Yamoto Bendi.
UTAMBULISHO! Bendi ya Yamoto inatarajiwa kumtambulisha rasmi Mshindi wa Bongo Star Search (BSS 2015), Kayumba Juma, Desemba 19, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Mshindi wa Bongo Star Search (BSS 2015), Kayumba Juma
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mratibu wa shoo hiyo, Mohamed Seif ‘Mudy K’ alisema kuwa Yamoto pia wataachia ngoma mpya baada ya Cheza kwa Madoido ijulikanayo kama Imo.
“Kutakuwa na sapraiz kibao ambapo Baby J mara ya kwanza atatambulisha wimbo mpya,” alisema Mudy K na kusisitiza kuwa kiingilio kitakuwa shilingi 10,000 tu.