia na kutakiwa kwenda jela miezi sita na kulipa faini ya shilingi 300,000.

“Matusi hayafai mbele ya jamii, hii ni aibu kutoa maneno mazito kama hayo kw akuwa sote tumetokana na mwanamke, hivyo anapaswa kuheshimiwa na haipendezi kutoa maneno mazito kama hayo”…

TAARIFA SAHIHI KUHUSU MABUNDA YA NOTI KWENYE NDOO ZINAZENDELEA KUZAGAA MITANDAONI

$
0
0
Habari zilizosambaa mitandaoni kuhusiana na mabunda ya noti za dola ya Kimarekani kuwa zimekutwa nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa wa mtandao wa wizi bandarini na TRA sio za kweli, 
Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha.Ukweli ni kwamba mabunda hayo ya noti yalikamatwa huko jijini York, Portland, Marekani Mwezi Septemba mwaka 2010, na sio hapa Dar es salaam, Tanzania kama ambavyo wadau wengi wa mitandao hasa ya Whatsapp na Instagram wanavyovumisha.
Tumelazimika kutoa habari hii ili kuokoa wadau wetu wengi katika vuguvugu hili la uvumi wa mitandaoni ambayo hupelekea kazi kuwa ngumu kwa wengi wetu tunaotafuta na kutoa taarifa za uhakika na ukweli. Maana samaki mmoja akioza wote huonekana wameoza.
Vile vile hii ni kuwafumbua wale wote wanaohusika kusimamia na kutekeleza sheria ya mitandao wawe macho na kuanza kuchukua hatua madhubuti ili kupunguza kama si kuondoa kabisa tabia hii mbaya ya kusema uwongo kila kukicha.

BREAKING NEWZZZZZ!!!! TAARIFA YA UPOTEVU WA MAKONTENA AZAM ICD TOKA SSB GROUP OF COMPANIES

$
0
0
Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyoripotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake ya Bandari ya Dar es salaam hivi karibuni.
Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa na kampuni hio ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika katika sakata hilo. Isipokuwa kumetokea upotevu wa makontena yaliyoingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la kuhifadhia makontena(ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo la Azam ICD.
Aidha imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kampuni hiyo (SSB Group of Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika na upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.


SSB Group of Companies



Corporate Affairs Department



November 29, 2015

CHANZO MICHUZI BLOG

THROUGH HERE NEWSPAPER TODAY MONDAY NOV, 30.2015 FOR STORY INFORMATION,GOSSIP SPORTS HARD NEWS

NEWS ALERTS!!!! LOWASSA, MBOWE WATUA ALIPOUAWA ALPHONCE MAWAZO

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho Mhe. Edward Lowassa pamoja na viongozi mbalimbali wakitazama eneo ambalo Alphonce Mawazo alifanyiwa kitendo ya kinyama cha kukatwakatwa mapanga na watu wanaosemekana ni wafuasi wa CCM ikiwa ni umbali mchache kutoka kutuo cha polisi na ofisi za CCM katika barabara kuu inayoelekea Geita kutokea Busanda. 

Umati mkubwa wa wakazi wa Jimbo la Busanda waliojitokeza kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mgombea ubunge na M/kiti wa Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.
Mwili wa Marehemu Alphonce mawazo ukipokelewa na wakazi wa jimbo la Busanda ambako alikuwa akiwania Ubunge katika jimbo hilo




WAZIRI MKUU: TUMEDHAMIRIA KUWATUMIKIA WATANZANIA...TUTAHAKIKISHA MAPATO YA TAIFA YANATUMIKA KWA MASLAHI YA WATANZANIA WOTE

$
0
0
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya wachache.
Alitoa kauli hiyo jana mchana (Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Serikali imeanza kukabiliana na upotevu wa mapato ya Serikali na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma. Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama mapato ya nchi, kikusanywe na kitumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi wa Watanzania wote na si kwa watu wachache,” alisema. 

Akifunga maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kupambana na maovu yote na kuondoa kero zinazowaumiza wananchi wa kawaida.

“Wako watu wanaoamini kwamba hatuwezi, nawaomba waondoe hiyo dhana. Wako watu wanaodhani kwamba kwamba utawala huu ni wa watu wapole, nao pia waondoe hiyo dhana,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya waumini waliohudhuria sherehe hizo zilizoanza Novemba 27, 2015. 


“Tunawaomba Watanzania wote mtuunge mkono kwenye vita hii na mtuwezeshe kuifanya kazi hiyo. Tunaomba waumini wote mtuombee katika sala zenu za kila siku ili tuweze kuongoza kwa haki na kuwaletea Watanzania wote maendeleo,” aliongeza. 

Akinukuu kitabu cha Mithali sura ya 29 mstari wa pili, Waziri Mkuu alisema: “Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua. Mtuombee viongozi wenu tuwe waadilifu na wenye kutenda haki. Nasi tutaendelea kuwa waadilifu ili watu wetu wasigue,” alisema.

Aliwataka viongozi wa kanisa hilo waendelee kuisaidia Serikali katika kujenga kundi la watu wenye maadili mema ili walisaidie Taifa kuwa na watu waadilifu na hivyo kupunguza kero nyingi zinazoikabili jamii.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini wa kanisa la hilo kutoka mikoa mbalimbali, Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT, Askofu Silas Kezakubi alisema Kanisa hilo litaendelea kumuombea Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake ili wawe na afya njema, wawe na hekima na kuahidi kwamba wataendelea kuwaweka chini ya ulinzi wa Mungu siku zote.

Alisema wao kama kanisa wanaamini kwamba Serikali ya awamu ya tano ina nia ya kuwatumikia wananchi kwa bidii na uadilifu lakini akasisitiza kuwa siri ya bidii na uadilifu inapatikana kwenye neno la Mungu.

Akisoma risala ya kanisa hilo, Askofu wa AICT Dayosisi ya Kibaha, Askofu Charles Salalah alisema kanisa halina budi kushirikiana na Serikali kwa sababu wote wanawahudumia watu walewale isipokuwa katika malengo tofauti. 


Alisema kanisa hilo linahubiri maadili mema na bidii katika kazi kwa vile linaamini kuwa maendeleo hayadondoki kutoka juu wala hayaoti kama uyoga bali yanapatikana kwa watu kufanya kazi. 


Akisisitiza kuhusu uadilifu, aliwataka wazazi kudumisha ndoa zao ili watoto wapate malezi mema kutoka kwa baba na mama na kwamba baba na mama wasipokaa vizuri, watoto hawawezi kuwa waadilifu. 

“Wazazi tunao wajibu wa kupanda mbegu bora ya uzalendo kwa watoto wetu. Endapo tutapanda mbegu mbaya ya kuwagawa watoto wetu kwa itikadi tofauti, ni lazima tujue kuwa tutavuna tunachopanda.”

“Tukumbuke kuwa tunalo Taifa moja tu la Tanzania. Hata kama watoto wetu watakuwa na upenzi na vyama vyao, ni lazima tuwalee katika misingi ili wakue wakijua Taifa letu ni moja tu. Ndiyo maana tunaweka mkazo kwenye familia kwa sababu maadili mema yanaanzia nyumbani,”alisisitiza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, NOVEMBA 29, 2015.

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 ya Kanisa la Africa Inland Church Dayosi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiwa meza kuu na viongozi wa kanisa la Africa Inland Church wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015.
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim majaliwa akiwasha moja ya pikipiki tatu ili kuashiria mkakati wa kueneza injili wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 ya kanisa la Africa Inland Church Dayosisi ya Pwani kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 2674 articles
Browse latest View live